ipo hivi
1.kitu cha kwanza watu wengi wanadhani pesa zinatoka kwa youtube, LA HASHA!! Youtube anasimamia malipo tu, youtube ni kama dalali maarufu anaewaunganisha wanaotaka kutangaziwa kwa mfano kwa hapa tanzania vodacom, tigo na makampuni mengine na hata wewe unaweza kuandaa tangazo lako ili utangaziwe bidhaa yako. youtube akipewa hilo tangazo atalipwa kwa kigezo cha kwa kila views elf 1,
youtube ataingia mkataba na wenye channel za youtube kama kina diamond, millardayo, middle simba, n.k kwa hiari yao wakubali kwamba matangazo ya vodacom yatakua yakionekana kwenye video zao kabla hazija play au pembeni mwa video, aina maarufu ya matangazo ni yale yanayoonekana kabla video haijaanza huwa kuna kitufe cha kuruka tangazo.
vodacom anaweza kulipa elf 4 kwa watu elfu moja wataoliona tangazo hapo youtube kwenye kabla hawajatazama video au pembezoni mwa video zinapocheza, youtube atachukua kama asilimia 30 ya hio elf 4 na diamond huchukua asilimia 70 ya mapato hayo, kwahio kwamfano video ya diamond ikionesha tangazo kwa watu milioni mfano kwenye video ya jeje, diamond atapokea kama milioni 30.
youtube wanalipa kulingana na tangazo limeonekana mara ngap sjo kwa idadi ya views, katika views milioni 1 tangazo linaweza kuonekana kwa watazamaji laki saba,