Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakika nimefurahishwa sana na Mwandishi huyu Pascal Mayalla wa kipekee aliyemuuliza swali Rais lenye msingi na hata rais kajibu kwa ubabaishaji. Natafuta clip au mwenye nayo aiweke.
Kwanza kaanza kwa kuitaji JamiiForums kwa kusema ni mwanachama mwandamizi wa JamiiForums.
Tido,paskali,Binafsi swali la Sammy Awamu alilomuuliza rais magufuli limekuwa chachu na nimeliona la maana zaidi.
Ni mwandishi gani ameuliza swali lililokukonga moyo wako na lenye maslahi mapana kwa nchi yetu?
Mkuu ninaham ya kuumlza Pasco swari hili... Katika ule uzi wa jana uliofutwa na mod katika maoni yangu niliandika kuwa "Magu ninaemfaham ndo yule wa kuandaliwa maswari na si Magu wa mswari ya papo kwa hapo." Kinachonifanya niwe na ham ya kumuulza ni sababu Pasco alilake komenti yangu..Sasa naweza nikaamini ule uzi wa jana kwamba kuna waandishi walipewa maswali ya kuuliza. Haiwezekani waandishi wote wale swali la msingi na lenye akili litoke kwa Pasco Mayalla peke yake.
Ni kweli kauliza swali zuri lakini rais kamjibu kiutu uzima.rais anayo mamlaka yote dhamira ikiwa ni nzuri hata kama sheria haimpi mamlaka hayo tuache ushabiki wa kimachinga eti sheria na vitu vingineKamuuliza kuwa kapata wapi mamlaka ya kuzuia safari za watumishi nje wakati kuna mihimili mitatu na yote inajiongoza yenyewe? Pia kwa nini mikusanyiko ya kisiasa inatambulika na katiba lakini yeye kaizuia wakati aliapa kutumikia nchi kwa mujibu wa katiba?
Kama wangekuwepo hata watano tuu wenye mwelekeo wa Pasco hakika angependa hayo masaa mawili ya ishe aondoke, lakini kwa vile waliopo wengi ni makanjanja basi kawaambia waulize mpaka wachoke wenyewe.
Pascal jitokeze kutupongeze kaka
Ni mjinga pekee ambaye angeshindwa kutumia platform kama ile kujitangaza, hata hivyo pamoja na hilo kauliza swali lake vizuri.Mayala alianza hotuba,kujifagilia na kutangaza kampuni yake na kujipigia debe la kutafuta fursa ikulu .Sehemu kubwa ya aliyonngea yalikuwa hasa ya kujinadi mnadani yeye binafsi.Kwangu naona kama aligeuza Ikulu na ile press conference kama gulio la kujinadi zaidi kuliko kuuliza swali.