Hongera kocha wa Taifa Stars kwa kuwa mkweli. Taifa stars haijaenda AFCON kushindana

Hongera kocha wa Taifa Stars kwa kuwa mkweli. Taifa stars haijaenda AFCON kushindana

Watulie tu wacheze mpira, lolote linaweza kutokea, mbona Msumbiji wamewanyosha Egypt?, Cape Verde kamatandika Ghana, Namibia kamtandika Tuisia, Angola kadrw na Algeria
 
Mkuu hakuna watu Wanafiki kama sisi Waafrika yaani kuna watanzania leo wanasema kuwa tunakwenda kushinda ila kwenye mikeka tumempa Morocco 3+
 
Tunaingia kama underdogs hilo lipo wazi, kuwa underdog kuna faida nyingi kuliko hasara, mfano mzuri ni mechi ya EGYvsMOZ, hakuna aliyewapa Moz chance ila walimshangaza kila aliyeangalia ile game.
 
Kwani ulishawahi kuwasikia like playing in big European clubs like R. Madrid, Barca, PSG, Arsenal, Juve, Milan, Man City au hata Aston Villa tukiacha mbali zinazoshiriki daraja la pili UK au Bundasliga?🤣🤣🤣🏃🏃
Kwa nini unamchanganya aseno kwenye timu kubwa?
 
Amesema kuwa Shirikisho la Soka Afrika ( CAF ) linaipendelea sana nchi ya Morocco kwakuwa ni Taifa Tajiri na linaipangia Ratiba nyepesi ili Kuibeba katika Mashindano mbalimbali tofauti na nchi zingine ( ikiwemo yake ya Algeria ) ambayo inachukiwa na CAF.
Mpuuzi kweli, anataka kuichonganisha Tanzania kidiplomasia na nchi zingine, mpuuzi sana aondolewe maramoja
 
Jamaa ana kibri sana na ni jeuri mno achilia mbali dharau binafsi hua simkubali.
 
Ukweli lazima usemwe na ukweli humuweka mtu huru.

Kocha wa taifa stars anajua uwezo wa wachezaji wa taifa stars, hivyo ameamua kusema ukweli...."kwamba kwa kikosi hiki, taifa stars haitoboi. Hivyo tumekuja kutalii na kuwapa changamoto wachezaji kwa manufaa ya baadaye".

Tujifunze kuwa wakweli kama kocha wa taifa stars. Hivi kweli Kuna mtanzania anaamini taifa stars itavuka hata makundi? Kwa wachezaji gani?

Mungu mbariki kocha wa Taifa Stars.
Kama ni kweli amesema hivyo anatukosea sana sisi ccm hajui namna tulivyoangaika kushawi michango ya taifa stars ..
 
Kama ni hivyo Taifa Stars inakwenda Ivory Cost kufanya nini?
 
Back
Top Bottom