Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
- Thread starter
- #121
Mzee summarize. Ongea kwa bullet points. You are using too much energyNinashangazwa sana na hawa watu wanaopinga chanjo bila kuwekea madhara yake kwamba tukichanja tutapatwa na madhara yepi
Na je wameingia maabara zipi kuthibitisha haya
kwa sababu ninachokiona kwa hawa ni uchonganishi wanaowafanyia wananchi dhidi ya kiongozi wao mkuu na ambaye ndiye Rais wa nchi kwa sababu yeye Rais anahamasisha chanjo kwamba raia wake wote wachache na hivyo hiyo ndiyo namna ya kupambana na korona na anawahakikishia na kuwashawishi kwamba kwa kufanya hivyo itawazuia kufa kwa Korona na kwa sababu yeye ndiye was kiongozi mkuu wengi wa wananchi watamwelewa na kuchanja ama kunao watakao kataa kuchanja kwa sababu kwamba wao wamewasikiliza watu wao wanaowaamini
lakini wakati ambao Rais na viongozi wengine wa serikali wakihasisha kuchanja anaibuka mtu mwingine ambaye anayo madaraka yake kwa kikundi ama kundi flani la watu naye anapingana na Rais na kusema kwamba tusichanje kwa sababu chanjo inayo madhara ambayo hayajaorodheshwa wala kutajwa kwenye mikutano ama matamasha wanayoyatumia katika kupingana na Rais na viongozi wengine wenye kuungana na Rais kwenye ushawishi wa kuchanja
sasa hapa kaswali kangu kadogo tu ni kwamba je hawa wapingaji wa chanjo siyo kwamba wanamchonganisha rais na wananchi wake? hapa kwa tafsiri nyepesi tu ni kwamba anawaambia wananchi ya kwamba rais anataka wananchi wafe ndiyo maana anawahamasisha wakachanje ili wafe je hii siyo hujuma na kukosa utii?
nashauri watu wa namna ya kina Gwajima vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kuhangaika nao kwa kuwashughulikia maana kwa sababu chanjo ni hiari ikiwa wao hawataki na wala hawamini ktk chanjo walipaswa kukaa kimya maadamu hawajalazimishwa kuchanja na wala kama siyo uchonganishi hawakupaswa kuwashawishi tena kwa waziwazi watu wengine kwamba wasichanjwe
wanapaswa kuyaheshimu madaraka ya Urais kwani Urais hauna mipaka katika kuongoza kwake
na pia nashauri ni wakati wa vyombo vya usalama kushughulika na hawa watu wa namna ya Gwajima kuwaelewesha ama kwa taratibu au kwa namna yeyote ya kwamba hawaruhusiwi kulitolea ufafanuzi wala tafsri ya kupingana ktk hili swala la kupambana na kuizuia korona na kwamba waelewe serikali haijasema kwamba imefungua mjadala wa chanjo ya Korona na kwa hivyo wao kama wao hawaruhusiwi kuliongelea kwa namna ya tofauti ama namna inayokinzana na Serikali katika swala hili na kwa yeyote atakayebainika akitoa tafsri yenye kupotosha kuchanjwa Korona atachukuliwa hatua kali za sheria
nakaa sana nawatafakari hawa watu najiuliza je wanayo nia gani? Kwa nini wanafanya haya?
napata jibu kwamba ni watu wenye tamaa mbaya za kimadaraka watu wasijali wenzao wala maisha ya wenzao na hapa ni kwamba wanatafuta tu kujulikana kwa ajili ya maslahi yao binafsi ya kisiasa siku za baadaye kwani kwa kupingana huku kwao pia kuko ktk hali ya kubahatisha na kama upigaji ramli kwamba ikiwa kama gonjwa halitakuwa na mlipuko kama tunavyoelezwa basi nao watajitokeza sasa na kusema kuwa wao ni manabii na walitabiri na sasa watu hawajakufa kama walivyotangaziwa wao watu wenye kufahamu mambo mengi na kumbe watu wakifa haina madhara kwao kwa sababu waliopaswa kuwahoji walishafariki
kwani nini wasituambie madhara yake kisayansi?
naomba serikali ije na mwarubaini kwenye hili swala.
Itoe onyo kali na ipige marufuku kabisa kwa vyombo ambavyo havina dhamana ya kusimamia afya za wanachi kuongelea ama kutafsri kwa njia ya tofauti na ile inayopendekezwa na kusimamiwa na serikali
na pia kwa sababu mtu kama Gwajima pengine kwa sababu zake za kimaslahi ndizo zilizopelekea yeye kuwepo kwenye siasa na hatimaye bungeni akiamini kwamba kunazo pesa nyingi zaidi ya alizokuwa anapata kwenye kuhubiri kwake na sana amegundua kwamba ni tofauti na alivyotegemea kwani kanisani ndiko kwenye pesa na sasa anataka kujiondoa kwenye siasa ili arejee kwenye kuhubiri kwa namna hii anakosa njia nzuri ya kujiondoa hivyo anaamua kujilipua kwa namna hii akitafuta kugombana na serikali ili serikali umuondolee hadhi ya ubunge
Namshauri mwenyekiti wa ccm ashauriane na uingozi wa chama ngazi za juu awashawishi wamkubali kumnyang’anya kadi ya ccm Gwajima na kumfukuza uanachama wa ccm hivyo kwamba apoteze sifa ya kuwa mbunge kwa sababu atakuwa hana chama na hivyo kuondokana naye ili aweze kurudi vizuri kwenye kazi yake ya mwanzo ambayo ni uchungaji
Naomba kwa leo niishie hapa kwanza.