Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda. Naandika hapa kukupongeza kwa moyo wa dhati kabisa kwa kupata mwana ambaye nasikia umempa jina la Keegan. Hongera sana. Najua relief iliyomo moyoni mwako kwa sasa. Maana watu walisema kila msemo. Mungu Mkubwa kaka, mwamini Yeye ndiye mtoa na mnyima wa vyote.
Lakini nna jambo moja kubwa nataka niseme nawe kidogo kuhusu barabara za jiji la Dar es salaam ambalo kila kona sasa hivi lami mbovu imekatwa 'Kashata' bila shaka ni kwa ajili ya kuziba mahandaki. Tatizo kaka RC hao wakata kashata wanafanya hivyo leo lakini wanakuja kufukia mahali hapo mwezi ujao. Na lami ikikatwa inakuwa kali kama kisu. Hivyo matairi ya vigari vyetu vya mkopo yanaathirika kishenzi!
Mfano mdogo tembelea barabara ya Kinondoni Muslim ambayo leo imekatwa 'kashata' toka kwa Manyanya hadi barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Hebu waeleze watu wako wazibe hizo kashata mara tu baada ya kuzikata lamini haraka, vinginevyo nia njema ya kukarabati barabara zetu itageuka janga kwa watumiaji barabara.
Kwa leo ni hayo tu. I hope utapitia hapo na sehemu zingine uone uozo huu