Gwajima hana jipya.
Maswali yake amekopi na kupesti kwa hao hao wazungu.
Wazungu wameulizana sana hayo maswali ya Gwajima. Na huko kwa wazungu bado wanauliza sana lakini sayansi sio kama dini mtu anaweza kufanya utafiti na kujua kama zina sumu au hazina.
Gwajima amekua Kama Kibwetere. Atapeta maafa makubwa sana kama ataendelea kuchochea watu kwenye mikutano na mikusanyiko yake kipindi hiki cha Korona.
Huwezi kuwa Mhubiri au Askofu halafu unashindwa kuhubiri habari za toba badala yake unatumia muda mwingi kuzungumzia siasa kwenye Taifa lililojaa Wazinzi ,walevi,wauaji, watu wanaoua waume zao au wake zao, watu wasioheshimu baba zao na mama zao, watu wanaotukana hovyo , watu wanaofanya biashara za vitu feki ,riba kubwa inayopira vipato vya watu, watu wasiowapenda majirani, watu wala rushwa, walawiti, mashoga, washirikina maRPC wanaobambika watu kesi, watu wenye chuki ,waonevu, mawaziri na watawala wasiolipa kodi na wote waliojaa maovu kwenye mioyo yao .
Sio watu wote wanaoweza kutembea juu ya maji kama YESU hivyo kuwaambia watu wasipande botia au meli kwa sababu tu YESU alitembea juu ya maji ni kuwadanganya huku ukijua kuwa watazama kwa sababu hawana imani kubwa.
Sent from my TECNO L8 Lite using
JamiiForums mobile app