Hongera Paul Makonda kwa kupata mtoto wa kiume

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda. Naandika hapa kukupongeza kwa moyo wa dhati kabisa kwa kupata mwana ambaye nasikia umempa jina la Keegan. Hongera sana. Najua relief iliyomo moyoni mwako kwa sasa. Maana watu walisema kila msemo. Mungu Mkubwa kaka, mwamini Yeye ndiye mtoa na mnyima wa vyote.

Lakini nna jambo moja kubwa nataka niseme nawe kidogo kuhusu barabara za jiji la Dar es salaam ambalo kila kona sasa hivi lami mbovu imekatwa 'Kashata' bila shaka ni kwa ajili ya kuziba mahandaki. Tatizo kaka RC hao wakata kashata wanafanya hivyo leo lakini wanakuja kufukia mahali hapo mwezi ujao. Na lami ikikatwa inakuwa kali kama kisu. Hivyo matairi ya vigari vyetu vya mkopo yanaathirika kishenzi!

Mfano mdogo tembelea barabara ya Kinondoni Muslim ambayo leo imekatwa 'kashata' toka kwa Manyanya hadi barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Hebu waeleze watu wako wazibe hizo kashata mara tu baada ya kuzikata lamini haraka, vinginevyo nia njema ya kukarabati barabara zetu itageuka janga kwa watumiaji barabara.

Kwa leo ni hayo tu. I hope utapitia hapo na sehemu zingine uone uozo huu
 
Mambo mengine ni ya binafsi sana hayapaswi kuingizwa ktk siasa.
Mange na wenzie walivuka mstari kumshambulia Makonda kuhusu familia.
Na Mange hii ndio asili yake kushambulia wengi hadi mambo binafsi kama vile alivyomshambulia Mzee Lowassa kipindi flani.
Au anavyomshambulia mheshimiwa flani kwa mambo binafsi sana kiasi cha kuwaumiza wasio husika na migogoro yake.
 
Acha walopoke, siku Makonda akimwonyesha live, chata ni yake, hawa hawa watadai ni wa kaka ake .
 
Mama yangu ndio hakika ila baba sina hakika
km umeishi miaka yote ukiamini huyo mwanaume hapo kwenu ndo baba ako huku akikusomesha na kukuletea ugali basi mwache mtoto Keagan naye apate nafasi ya kuamini Kuwa Paul Makonda ndiye baba ake naye afurahie haki ya kuita baba....he is to young kuanza kumvunjia heshima na kuviolate haki yake.....Watz tuache roho za kishetani
 
Mkuu, wewe ndio Mrs makonda nini?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…