Ndagullachrles
JF-Expert Member
- Jun 20, 2023
- 256
- 259
Moshi
Hatua ya Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT)Moshi Manispaa kuanzisha mradi wa ushonaji nguo zikiwamo sare za Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni hatua ya kupongeza.
Pia hatua hii ya kuanzisha mradi huo ni mfano wa kuigwa na Jumuiya zote za Chama Cha Mapinduzi (CCM),ikiwamo umoja wa vijana wa ccm(UVCCM)na Jumuiya ya Wazazi .
Mwenyekiti wa UWT Moshi mjini,Theresia Komba anasema mradi huo utakuwa mhimili wa Jumuiya hiyo katika kuongeza ufanisi wa mapato ya Jumuiya.
Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo kutembelea mradi huo.
Anasema mradi huo utatoa fursa kwa Wanawake wenye ujuzi wa ushonaji wakiwamo wajasiriamali,wasichana na vijana wasio na ajira.
"Mradi huu utaboresha mapato ya Jumuia na ustawi wa wanawake Kwa ujumla",anasema .
Mradi huo wa ushonaji nguo utajikita kwenye ushonaji wa Bendera za CCM,sare za Chama ,Sare za shule na mitindo mbalimbali ya mavazi .
Komba anasema kuanzishwa Kwa mradi huu utasogeza huduma Kwa wanachama na Makada wa Chama Cha Mapinduzi.
Kwanza niwapongeze UWT Moshi mjini chini ya mwenyekiti wake Theresia Komba na katibu wake ,Catherine Sarwatt pamoja na kamati yake ya utekelezaji kwa kubuni mradi huu mzuri ambao utawaleta pamoja wajasiriamali,wasichana na wasio na ajira kupata fursa ya kujiunga kwenye mradi huo.
Hongereni sana UWT Moshi Manispaa kwa mradi huo mzuri na wengine nao waige kutoka kwenu.