Hotuba kwa Wazee wa Dar: Rais Samia kuteua Viongozi bila kujali itikadi za Vyama

Hotuba kwa Wazee wa Dar: Rais Samia kuteua Viongozi bila kujali itikadi za Vyama

Umesahau waziri mkuu alidanganya taifa kuwa marehemu dikiteta magufuli tu bukheri na afya njema, kumbe tayari alikuwa keshang'ata shuka?
Nayeye alidanganywa,hata makamo wake ambae ni Rais wa sasa pia alisema Rais ni mzima na anachapa kazi.
 
Hahahaha... Umeshageuka mara hii???
Wapinzani hawacheleweshi tena maendeleo?

Nilisema ni suala la muda tu mutamkana Jiwe na siasa zake. Hata miezi 2 haijaisha Umeshamgeuka Mwendazake.
Mbona kwenye utawala wa Magufuri Wapinzani wengi walipewa vyeo,hapo kuna jipya lipi?labda sema kwa Magufuri mlikuwa mnasema wananunuliwa hiyo ndio tofauti,ila hata enzi za Magufuri Wapinzani wameteuliwa.
 
Mama anaongea mambo kwa uwazi na yanafikirika kwa akili za kawaida na utekelezaji wake unawezekana sio zile porojo zakuambiana dona kantri mara nchi iwe kama ulaya uku ata vyoo majumbani hatuna..Hili jambo nila muhimu sana kwasasa kwasabu wako watu wengi nje ya mfumo rasmi wa siasa za majukwaani au kwenye chama kinachoongoza kitu ambacho endapo wangetumiwa vizuri nchi ingefika mbali.Hadi hapa mama amescore 50%,zilizobaki naamini kwakadri muda unavyoenda atarekebisha mengi muhimu.
 
Wahamiaji wa kununuliwa hakuna tena maana akiwahitaji atawatafuta maenyewe.
Mambo yatajirudia - maana akisha wachagua, Wataunga juhudi (Prof Mkumbo, mama Anna Mgw..) hivyo Msifurahi mwanzoni. Wote ni kuuma! Magufuli aliuma kwa kubana na meno, Samia anaumwa halafu analegeza meno (anaachia) huku akivuvia! Mwisho wa siku upinzani unabaki skeleton - mifupa mitupu.
 
Jiwe tumemkanaje?

Slaa, Mgwira, Kitila, Mtatiro, Kafulila wote hao waliteuliwa na jiwe enzi zake..
Wewe kweli ni Mataga.
Slaa,Mtatiro na Kafulila wakati wanateuliwa walikuwa wapinzani? Si walishaunga mkono juhudi ndio wakakutana na uteuzi huko mbele wakiwa CCM tayari!!

Yaani hata mambo ya chama chako mwenyewe huyajui!!!
 
Mbona kwenye utawala wa Magufuri Wapinzani wengi walipewa vyeo,hapo kuna jipya lipi?labda sema kwa Magufuri mlikuwa mnasema wananunuliwa hiyo ndio tofauti,ila hata enzi za Magufuri Wapinzani wameteuliwa.
Wapinzani gani walipewa vyeo?
Utanitajia Mtatiro,Kafulila na Slaa?

Wakati wanapewa hivyo vyeo walikuwa ni wapinzani au walishaunga mkono juhudi ndio wakakutana na vyeo huko mbogamboga?

Mataga yaani hata kumbukumbu hamutunzi kwenye vichwa vyenu
 
Rais Samia amesema kuanza sasa ataanza kuteua wachapakazi bila kujali itikadi ya kisiasa katika Serikali yake.

Amewataka watanzania kujiandaa kisaikolojia kupokea mabadiliko yatakayoleta Umoja wa Kitaifa.

Huko mbele katika kupanga safu za kujenga uchumi sitochagua, Mtanzania yeyote mwenye weledi na umahiri anayeweza kuleta manufaa kwa Taifa nitamuingiza afanye kazi, sitochagua huyu katoka Chama kipi yule katoka Chama gani lengo letu ni kujenga umoja wa Watanzania


Utabiri Wa yule mchungaji unatimia.
 
Leo unapata tabu, [emoji23][emoji23][emoji23]

Jiandae kuona Lisu akiteuliwa kutekeleza sera za ccm utake usitake.
Umeshageuka tena!

Lisu si ni kibaraka wa mabeberu?

Cha ajabu Kesho Mama akimteua Lisu utakuja hapa kupiga makofi na kumpongeza kwa kuteua.

Yaani Mataga akili zenu sometimes mnazielewaga wenyewe.
 
Hapa mama anafanya muendelezo wa watangulizi wake. Sifa kubwa iende kwake kwa sababu ameweka bayana kwa nini atawaingiza kwenye safu ya uwongozi wake. Ni kwa sababu ya uwezo wao wa utendaji. Big up madam president.
 
Swali lilikuwa specific kwa BAK na nilikiwa na sababu kumuuliza yeye ila wewe uliamua kuvaa viatu vyake..... hukunijibu ila ukazunguka zunguka weeeee kisha ukaja na hoja za kuniuliza mm ni nani JF🤣
Sikia ww, swali specific unamfuata mtu inbox, ukimuuliza hapa ni la wote na yoyote. Hakuna mtu anajibu kwa utaratibu wako uutakao, maana humu ni kwenye social media. Huku ni kama uwanja wa wrestling, unapigwa ngumi, mateke, na viti, hata walioko nje ya ulingo usishangae wapo ulingoni. Kama hujui hilo basi hiyo ndio social media.
 
🤔🤔🤔
Katiba mpya lini?! Tume huru ya uchaguzi?!
Binafsi sidanganyikiiiiiii.....akija mwingine anaanzisha songi jipya na kama kawaida wagagagigikoko makofiiiiiiii~
 
Taja aliyeagiza polisi wanaolinda getini wasiwepo siku ya shambulizi. Ukijua aliyeagiza hilo umefunga ushahidi.
Kwanini usiweke ushahidi hapa kama kuna mtu aliagiza hayo?
 
Maendeleo hayana vyama. Au unajifanya hukusikia kwa sababu usemi ulisemwa na marehemu Magufuli. Duh sasa kamanda unaunga juhudi hivi hivi? Unachekesha.
Sijaunga juhudi ila nasema hivi,ni heri Zimwi ulijualo (CCM ASILIA) kuliko lile Zimwi la (WACHUNGA NG'OMBE) ambalo lilitaka Kutumeza na kututeketeza
CCM ASILIA itaturudisha kule kwenye Awamu ya Nne kwenye Demokrasia na Katiba mpya

Tunamfurahia Mama na mengi Moyoni ila lengo letu ni Tanzania yenye Demokrasia na yenye kuheshimu KATIBA na SHERIA na HAKI ZA BINADAMU.

umenielewa Mataga?
 
Umeshageuka tena!

Lisu si ni kibaraka wa mabeberu?

Cha ajabu Kesho Mama akimteua Lisu utakuja hapa kupiga makofi na kumpongeza kwa kuteua.

Yaani Mataga akili zenu sometimes mnazielewaga wenyewe.
Akiteuliwa hawi tena kibaraka maana mienendo yake inakuwa chini ya usimamizi mkali
 
Wewe kweli ni Mataga.
Slaa,Mtatiro na Kafulila wakati wanateuliwa walikuwa wapinzani? Si walishaunga mkono juhudi ndio wakakutana na uteuzi huko mbele wakiwa CCM tayari!!

Yaani hata mambo ya chama chako mwenyewe huyajui!!!
Usiwe na hasira za kijinga!

Kwani hili povu lako lote la nini?

Unapinga wapinzani kuteuliwa ama vipi? Maana sikuelewi
 
Back
Top Bottom