Elections 2015 Hongereni tena Segerea: Nina furaha tele na sijatetereka

Nakupongeza sana Mtatiro kwa msimamo wako huu uliojali maslahi ya taifa kwenye kipindi hiki kigumu na muhimu sana kuelekea kwenye Tanzania mpya.
 
Ukawa tumewaahidi kuwaongezea wabunge tu. Ila sarakasi mnazoendelea ruka mwapunguza ari ya wananchi kuwapeni hata wabunge.

Mapambano ya ukombozi siyo mepesi kama unavyofikiria mkuu,cha msingi ni uvumilivu na kukaza mkaja na buti ili kuyafanikisha
 
Mtatiro umeonyesha ukomavu wa hali ya juu katika siasa. kweli tumekaribia nchi ya ahadi
 
Mtatiro utakuwa umelambishwa pesa ya kutosha. Siyo bure, mawazo yangu tu. sisi wanasiasa atu give up kirahisi namna hiyo
Ivi umesoma io post yake ukaielewa au unalaumu pasipo kuelewa. Jaribu kurudia tena kuisoma Mtatiro ni CUF na maelezo yake yanajitosheleza yupo tayari kumsaidia mgombea atakaesimamishwa na chadema (UKAWA) mpaka tupate jimbo. Kama ujui Mtatiro alikuwa agombee kwa tiketi ya chama chake cha CUF lakini kwa vile kila jimbo linamsimamisha mgombea moja wa Ukawa, jimbo la Segerea limeenda chadema na co CUF
 
Big up sana J. Mtatiro. Ni wachache sana wapo kama wewe!
 
umeonyesha ukomavu mkubwa sana kaka!mungu atakubariki.nimeanza kuamini kuwa kweli sasa wote tumejua "nia yetu"
 
Naona kuna dalili ya jina la Mahanga kujitokeza tena segerea
 
Hapana shaka kwa uthabiti wa moyo wako kwa kutokuwa mbinafsi, thamani yako imepanda maradufu!! Wewe ni mtu muhimu sana kwa mageuzi ya nchi hii, na ninakutabiria makubwa sana katika ulingo wa siasa za Tanzania. Siku kizazi chako kitakuwa kinashika rasmi hatamu ya siasa za nchi hii, wewe utakuwa mtu mzito! Na sisi wapiga kura tumeliweka hilo katika kumbukumbu zetu. Nimekufananisha na mtoto wa chacha wangwe ambae siku za karibuni alitoa jina lake katika watia nia wa kugombea ubunge tarime, na akakubali kugombea udiwani kwanza. Busara hizi zipo kwa binadamu wachache sana. Nakutakia kila la kheri. Lakini, bado nasikitika kukukosa mjengoni.
 
Ngoja Lipumba arundi kutoka kutumbua bilioni 3 za bure za chama cha zamani.
 
yaani cdm wakimrudisha mahanga ntaona ni chama cha watu ambao kwa kweli. muelekeo wamepoteza..ni zaidi ya UJUHA...ila sio utabiri kwa jinsi inavyokwenda..tusikia na kuona mengi..
 
Dah,Unastahili uenyekiti wa CUF,umekomaa kiasi cha kutosha,Hima viongozi wakuu wa CUF
 
Pole kwa kukatwa mkuu,chezea mbowe ww utabaki kua nyumbu wake na bado utakoma...
 
Asante kaka mtatiro kwa ukomavu wa kisiasa, wewe ni mfano wa kuigwa na wanasiasa walio wengi.

Masilahi ya taifa kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…