Hongera Mbowe umeshinda mchezo wa kisiasa


Bora umekuja kwa id hii. Sina popote ninapokataa kumpokea yoyote ndani ya CDM, na wala sijawahi kukataa hilo. Msimamo wangu uko wazi, sio sahihi kumpokea mwanachama yoyote last minute, kisha kupewa nafasi ya kugombea, hasa inapokuwa nafasi ya urais, huku kikiwa na watu wake wa muda mrefu kwa nafasi hizo. Naheshimu utetezi wako, lakini jitahidi usipotoshe.

Kwangu hata wakihamia CCM wote ndani ya CDM ni sawa. Ila linapokuja suala la mtu kupewa nafasi ya uongozi, umakini unahitajika. Kwenye suala la Shibuda, Lowassa, Esther Bulaya nk umakini haukuwepo. Ila kwenye eneo la urais lile lilikuwa kosa la dhahiri, na lilidhihirisha CDM sio chama makini, na kikubwa hawana msimamo. Je ni sahihi CDM kuendelea kuwa chama cha kuokoteza viongozi wa dakika za mwisho?

Ni kweli tabia za Magufuli zilikuwa wazi hilo sina tatizo nalo kabisa. Na huenda fedha za ruzuku hazikuwa zikitoka kwa wakati ama zote. Je hazikutoka zote hata kama zilichelewa? Je kwanini hazikutumika kufanya hayo baada ya kutoka? Mbona CDM hawakusema kuwa pesa za ruzuku hazitoki, na wala ripoti ya CAG haikusema fedha kutokufika? Washauri CDM waseme ni kiasi gani hawakupokea fedha za ruzuku wakati wa Magufuli, na utaratibu ni upi ili kuondoa upotoshaji unaofanyika. Kinyume na hapo bado ninachosema kitabaki hivyo hivyo.

Sina popote ninapotaka Mbowe atoe fedha zake mfukoni, ndio maana nilishangaa hivi majuzi akisema ametumia mabilioni kadhaa ndani ya CDM, japo hakusema pia alipata mabilioni mangapi akiwa ndani ya CDM. Mpaka kufikia hapa, post yangu namba 92 hujaipa majibu stahiki, labda kama utarudi na hiyo id mpya ili utoe majibu stahiki.
 
Nakushukuru kwa maoni yako yenye wingi wa busara. Tuje hapo kwa Lowassa. Nitaanzia hapo hapo kwa Shibuda. Ifahamike Shibuda alikuwa bungeni kama mbunge wa CDM, lakini aliyekuwa hashirikiani na cdm tena kiutendaji.
1. Shibuda nilikutolea kama mfano tu. Lakini wako wengi tu waliopokelewa na wengi wakawa wa manufaa. Hata Mzee Edward Lowassa aliipa faida CHADEMA unless uwe kipofu kutoona. Lowassa na CHADEMA Kwa ujumla kutoshinda U - rais mwaka 2015 sababu siyo Mbowe.

Sababu ni mfumo mbaya unaosimamia chaguzi Kwa kujengwa ktk mfumo mbaya wa kikatiba na kisheria. Chini ya mfumo huu hata kama ungemfanya John P. Magufuli awe mgombea wa CHADEMA mwaka huo wala asigeshinda.

Na ukidhani kuwa akiondoka Freeman Mbowe CHADEMA bila kuubadili mfumo wa uchaguzi Kwa kuubadili sheria na katiba basi mambo yanabadilika na CHADEMA kutawala nchi hii, utakuwa unajidanganya na ni wazi unakuwa huna macho ya kuona tatizo lipo..

2. So long as ume - highlight yaliyokuwa mapungufu ya Shibuda, niseme kidogo hapo. Kwamba, ukiongoza kundi kubwa la binadamu lenye watu wenye tabia na hulka tofauti tofauti, tegemea lolote toka Kwa yeyote.

Ndani yake watakuwepo wenye tabia za ukorofi, ubishi, wagomvi, wasiopenda kushirikiana, wazinzi, waasherati. waongo, wasio na uvumilivu, wambea, wazushi nk nk..

Lakini wote ni wako na lililo muhimu ni kujua namna njema ya kwenda nao. Ndiyo maana ili uwe kiongozi wa taasisi kubwa kama CHADEMA, unapita ktk chekecheo kwanza. Freeman Mbowe ana sifa hizo na amefanikiwa sana kuiongoza CHADEMA Kwa ufanisi.

Ilifika mahali tukawa tunajiapiza kuwa tusirudie tena kuokota wañaccm tena kwa njia ya voda Fasta. Mbona 2015 ndio tukafanya kosa kubwa kuliko la huyo Shibuda?
1. Chama hakikujiapiza. Labda ulisikia mtu mmoja akijiapiza ukadhani ni chama na sasa una - misinterpret mambo. Kumbuka chama cha siasa ni watu wote iwe wabaya au wazuri hata kama wanatoka chama kingine kikiwemo CCM, wote ni watu

2. CHADEMA hakikufanya ubaya wowote kukaribisha wanachama wapya mwaka 2015 toka CCM akiwemo Edward Lowassa. Kumbuka nimesema, chama cha siasa ni watu. Edward Lowassa ni mtu. Kutofikiwa Kwa matarajio (expectations) hilo ni jambo jingine linalohitaji mjadala tofauti.

Usichanganye mambo. Usiongozwe na hisia na mapenzi yako binafsi ktk kufanya judgement ya mambo haya. Tuongozwe na facts..
Hapa sasa ndio nakuona Tindo halisi..

Yaelekea Tindo huzielewi siasa za ulimwengu wa tatu. Katika siasa za huko ndugu Tindo, adui yako sasa kiuhalisia ndiyo rafiki yako baadae au kesho na kinyume chake ni hivyo hivyo..

Unashangaa hili?

Mbona humshangai Dr Wilbroad Slaa aliyeituhumu CCM na viongozi wake na baadae kuungana nao kufanya kazi zao huko CCM?

Mbona huwashangai kina Sumaye, Lowassa na wengine waliotoka CCM kuja upinzani kwa kuwananga wenzao huko walikotoka yaani CCM na leo wapo meza moja hukohuko CCM wanakula pamoja na kina Kasheku Msukuma, Nnape Nauye, Lusinde nk nk ambao wakati wanatoka CCM kuja CHADEMA mwaka 2025 waliwarushia kila aina ya tusi hawa wazee?

Wenzako CHADEMA walishatoka kuwaza na kufikiri kama unavyofikiri wewe. Wenzio waruka Kwa masafa ya 5G wewe bado uko kwenye frequency za 2G..!

Namna ya kufikiri na kufanya siasa inabadilika Kila siku Tindo. Wewe umeachwa maili nyingi nyuma, Anza sasa kukimbia ili uende sambamba na wenzako..!!
Haya siyajui..

Naamini hata wewe hujui lolote isipokuwa unasukumwa na "kufikiri" tu huku ukiwa huna facts zinazosimama kama "base" ya hoja yako..

Kwa sbb kila mtu angetarajia ujadili mapato na matumizi ya fedha za CHADEMA, ukiwa unajua mapato Yao halisi, bajeti yao, vipaumbele vya kitaasisi nk nk..

Lakini wewe huna haya badala yake Unataka tujadili hersays za kwenye vijiwe vya kwenye kahawa. Hizi sio facts bali ni propaganda na uzushi tu. Mimi siko huko..!
Je katika mazingira hayo, unawezaje kusema mwenyekiti huyo ni bora, na anastahili kufumbiwa macho hata baada ya kukaa muda mrefu?
Unadhani sio Bora kumbe? Kwangu Mimi ni Bora sana. Amefanya mengi mazuri na makubwa. Ndiyo maana unamjadili
1. Asante Kwa ku appreciate ingalau Kwa kidogo alichofanya..

2. Hayo mengine ni yako. Mimi naheshimu na tutafika tu huko tuendako
Ni hatari kubwa kwa taasisi kama hiyo kuwa na mtazamo wa kiongozi wa muda mrefu, kwa kichaka cha siasa za Afrika.
Hakuna hatari bali ndiyo taasisi hiyoooo inakua na kuendelea kuishi na kuwa tishio.
Je akifariki hiyo taasisi itakuwa mwisho wake, maana hiyo taasisi haitahamia ulaya?
Basi subiri afe. Lakini usishangae pia ukaanza kufa wewe..!

All in all, CHADEMA has millions of members all over the country and the world at large wenye uwezo pengine kuliko uwazavyo.

Kwa sasa tunasema, FREEMAN MBOWE anatosha.

Tatizo lako ni hili. Huijui CHADEMA..!!
Kama tunaimani hiyo kuhusu Mbowe, ni kwanini tunataka kuitoa CCM

Haa haa, hujui ni kwanini?


Una maana Mbowe/CHADEMA na CCM ni kitu kimoja? Kwa hiyo CCM isitoke siyo?

If that's the case, kulalamiko kote huku sababu yake ni ni..? Unajua sikuelewi..

na tunashangaa inaposema haimini kama chama kingine kitaweza kuongoza nchi?
Hizo ni siasa tu..

Ndugu Tindo, kama umeamua kuwa kwenye siasa, basi jitahidi kujua michezo ya kisiasa inavyochezwa vinginevyo utapata shida sana kuwaelewa wanasiasa ili uendane nao..


Ni Kwa sababu nakuwa kwenye majukumu mengine boss..

But here I am now. Na natumaini utanielewa..

Asante, tuendeleee na mjadala..
 
Jamaa una vituko sana, una ushahidi gani kwamba nina Id zaidi ya moja huku? kama upo hebu uweke hapa, unaishi kwa hisia tu[emoji3][emoji3][emoji3] jitahidi kuwa realistic, hili sio jukwaa la hisia, huu mtazamo wako ni sawa na kuamini watu hawawezi kufanana mitazamo huku, au wakifanana, basi ufanane wewe tu, na wale wa kundi lako, badilika!

- Issue yako ya Lowassa kupokelewa na kugombea muda mfupi baada ya kupokelewa, wewe unaona ule uamuzi ulikuwa mbaya, lakini kwangu uamuzi wa kumpokea Lowassa, akagombea, kisha akapata kura milioni 6, zaidi ya mgombea yeyote aliyewahi kutokea Chadema, akaongeza idadi ya wabunge wa Chadema, huu uamuzi kuuita mbaya ni kutokitakia chama mema uliojaa mawazo mgando, unataka kidumae, na hapa usiuite ule uamuzi tabia, unakosea, tabia ni lazima tendo lijirudie, lakini bado hakuna yeyote aliyepewa nafasi kama ya Lowassa, unakosea...

- Suala la pesa za ruzuku wakati wa Magufuli, hapa kwanza tukubaliane mimi sio msemaji wa Chadema, nachoandika ni mawazo yangu hasa nikizingatia hali halisi tuliyokuwa nayo wakati ule.. unapodai kwanini pesa za ruzuku kama zilitoka hazikutumika kujenga ofisi za chama, hapa ni sawa na kuwapangia Chadema matumizi...

Mimi nawe hatupo kwenye vikao vyao vya maamuzi, hivyo hatuwezi kujua nini walikubaliana hizo pesa za ruzuku zikafanye, muhimu kama unaamini ripoti ya CAG, na kama ripoti haikuwa chafu kwa upande wa Chadema, basi tuamini hizo pesa za ruzuku [iwe zilitoka kwa mafungu, au zote] zilitumika vizuri, tusiwapangie matumizi wale sio mbuzi wasiojielewa.

- Hoja yako ya mwisho, unaendelea kuishi kwa wasiwasi na mashaka tu, nimekwambia weka hapa ushahidi wako kuthibitisha nina Id mbili au zaidi humu JF, una kaugonjwa ka kudhani watu hawawezi kufanana mitazamo, au ni wewe na wenzio pekee ndio wenye haki hiyo!

Na unapenda sana kujisifu hoja zako hazijibiki, wakati majibu unapewa, wewe unaishia kulazimisha tu Id nyingine! usitumie hisia zako kama mlango wa kutokea, unajidanganya!, sina huo utoto uliokariri kwa wengine, najiamini.
 
Nahisi nimeanza kufananishwa nawe tena kwa sababu za kihisia tu, kisa tunafanana mawazo[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Tindo anasema angeiona CHADEMA na Freeman Mbowe ni "babu kubwa" na wamefanya maamuzi sahihi kumkaribisha Edward Lowassa kama angeshinda u - Rais.

Hayo mafanikio mengine hayaoni kabisa ya CHADEMA kupata kula 6+M, idadi ya wabunge kuongezeka nk nk kwake si kitu. Kwake mafanikio ni Edward Lowassa angekuwa Rais regardless of others hindering factors.

Na ndiyo sbb hii inamfanya brother Tindo am -Judge Mbowe kama kiongozi aliyeshindwa kuiongoza CHADEMA.

It's very ridiculous, right?
 
Nahisi nimeanza kufananishwa nawe tena kwa sababu za kihisia tu, kisa tunafanana mawazo[emoji3][emoji3][emoji3]
Hilo linashangaza.

Mimi sikujui na wala wewe hunujui..

Basi tu tumekutana tu hapa.

After all Mimi nimejiunga JF juzi baada ya kuwa guest Kwa muda mrefu.
 
Jamaa umenizidi busara, hongera, mimi huwa natwanga tu sina busara kama zako, ajabu huyu mtu ndie anajiita mwenye hoja zisizojibika!

Tindo ameathiriwa na misimamo isiyobadilika, ameshindwa kuendana na wakati na mazingira, mfano miaka mingi anaamini Mbowe hafai kuwa mwenyekiti kwasababu amezidisha miaka kumi, kwake kiongozi akizidisha miaka kumi anaamini akili ya kiongozi inasimama!

Hivyo, ikitokea kwake kiongozi huyo akafanya mambo yenye manufaa kwa chama chake, yeye haoni, mfano haya maridhiano kuleta mikutano ya siasa, kwake haoni umuhimu wake, amekomaa tu na sababu kwa kiharakati Mbowe hafai, matokeo yake sasa akiulizwa kama amewahi kuandamana, anajibu ana kilema ili kutuzuga, anadhani akisema ana kilema ataaminika bila ushahidi wowote...
 

ngeli
 
You are right, Ameandika kama mkt au mtu wa karibu na mkt ktk uongozi.

Hoja nzuri pia🙏🙏
 
You are right, Ameandika kama mkt au mtu wa karibu na mkt ktk uongozi.

Hoja nzuri pia[emoji120][emoji120]
Haya mawazo unayoita mazuri kimsingi ni ya wapiga ramli, sababu hayana uthibitisho wowote, labda nawe uwe umepiga ramli kama mwenzako, fani inayowafaa nyie ni uganga wa kienyeji..
 

Hongera kwa kurejea. Tuanzie hapo kwa Shibuda. Sina popote ninapokataa mtu ama kiongozi yoyote kupokelewa ndani ya CDM. Ninachokataa ni mtu kupokelewa ndani ya muda mfupi na kupewa nafasi ya kugombea. Case study ikawa huyo Shibuda baada ya kuingia muda mfupi, akaendelea na tabia zake za kiccm. Hilo lilipelekea kutoshirikiana na chama. Labda useme hakunyimwa ushirikiano.

Narudia tena, sina popote ninapokataa mtu kupokelewa na kupewa uanachama, ninachokataa ni mtu kupokelewa tena ndani ya muda mfupi, na kupewa nafasi ya kugombea, huku wanachama waaminifu wakiachwa. Matokeo yake hao watu wa kuokoteza wanakuwa wepesi kutokuenda na mtazamo wa chama, au kukosa uvumilivu. Kwenye hili tukubali kutokubaliana.

Nijuavyo Slaa hakuwa mwanachama wa CCM baada ya kuondoka CDM, bali alifanya majukumu ya kiserikali. Je kufanya majukumu ya kiserikali ni kufanya kazi za CCM? Unanituhumu kwa hisia, ila unataka niamini Slaa alienda kufanya kazi za CCM.

Huu upotoshaji kuwa Lowassa alileta kura 6m huwa nikisikia nacheka sana. Kwahiyo kazi yote kubwa ya CDM toka 2010-2015 haikuleta hizo kura 6m, bali uwepo wa Lowassa ndio ulileta hizo kura ndani ya miezi miwili! Kama Lowassa alileta kura 6m+ akiwa na miezi miwili, alileta viti vingapi vya ubunge na udiwani akiwa na miaka miwili?

Ni kweli mwenendo wa kufanya siasa unabadilika, na kubadilika ni lazima, ila sio kama unavyosema ww. Nimejibu haya maana nimeona wangalau yanaelekea, hayo mengine naona ni burudani kama burudani nyingine.
 
Haya mawazo unayoita mazuri kimsingi ni ya wapiga ramli, sababu hayana uthibitisho wowote, labda nawe uwe umepiga ramli kama mwenzako, fani inayowafaa nyie ni uganga wa kienyeji..
Kwamba hata sauti ya mwanao akiongea au kuandika msg Kwa simu huwezi ijua Hadi ufanye research?

Usisahau kuwa AKILI iliumbwa ndani ya mtu kabla ya ELIMU.
 

Naona unajitahidi kunilisha maneno, mimi sikuwa muumini wa Lowassa au mwanaccm yoyote, lakini ingetokea Lowassa Kawa rais, bado angeongoza kwa mitazamo ya kiccm na sio zaidi ya hapo. Tushukuru tu hakuwa rais. Hivyo sina popote ninapoona angekuwa rais ingekuwa sawa.

Nasema hivi, kura 6m+ ilizopata CDM ni kazi yake ya siasa iliyofanya mara baada ya uchaguzi wa 2010-15. Na kwenye kazi hiyo Lowassa hakuwepo, bali CDM ndio ilifanya kazi ya kuweka wazi uchafu wake, ila kwa masikitiko makubwa ikameza matapishi yake miezi miwili kabla ya uchaguzi wa 2015, na hamasa yake ya kupambana na ufisadi. Mengine ni historia.

Lowassa alishindwa kuondoka na wabunge 50 aliosema ataondoka nao CCM ambako alikuwa na influence, lakini aweze kuleta kura 6m+ ndani ya CDM?! Kwa taarifa yako CDM ingeweza kupata kura zaidi ya 6m, na bado haiba ya CDM ingeendelea kuwepo bila huyo Lowassa. Hili hata upoteze miaka kulitetea ni ukweli usiobadilika. Kama kuna walioona faida ya Lowassa ndani ya CDM, basi ni viongozi. Ndio maana walikuwa wanamkalisha high table kwenye mikutano ya CDM akiwa analala tu, huku akiwa hana cheo chochote cha kikatiba cha kumkalisha high table. Pale ndio nilijua kweli hela ni mwanaharamu. Kwenye hili la pesa za Lowassa bisha, panga pointi, au chochote utakacho lakini habari ndio hiyo.
 

Ww kwa haya maoni yako Imebidi nicheke tu. Hebu acha niendelee na yule aliyesema sio ww. Yule huenda akawa na majawabu, maana naona kuna majibu zaidi kuliko majawabu. 2+2 ukisema ni 5 hilo ni jibu, lakini ukisema ni 4 hilo ni jawabu. Acha yule niendelee naye, ww umesema huna busara hivyo unaweza kunitangwa. Naogopa kitwangwa😂😂
 
Kwamba hata sauti ya mwanao akiongea au kuandika msg Kwa simu huwezi ijua Hadi ufanye research?

Usisahau kuwa AKILI iliumbwa ndani ya mtu kabla ya ELIMU.
Kuandika comment JF ni tofauti na sauti ya simu inayoizungumzia, hapa hatuwasiliani kwa sauti.
 
Hapa nafurahi umeshatambua mimi sio yule, nashukuru kwa kufahamu hilo, hivyo uache kuendeshwa kwa hisia za Id mbili ukiwa JF na kujibu comments za wengine kwa kutumia hisia, hapa tunahitaji facts.

Mwisho, mimi huwa natwanga kwa hoja, sikutwangi kwa mawe au ngumi, najua hii itakuwa njia yako kukimbia, nimekuelewa, kuhusu mjadala wenu nawaachia, niliingilia tu baada ya kuona umejimwambafy kwa hoja zako nyepesi zilizojaa hisia kuwa hazijibiki!
 
Kuandika comment JF ni tofauti na sauti ya simu inayoizungumzia, hapa hatuwasiliani kwa sauti.
Kujua handwriting ya mwanamke na Mwanaume Huwa unafanya utafiti?

Ndivyo ilivyo,

Mimi niliwahi kumsikia Dr Issaac wa Clouds kipindi Cha njia panda na niliweza kutengeneza image ya sura yake akilini mwangu,

Nilipokuja Kumuona live, ndivyo alivyoonekana.

Ukipenda Amini. Usipopoamini sawa pia.
 
Sidhani kama CCM watawapa katiba mnayoitaka na tume huru mnayoitegemea.

Hivyo ndo vinawaweka madarakani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…