Hongereni sana Law School of Tanzania kwa kulinda ubora wa fani ya sheria hapa Nchini

Hongereni sana Law School of Tanzania kwa kulinda ubora wa fani ya sheria hapa Nchini

Kwa moyo wa dhati nipende kuwashukuru watendaji wote wa Law School of Tanzania (shule ya sheria ) kwa kuzingatia weledi katika kufundisha na hatimaye kutoa wanasheria ambao watatumika serikalini pamoja na sekta binafsi.

Napenda nikiri wazi kabisa kwamba shule hii ni moja wapo ya taasisi chache za Serikali zinazozingatia weledi.

Watendaji wake hawafungwi na jina la mwanafunzi wala uwezo wake kiuchumi.

Wanazingatia kujiweka mbali na ukaribu na wanafunzi utaopelekea kutoa upendeleo katika usahihishaji.

Wanazingatia mno ubora wa mwanafunzi katika kutoa kile alicho nacho kichwani kwake.

Nawaomba wasiache hata mara moja ubora huu kwani kwa kufanya hivyo wataliangamiza Taifa kwa kutoa wanasheria wasiokuwa na uwezo hivyo kuharibu taaluma ya sheria.

Mungu aendelee kuwatia nguvu kwa kusimamia taaluma zenu kwa manufaa ya Taifa.
Matokeo ya mitihani Shule ya Sheria Tanzania;
Jumla ya Watahiniwa - 633
Waliofaulu (Passed) - 26
Watakaorudia (Supplementary) - 342
Waliofeli (Failed) - 265

Ukikokotoa hapo utaona ufaulu huu ni wa kiwango cha asilimia 4 tu. Yaani katika watu 4 katika kundi la watu 100, ndio walofaulu.

Tatizo lipo wapi? Ni kwa wanafunzi wa Shule ya Sheria? Au ni wanafunzi wa vyuo vikuu wanaojiunga na Shule ya Sheria? Au ni vyuo vinavyozalisha wahitimu wa shahada ya sheria? Kwamba wanazalisha wahitimu wasio na uwezo kiasi cha kushindwa kufaulu masomo ya Shule ya Sheria? Au tatizo lipo kwenye Shule ya Sheria? Kwamba wanafunzi hawafubdishwi vizuri lakini wanapewa mitihani migumu? Au mazingira ya elimu ni magumu?

Kupata majibu sahihi hapa ni lazima kuwe na utafiti. Lkn binafsi najua Elimu Ya Sheria ni ngumu. Na mahali panapoitwa Shule ya Sheria ni pagumu hasa kwa vijana wengi wa kitanzania wanaopewa elimu kwa lugha wasioimudu - achilia mbali mazingira duni ya elimu duni tangu hatua za awali.

Mwisho nimnukuu Dr. Kitila Mkumbo aliyewahi kusema; "Elimu ya Chuo Kikuu ni ya Kujitafutia". Nami namuelewa kwa kujua, Chuo Kikuu hakuna 'Walimu' wa kukutafutia 'Notes' na kuja kukufundisha hadi uelewe. Hapana. Chuo Kikuu kuna 'Wahadhiri' ambao kazi yao ni kutoa 'Hadhara' au 'Hotuba' halafu mwanafunzi anakwenda kuchimba mwenyewe. Sasa huo uwezo wa 'Kuchimba Mwenyewe' unajengwa na walimu huko Vidudu, Msingi na Sekondari.
 
Kwa moyo wa dhati nipende kuwashukuru watendaji wote wa Law School of Tanzania (shule ya sheria ) kwa kuzingatia weledi katika kufundisha na hatimaye kutoa wanasheria ambao watatumika serikalini pamoja na sekta binafsi.

Napenda nikiri wazi kabisa kwamba shule hii ni moja wapo ya taasisi chache za Serikali zinazozingatia weledi.

Watendaji wake hawafungwi na jina la mwanafunzi wala uwezo wake kiuchumi.

Wanazingatia kujiweka mbali na ukaribu na wanafunzi utaopelekea kutoa upendeleo katika usahihishaji.

Wanazingatia mno ubora wa mwanafunzi katika kutoa kile alicho nacho kichwani kwake.

Nawaomba wasiache hata mara moja ubora huu kwani kwa kufanya hivyo wataliangamiza Taifa kwa kutoa wanasheria wasiokuwa na uwezo hivyo kuharibu taaluma ya sheria.

Mungu aendelee kuwatia nguvu kwa kusimamia taaluma zenu kwa manufaa ya Taifa.
Guys more than 99 percent humu tumepita law school...so tunajua ugumu wa law school...binafsi bado nawalaumu WANAFUNZI kwa kiwango kikubwa, law school inakutaka uwekeze muda na akili yako yote pale, binafsi sikufaulu first sit I had kurudia civil na ni wazi nilitarajia Hilo kwa Jinsi nilivoona mtihani ule...Wala sikuonewa..vijana wengi siku hizi hawajitumi sana, Tena siku hizi mambo mengi yapo katika kiganja Chao lakini hawajitumi sana, kijana yupo chuo kikuu hasomi kwa bidii Wala hafikirii kwamba baada ya chuo Kuna maisha Tena maisha magumu haswa
Sidhan kama walimu wanafelisha

Mfumo wa lst ni kama mfumo wa mahakama sheria, mwenendo, hukumu revision, review appeal hapo ukitoka llb ya kuangalizia hutoboi jumlisha na cooperate issues ndio mlima mzito hayo ni mambo mengi kwa muda mchache

Sio kweli wanafunzi wa law school wengi incompetent ila wanajifanya wanajua sana kichwani hakuna kitu unamuambia aandike barua ya kuomba kazi tu hajui mpaka anakuomba desa atafaulu vip mitihani ya uwakili
 
Washatolea ufafanuzi
Kuwa wanafunzi wengi ni Vilaza
"vilaza" si jina sahihi "ni zaidi ya vilaza" na fani imevamiwa na haya mavyuo ya kata yanabeba kama treni kajamba nane, ilimradi wapate ada tu, sasa na bado hapo masomo yamepunguzwa sana, hawa watoto wangemkuta mtu kama DKT TULIA CKSON, JAJI ASINA OMAR, DR MAJAMBA si darasa zima lingefeli?
 
Kwahiyo unaweza kutoka veta ukaenda kuomba uwakili kwa Jaji mkuu?

Hivi Ccm uko huwa wanawaingiza nini kwenye ubongo?
Ni sawa ukasema anaetoa Diploma au Degree ni Rector

Unachanganya madesa mkuu emu endelea kujifunza
Haha nimekukamata vizuri popoma wewe.

Narudia tena kukusahihisha; Law school inatoa mawakili sio wanasheria.

Mwanasheria na wakili ni watu wawili tofauti kabisa ila layman kama wewe hawezi kuelewa kamwe.
kuhusi swala la uwakili na uanasheria Jamaa kaelezea vizuri mtu yeyote mwenye ubongo anaelewa...ila nyie vichwamaji hamjaelewa.
Mnafanya ionekane wote tunaokipondea chuo cha LST ni vilaza.

NB:Chuo kinazingua, haiwezekani watu wafeli vile.
 
kuhusi swala la uwakili na uanasheria Jamaa kaelezea vizuri mtu yeyote mwenye ubongo anaelewa...ila nyie vichwamaji hamjaelewa.
Mnafanya ionekane wote tunaokipondea chuo cha LST ni vilaza.

NB:Chuo kinazingua, haiwezekani watu wafeli vile.
Wewe nawe umekurupuka mkuu umeshikia mada katikati siku nyingine soma mpaka mwisho usikurupuke, watu km nyinyi hamkosekani katika wale 320 waliopata SUP km sio 250 walio DISCO wewe utakua ni mmoja wapo maana unadandia hoja kwa kukurupuka

Siku nyingi unapoona mjadala unaendelea soma mpaka mwisho acha kudandia mada katikati alafu unaanza kukosoa tu

Narudia tena kwa msisitizo soma mpaka mwisho
 
Wanaofaulu pale Law school ukisoma fact sheet yao ni chini ya 10% kila mwaka, tatizo linaweza kuwa sehemu zote mbili shule na wanafunzi.

Kiuhalisia sio vizuri kumaliza digrii ya sheria na kuunganisha law school, labda kama mtu ameshakaa kwenye.firm wakati anasoma digrii yake.

Ni vizuri na inashauriwa baada ya kumaliza digrii mtu akae angalau miezi 6 hadi mwaka 1 kwenye law firm ajifunze kwa vitendo ndio aende law school, kama ilivyokuwa lazima kwa zamani ufanye intern miaka miwili ndio ukafanye mtihani wa Bar

Tatizo digrii zote za sheria ni porojo tu (theory) ambayo hautaitumia kabisa pale law school na hata ukiitumia haifiki 25% ya ulichokivuna, law schoolni kama vile unaanza kusoma upya na unasoma mambo mapya.

Usishangae mtu ana GPA ya 4+ au hata ana PhD na law school ame disco hio ipo na inawezekana kabisa.

So ukitaka kumshauri mtu mwambie akae kwenye law firm kwanza ajifunze kisha aende sasa LST kupambania kombe
Ndugu Mgeni wa Jiji, huko kwingine tunaweza tukatofautiana ila ushauri wako wa kuwa vijana wakafanye practise kwanza angalau kwa miezi 6 mpaka mwaka binafsi nimeukubali kwa asilimia zote.
Kuwa Wakili inahitaji uende extra miles inahitaji uwe umepractice kwa kiasi kikubwa na hivyo basi internship kwa vijana ni jambo zuri kwa mustakabali wao hasa wanapoingia shule ya Sheria.
 
Naomba nieleweshwe hapa ina maan mtu akimaliza degree akashindwa kwenda LST anakuwa n jukumu gan au atahusika n nn mtaani ?na hiy degree yake [emoji120][emoji120]
 
Waalimu wa hiyo taasisi sio effective.

Taifa lingeweza pata mawakili bora na wengi zaidi kwa wahitimu wa sheria kufanya mtihani(bar examination) baada ya kujifunza sheria kwa vitendo
(apprenticeship) kwenye ofisi za mawakili wabobezi na mahakama kwa angalau miaka miwili baada ya kuhitimu.
Naunga mkono. Hoja [emoji111]
 
Siku hizi nayo huenda imekuwa simplified maana hata ambao hawana msingi wa Accouts wanazipata kirahisi tu tofauti na zamani!

Mtu amesoma course irrelevant sijui masomo gani ya arts n.k. Lakini utasikia amepata CPA [emoji87]

Naona kama heshima imeshuka!

Jamaa sijui kachoka yule?!

Hatusemi kuwa wabane sana kama zamani lakini pia sizani kama ni sahihi kuirwhisisha kiasi kwamba hata ambae hajasoma
Masomo ya commerce na bookkeeping and the related one tangu Shule ya msingi hadi chuo kikuu halafu aje kupata CPA itashangaza mno aisee?!

Kama mtu yeyote anaweza kupata!

Kwahiyo unataka CPA izidi kukazwa zaidi ya hapa, mbona hauwatakii watu mema mkuu
 
Back
Top Bottom