Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Matokeo ya mitihani Shule ya Sheria Tanzania;Kwa moyo wa dhati nipende kuwashukuru watendaji wote wa Law School of Tanzania (shule ya sheria ) kwa kuzingatia weledi katika kufundisha na hatimaye kutoa wanasheria ambao watatumika serikalini pamoja na sekta binafsi.
Napenda nikiri wazi kabisa kwamba shule hii ni moja wapo ya taasisi chache za Serikali zinazozingatia weledi.
Watendaji wake hawafungwi na jina la mwanafunzi wala uwezo wake kiuchumi.
Wanazingatia kujiweka mbali na ukaribu na wanafunzi utaopelekea kutoa upendeleo katika usahihishaji.
Wanazingatia mno ubora wa mwanafunzi katika kutoa kile alicho nacho kichwani kwake.
Nawaomba wasiache hata mara moja ubora huu kwani kwa kufanya hivyo wataliangamiza Taifa kwa kutoa wanasheria wasiokuwa na uwezo hivyo kuharibu taaluma ya sheria.
Mungu aendelee kuwatia nguvu kwa kusimamia taaluma zenu kwa manufaa ya Taifa.
Jumla ya Watahiniwa - 633
Waliofaulu (Passed) - 26
Watakaorudia (Supplementary) - 342
Waliofeli (Failed) - 265
Ukikokotoa hapo utaona ufaulu huu ni wa kiwango cha asilimia 4 tu. Yaani katika watu 4 katika kundi la watu 100, ndio walofaulu.
Tatizo lipo wapi? Ni kwa wanafunzi wa Shule ya Sheria? Au ni wanafunzi wa vyuo vikuu wanaojiunga na Shule ya Sheria? Au ni vyuo vinavyozalisha wahitimu wa shahada ya sheria? Kwamba wanazalisha wahitimu wasio na uwezo kiasi cha kushindwa kufaulu masomo ya Shule ya Sheria? Au tatizo lipo kwenye Shule ya Sheria? Kwamba wanafunzi hawafubdishwi vizuri lakini wanapewa mitihani migumu? Au mazingira ya elimu ni magumu?
Kupata majibu sahihi hapa ni lazima kuwe na utafiti. Lkn binafsi najua Elimu Ya Sheria ni ngumu. Na mahali panapoitwa Shule ya Sheria ni pagumu hasa kwa vijana wengi wa kitanzania wanaopewa elimu kwa lugha wasioimudu - achilia mbali mazingira duni ya elimu duni tangu hatua za awali.
Mwisho nimnukuu Dr. Kitila Mkumbo aliyewahi kusema; "Elimu ya Chuo Kikuu ni ya Kujitafutia". Nami namuelewa kwa kujua, Chuo Kikuu hakuna 'Walimu' wa kukutafutia 'Notes' na kuja kukufundisha hadi uelewe. Hapana. Chuo Kikuu kuna 'Wahadhiri' ambao kazi yao ni kutoa 'Hadhara' au 'Hotuba' halafu mwanafunzi anakwenda kuchimba mwenyewe. Sasa huo uwezo wa 'Kuchimba Mwenyewe' unajengwa na walimu huko Vidudu, Msingi na Sekondari.