Wajumbe nilizingatia ushauri kama ulivyopendekezwa na
Fereke....... hakika haya mafuta ya mnyonyo nimeyakubali, tatizo jana limepotea kabisa na sasa niko vizuri..... Tafadhari msikimbilie mi operation kama hali zenu sio mbaya sana, ni bora kujaribu mbadala na mm nipendekeza Mafuta haya kama mbadala #1..... Ahsanteni
nimeambatanisha na picha za mafuta hayo.... nilinunua pharmacy kwa 5000... Japo huyo mtaalamu wa hapo Pharmacy alinishangaa kumuambia kuwa nimeshauriwa iyo ni dawa ya Bawasiri ya nje.... akataka aniandikie mavidonge ya kunywa na kuingiza sehem ya haja kubwa.... nikamuambia naomba mafuta tu, hayo mengine kama mafuta haya yatashindwa kutatua tatizo langu.