Hotuba kwa Wazee wa Dar: Rais Samia kuteua Viongozi bila kujali itikadi za Vyama

Hotuba kwa Wazee wa Dar: Rais Samia kuteua Viongozi bila kujali itikadi za Vyama

Erythrocyte, rafiki yangu, nilipoyasikia tu maneno ya mama nikakuwaza wewe kuhusu hizo fursa alizotangaza.

Mama kweli "anafungua nchi"!

Hapa kweli CHADEMA bado 'ITASAVAIVU'? Mtego wa panya unanasa kila takataka!

------------
Ni jambo jema sana kuunganisha nchi, lakini kweli kuteua watu ndiyo njia ya kuwaunganisha?

Huko CCM hakuna kabisa watu wanaofaa kusimamia sera za chama chao, hadi atafute nje ya chama?

Hawa watakaoingizwa serikalini wakitokea vyama vingine, bado watakuwa wanasimamia sera za vyama vyao, au itawalazimu sasa wawe watu wa CCM?

Ni wazi sasa, mama hakuwa ndani ya CCM kifikra, alikuwa huko kiwiliwili tu!

Na CCM wenyewe sasa watasemaje juu ya hili. Yule mtangulizi wake aliogopwa kwa kutumia mabavu, kwamba hakuna aliyeweza kunyanyua kidole kuhoji chochote, je mama yeye atatumia mbinu gani waCCM wasihoji?
Mama ndio mwenyekiti wa CCM na wamempitisha kwa 100% .kauli ya mwenyekiti ina nguvu
 
Tunakoelekea Mama ataipatia Tanzania Katiba Mpya. Trust Me
Hapo ni shida,sio japo rahisi mkuu.mwiji,mkapa,kikwete,jpm,wote walisita kufanya hivyo,hili Jambo sio rahisi ,ni uwe tayari kubeba eidha lawama au sifa,na pia uwe tayari kukabiliana na lolote litakalojili baada ya uamuzi.ngoja tuone!
 
Sioni jipya hapa.

JPM aliwateua akina Kitila Mkumbo, David Kafulila,Wilbroad Slaa, Julius Mtatiro na Anna Mghwila wakiwa upinzani ! Issue ni kuwa ukishateuliwa inabidi ukubali kutekeleza ilani ya CCM, na hapo ndipo ulipo ugumu kwa vyama vya upinzani; ni ugumu huo unaowalizimisha wateule kuhama vyama baada ya kuteuliwa.
Kabisa!

Kinadharia ni jambo zuri sana.

Ila kiuhalisia…hmm!!
 
Rais Samia amesema kuanza sasa ataanza kuteua wachapakazi bila kujali itikadi ya kisiasa katika Serikali yake.

Amewataka watanzania kujiandaa kisaikolojia kupokea mabadiliko yatakayoleta Umoja wa Kitaifa.

Huko mbele katika kupanga safu za kujenga uchumi sitochagua, Mtanzania yeyote mwenye weledi na umahiri anayeweza kuleta manufaa kwa Taifa nitamuingiza afanye kazi, sitochagua huyu katoka Chama kipi yule katoka Chama gani lengo letu ni kujenga umoja wa Watanzania


Labda baafa ya 2025. Ila kwasasa ajikite kutengeneza democrasia na kuacha siasa huru.
 
Back
Top Bottom