Katika maswali ya hovyo kabisa kuulizwa jana na wanahabari ni lile lililotoka kwa Pascal Mayala.
Unawezaje kuuliza ni kwa mamlaka gani aliyopata rais ndani ya mihimili 3 iliyopo yaani bunge, serikali na mahakama kwa yeye kujitwalia mamlaka ya kubana matumizi?
Kwanza napenda ifahamike kuwa pamoja na kuwepo kwa mihimili 3 inayojitegemea bado ifahamike kwamba inaingiliana Katika Utendaji.
Na Katika muingiliano huu ifahamike kwamba katiba yetu inamtambua rais kama:
1. Sehemu ya bunge na anawakilishwa na Waziri mkuu Bungeni.
2. Rais ndiye msimamizi mkuu wa mipango yote ya ukusanyaji na matumizi ya fedha za umma Katika nchi yetu.
3. Rais ndiye msimamizi mkuu wa Utendaji kazi kwa watumishi wote wa umma Katika nchi yetu. Iwe ni kwenye fedha, afya, ulinzi, usalama, Elimu n.k.
Bunge na mahakama ni taasisi za umma na watendaji wake ni watumishi wa umma wanaowajibika kuteleza sera zinazopangwa na kusimamiwa na raisi Katika matumizi ya fedha za umma.
Hivyo Swali la Pascal Mayala hali kuwa bora bali lilionyesha hafaham vema katiba yetu na majukumu ya rais wetu.
Alipaswa ajifunze kabla ya kuuliza.
Kwa wale mnaomshangilia mnaonyesha pia mnahitaji kufahamu haya.