Mkuu hasira za nini na matusi
Kwanini usimuulize mwenzako ambae baada ya kushindwa kujibu maswali niliyomuuliza, akaanza matusi!!
wewe lile Tozo la kila mwezi unalipia bado
Silipii... sasa cha ajabu hapo ni kipi? Tatizo lenu huwa hamfuatilii mambo vinginevyo mngejua gharama kadhaa zilianza kuondolewa na Muhongo Awamu ya IV. Kwanza walishusha bei za kuunganisha umeme, pia wakaja kushusha hadi Sh.27,000 kwa watu wa vijijini!
hayo Makampuni ya Wizi waliokuwa wanatuchuna na kila siku bei kupanda ungeyadhibiti na kuyatumbua
Kwani hayo makampuni tumeacha kutumia umeme wake?! Au unazungungumzia IPTL ambayo imepelekea serikali kutakiwa kuilipa Standard Chartered USD 185 Million? ingawaje hata hivyo mkataba wake ulishaisha?
huyo Ruge na Sigh ungewaweza
Nchi ilishapotea kaa mkubali, Magufuli hajaongeza lolote ila kudhibiti kidogo kilichopa wanyonge km wewe utumie mtandao wa JF kutukana 24/7
Danganyaneni wenyewe kwa sababu anayefuatilia anajua bado mambo ya hovyo hovyo yapo pale pale!
NI Magufuli huyo huyo ndie alinunua kivuko kibovu.... hayo tuyaache!
Alipoingia tu madarakani likaibuka sakata la LUGUMI.... taja hapa serikali ya Magufuli imefanya nini?
Kila siku Magufuli wamebaki kupiga kelele kwamba nchi iliharibika! Kila mmoja anafahamu wezi wakubwa nchi hii ni Top Government Officials and High Profile Politicians.... nitajie Mwanasiasa mmoja TU na top government officials mmoja TU ambao wamefikishwa mahakamani kutokana na tuhuma za ufisadi!!
Kila mmoja anajua Ruge na Singh wapo mahabusu almost 3 to 4 years now! Na kila mmoja anajua hawa jamaa hawakwenda pale BoT na vifaru bali walishirikiana na wale wale niliowataja:
Top Government Officials and High Profile Politicians.
Again, nitajie Top Government Officials mmoja TU and High Profile Politician mmoja TU waliounganishwa na ile kesi!!
Juzi tu hapa tukasikia sakata la Lugola... sie wengine siku ile ile tukasema wazi kwamba kelele za Magufuli kuhusu ufisadi, target yake ni wafanyabiashara ili baadae wawachomoe pesa, na Watendaji wa serikali wa ngazi ya kati kuja chini!
Again, tuambie sakata la Lugola limeishia wapi?!
Pamoja na hayo, jibu swali langu la msingi: Tangia Magu aingie madarakani, amejenga plants zipi na zinazozalisha MW ngapi!
Jibu kwanza hayo maswali, vinginevyo case closed manake sioni sababu ya ku-argue na watu wasiojibu wasichoulizwa! Sana sana nikikubanisha sana na kushindwa kujibu, huenda ukafanya kama mwenzako... kukimbilia matusi badala ya kujibu hoja!