Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Sheria ya vyama vya siasa inamruhusu mtu yeyote, bila kujali rangi, jinsia, na vinginevyo, kujiunga na chama chochote apendacho, ilimradi akidhi vigezo vilivyopo kwenye chama husika atakapokwenda.
Hii ndio sababu ya Chadema kuwapokea wote, Lowassa na Shibuda, utambue Chadema sio chama cha mtu binafsi, au mali ya familia fulani, au kikundi fulani cha watu kama unavyodhani, mpaka unakuwa na mawazo ya kuwatenga wengine, Chadema ni Public Political Party.
Hapa suala la Shibuda kutoungana na wenzake kwenye shughuli za chama, au Lowassa kuitwa fisadi muda wote wa mikutano ya siasa waliyofanya Chadema miaka iliyopita, hayawezi kuwa na uzito wa kuvunja sheria kumkataa mwanachama anayetaka kujiunga nao, mawazo yoyote ya kutompokea mtanzania yeyote kwenye chama, yalikuwa ni potofu yaliyojaa uvunjifu wa sheria, ajabu huu upotofu umekaa nao kichwani mpaka leo, tena ndio unauita nondo zisizojibika!
Suala la ruzuku baada ya uchaguzi wa 2015 - 2020 kwamba kwanini hiyo pesa ya ruzuku haikujenga ofisi za chama..
Tabia za Magufuli baada ya kuingia madarakani hakuna asiyezijua, alianza kubana kila kona, sio tu kuwapora watu fedha zao, lakini alifikia mpaka kuzuia ruzuku kwa Chadema, na kama alikuwa akiitoa, hakuitoa kwa wakati, na kwa kiwango kile kilichotakiwa, sasa unapomlaumu Mbowe kutokujenga ofisi, ulitaka atoe pesa zake mfukoni?
Na kama angezitoa si ndio ungeanza kulalamika kwamba chama kinaendeshwa kwa fedha za Mbowe?!
Bora umekuja kwa id hii. Sina popote ninapokataa kumpokea yoyote ndani ya CDM, na wala sijawahi kukataa hilo. Msimamo wangu uko wazi, sio sahihi kumpokea mwanachama yoyote last minute, kisha kupewa nafasi ya kugombea, hasa inapokuwa nafasi ya urais, huku kikiwa na watu wake wa muda mrefu kwa nafasi hizo. Naheshimu utetezi wako, lakini jitahidi usipotoshe.
Kwangu hata wakihamia CCM wote ndani ya CDM ni sawa. Ila linapokuja suala la mtu kupewa nafasi ya uongozi, umakini unahitajika. Kwenye suala la Shibuda, Lowassa, Esther Bulaya nk umakini haukuwepo. Ila kwenye eneo la urais lile lilikuwa kosa la dhahiri, na lilidhihirisha CDM sio chama makini, na kikubwa hawana msimamo. Je ni sahihi CDM kuendelea kuwa chama cha kuokoteza viongozi wa dakika za mwisho?
Ni kweli tabia za Magufuli zilikuwa wazi hilo sina tatizo nalo kabisa. Na huenda fedha za ruzuku hazikuwa zikitoka kwa wakati ama zote. Je hazikutoka zote hata kama zilichelewa? Je kwanini hazikutumika kufanya hayo baada ya kutoka? Mbona CDM hawakusema kuwa pesa za ruzuku hazitoki, na wala ripoti ya CAG haikusema fedha kutokufika? Washauri CDM waseme ni kiasi gani hawakupokea fedha za ruzuku wakati wa Magufuli, na utaratibu ni upi ili kuondoa upotoshaji unaofanyika. Kinyume na hapo bado ninachosema kitabaki hivyo hivyo.
Sina popote ninapotaka Mbowe atoe fedha zake mfukoni, ndio maana nilishangaa hivi majuzi akisema ametumia mabilioni kadhaa ndani ya CDM, japo hakusema pia alipata mabilioni mangapi akiwa ndani ya CDM. Mpaka kufikia hapa, post yangu namba 92 hujaipa majibu stahiki, labda kama utarudi na hiyo id mpya ili utoe majibu stahiki.