Ukifuatilia kwa mbaaali mtoa mada hajui anachokifanya
Kwanza mdogo wangu hutambui yafuatayo
1. Maelekezo ya kula shuleni hayakutolewa na walimu
Haya yalikuwa maelekezo na vikao shuleni vya wazazi viliitishwa na hizo b
ajeti shuleni ukifuatilia zilipangwa na wazazi kwenye vikao, walimu wanafanya kusimamia tuu
2. Kuondolewa kwa masaa haya mawili wameeleza sababu za kusitisha kitu hicho na si kwa sababu ya michango ya chakula kama unavodai.
Kosa kubwa la walimu nini?
Kosa kubwa la walimu ni ujinga waliojitwika wa kufanya majukumu yasiyo ya kwao. Yani leo kwenye kikao wazazi wanaomba kusaidiwa kukusanya michango hiyo kesho yanayokuja ni haya ( ambaye hakuwepo kwenye kikao anaona huo ni mpango wa shule)
Kosa lingine ni KUYAPENDA MATOTO UTADHANI YAKIFELI KWAKO HAULI.
Nyakati zimebadilika walimu wanapaswa kufanya kazi na si kama wito. Hakuna sehemu utashtakiwa kama mwalimu kisa litoto limefeli. Fundisheni tu habari za kula, kusafiri sijui nini waachieni wazazi wao.
Mnapokea matusi kwa kujitolea kufanya kazi zisizowahusu
Fundisheni tuuu mambo mengine amalizane na wazazi wake
Na.1 naipinga kwa kielelezo cha barua hii, hapa niwazi kuwa waliopitisha ni wdc hapo hakuna mzazi ila wazazi wametumiwa km daraja kwakuwa wanawajua uelewa wao.
Na.2 Nakujibu hivi! Kuondolewa kwa masaa hayo mawili niwazi kuwa nikwaajiri ya kuondoa michango maana masaa hayo mawili ndio ilikuwa Sababu ya michango hiyo , pitia usome barua hiyo niliyokuwekea sababu iliyopelekea kuwepo michango hiyo.
Sema wamejibiwa kistaha na kiheshima ili kukwepa fedheha.
Kuhusu kosa kubwa la walimu ambalo umeliita ni (nanukuu) ujinga hilo nakuunga mkono 100% kwasabu ulizozitaja lakini nikataka niongezee kuwa ni bola yanapokuwepo mambo ya michango michango basi wizara yenyewe itangaze na walimu wajiweke pembeni maana kazi yao nikufundisha.
Kama siyo wizara basi atangaze RC, DC, WEO, VEO, baada ya kuitisha mkutano wakijiji na wananchi kuridhia badala yakutumia kakikundi ka kamati ya shule ambako kanatumiwa na walimu km daraja.
Hii inamaana watakuwa mbali na uchafu wowote ule.
Nikweli kabisa mtoto asipofauru kwa ajiri ya njaa hutashtakiwa wala kufungwa isipokuwa baadhi ya walimu nao ni njaa tu zinawafanya kila kitu waone nikama fulsa.
Ndio maana hata ccm waligundua kamati za siasa za kata ,wilaya, na mkoa, zilitumiwa kupitisha wabunge wasiofaa ikaamliwa majina yote yatumwe kamati kuu ndio ifanye maamuzi ya mwisho.
Hivyo walimu wasijifiche kwenye kamati za shule maana wazazi walishagundua kuwa zinatumiwa na walimu .
Swala hapa nikujiweka kando kabisa.
Hayo mengine naunga mkono kwa 100%
Enzi na Enzi.