Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Mayala safi sana unajitambua na unaitendea haki tasinia ya habari, ili la kukanyaga katiba juu ya kuzuia wanasiasa kufanya siara hakujibu
 
Binafsi swali la Sammy Awamu alilomuuliza rais magufuli limekuwa chachu na nimeliona la maana zaidi.

Ni mwandishi gani ameuliza swali lililokukonga moyo wako na lenye maslahi mapana kwa nchi yetu?
Tido,paskali,

baada ya hapokuna haja ya kujihoji kama kweli baadhi ya magazeti yanafaa kununuliwa Tsh 1000,kwa aina ya wahariri walionao,hasa Jamhuri ya.manyerere ambaye aliulizia pombe(whisky) ikulu na msosi
 
Mambo muhimu hayajaulizwa ama hayajajibiwa kikamilifu matharani suala la ajira kwa vijana,mikopo,kilimo n.k.ameyajibu kwa figure of budget but not in reality.pia kashindwa kabisa kuonyesha kama anania ya dhati katika kukuza demokrasia.
 
Hongera Pascal, hata kama swali halikujibiwa vilivyo, naamini ujumbe uliokuwa ndani ya swali ulifika
 
Daaah ahsante sana Pascal Mayalla kwa kuuliza swali lenye maudhui kama ya swali nililouliza humu Jf jana. Pole pia kwa sababu swali hilo halikujibiwa ipasavyo.
 
Sasa naweza nikaamini ule uzi wa jana kwamba kuna waandishi walipewa maswali ya kuuliza. Haiwezekani waandishi wote wale swali la msingi na lenye akili litoke kwa Pasco Mayalla peke yake.
Mkuu ninaham ya kuumlza Pasco swari hili... Katika ule uzi wa jana uliofutwa na mod katika maoni yangu niliandika kuwa "Magu ninaemfaham ndo yule wa kuandaliwa maswari na si Magu wa mswari ya papo kwa hapo." Kinachonifanya niwe na ham ya kumuulza ni sababu Pasco alilake komenti yangu..
 
swali la Tido kuhusu udikteta limeua kesi zote mahakamani.....rais alisema kumuita dikteta ni muono wa mtu tu.

kwa maana hiyo yeye hajazuia muono wa mtu,na polisi pia wajitambue, wasilazimishe.muono wao ndio uwe muono wa kila mtu kwenye suala la kuwapeleka mahakamani wanaohisi magufuli dikteta
 
Ni kweli kauliza swali zuri lakini rais kamjibu kiutu uzima.rais anayo mamlaka yote dhamira ikiwa ni nzuri hata kama sheria haimpi mamlaka hayo tuache ushabiki wa kimachinga eti sheria na vitu vingine
 
Ukuu wa wilaya au mkoa au ukurugenzi utausikia kwa waandishi wenzako walio uliza kwa kujipendekeza
 
DR Ryoba , swali lake lilikuwa unajitathimini vipi wewe mwenyewe? Tido swali lake lilikuwa watu wanasema maamuzi yako kuhusu demokrasia ni kama unataka kufanya udikteta unasemaje kuhusu hilo? Mayalla swali lake lilikuwa umepata wapi mamlaka ya kuzuia mikutano ya kisiasa ?
 
Ni mjinga pekee ambaye angeshindwa kutumia platform kama ile kujitangaza, hata hivyo pamoja na hilo kauliza swali lake vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…