Hotuba na Ziara za Hayati Magufuli zilikuwa zinafuatilia sana kuliko zile za Mrithi wake

Hotuba na Ziara za Hayati Magufuli zilikuwa zinafuatilia sana kuliko zile za Mrithi wake

Nyakati hizo baada ya mishuhuliko yangu jioni natulia kwenye TV kumsikiliza JPM, nilipenda Yale maamuzi yake ya chapchap. Hakika tumempoteza mtu muhimu, RIP baba.
 
Angali hii pia
 

Attachments

  • Screenshot_20230312-195445_Chrome.jpg
    Screenshot_20230312-195445_Chrome.jpg
    181.1 KB · Views: 2
Asalaam Aleykum wana JF.
Nawapenda sana.
Nadondoka kwenye mada moja kwa moja.
Kulingana na utafiti mfupi nilioufanya, nimegundua kwamba Hotuba na ziara za Hayati JPM zilikuwa zinafuatiliwa na kusikilizwa na Watanzania wengi sana. Hii ni tofauti ukija kwa Hotuba na ziara za mrithi wake ambaye anaonekana kutokuwa na mvuto kwa Watanzania wengi hasa hasa kwa wanawake na vijana!
Unaweza kushuhudia hili kupitia kwa maongezi ya Watanzania wengi ambao walionekana kumwelewa zaidi Hayati kutokana na jinsi alivyokuwa anaonekana kuguswa na changamoto zinazowakabili hasa hasa Watanzania wa hali ya chini (aka wanyonge).
Huyu wa sasa hana mvuto kwa wengi kutokana na ile hali ya kuwajali zaidi matajiri na wale wa tabaka la juu kuliko maskini.
Fuatilia mitandao ya kijamii, Instagram, YouTube, Facebook n.k, utaona hata idadi ya watazamaji/wafiatiliaji (viewers) kwa hotuba za mama, ziko chini sana kulinganisha na zile za mtangulizi wake.
Naomba kuweka ushahidi hapa chini (angalia idadi ya "viewers").
Magufuli kimawazo na kimatendo alikuwa mbali sana na Watz wengi. Wengi hawakumuelewa.
Alitaka vitu vikubwa ambavyo watu wanaopenda vitu vya kawaida hawawezi, hawataki na hawa imagine.
Aliamini vitu vinawezekana. Hakutaka uzembe.
 
Magufuli kimawazo na kimatendo alikuwa mbali sana na Watz wengi. Wengi hawakumuelewa.
Alitaka vitu vikubwa ambavyo watu wanaopenda vitu vya kawaida hawawezi, hawataki na hawa imagine.
Aliamini vitu vinawezekana. Hakutaka uzembe.
Na kweli kazi zake zinaonekana Mkuu. Hata kama Watanzania wote tukimsaliti, kazi zake zitamtetea milele.
 
Alikuwa anaongea kutoka moyoni!
Hiki pi huenda kilikuwa kinawagusa sana watu.
Hawa wengine, maneno na uhalisia havipatani..
 

Attachments

  • RAIS_SAMIA_AWAPA_ZAWADI_MARAIS_WASTAAFU,_MTOTO_wa_MAGUFULI_APIGIWA_SHANGWE(144p).mp4
    10.7 MB
Hotuba zilikuwa na mvuto sana zile.
Nakumbuka Kuna kipindi niliwahi kuahirisha safari yangu ili tu walau nisikilize hotuba ya mwamba katika mojawapo ya ziara zake!
Nyakazilikuwa na baada ya mishuhuliko yangu jioni natulia kwenye TV kumsikiliza JPM, nilipenda Yale maamuzi yake ya chapchap. Hakika tumempoteza mtu muhimu, RIP baba.
 
Kwamba hadi leo anawalazimisha akiwa kaburini?! Maana kuna baadhi ya sehemu ukipita ni kawaida kukuta watu wanasikiliza hotuba za Hayati tena kwa utulivu wa hali ya juu. Ukiwauliza kwa nini, wanakwambia Hotuba za Hayati zilikuwa na mvuto sana kwa sababu alikuwa sauti ya wanyonge!
Hao ni majuha kabisa. Rais Wawa nyonge wakati vyuma kukaza iliibuka kipindi chake . Tatizo watanzania Wana ujinga na usahaulifu uliokomaa
 
Check hizi posts
 

Attachments

  • Screenshot_20230312-201230_Chrome.jpg
    Screenshot_20230312-201230_Chrome.jpg
    172.5 KB · Views: 2
  • Screenshot_20230312-201223_Chrome.jpg
    Screenshot_20230312-201223_Chrome.jpg
    261.1 KB · Views: 1
  • Screenshot_20230312-201211_Chrome.jpg
    Screenshot_20230312-201211_Chrome.jpg
    254.6 KB · Views: 2
Mwaka 2017 unga ulipouzwa 2000 kwa kilo,alikuwa wapi?kabla hajaingia madarakani sukari kilo ilikuwa 1800 ,ikawa 3000, mafuta ya kula yalipofika lita moja 8000 alikuwa nani?kwa bei ya sasa ya vyakula kutupa lawama za moja kwa moja kwa rais sio sawa sana!!japo kuna kitu cha kufanya lakini hakiwezi kuondoa hiyo hali.
Hospitalini kuna nini kilibadirika tena madawa ndio kulikuwa hakuna kabisa bora hata sasa.
Mkuu achana na hawa wajinga Wana usahaulifu na ujinga uliokomaaa
 

Watanzania ni watu wenye chuki, wivu na roho mbaya, wengi walikuwa wakifuatilia sana ziara za Magufuli kwasababu walikuwa na uhakika wa Magufuli kumdhalilisha na kumfuta kazi mtu katika hizo ziara.
Weka wazi kwamba ulikuwa mwathirika wa utawala wa JPM aidha fisadi, muuza madawa, mkwapuaji n.k
 
Ni kweli mkuu.

Kipindi kile amsha amsha zilikua nyingi.

Sasa hivi tumepoa kama uji wa mgonjwa yaani hata haieleweki tunapoelekea.

Tupo tupo tu yaani.
 
Ni kweli mkuu.

Kipindi kile amsha amsha zilikua nyingi.

Sasa hivi tumepoa kama uji wa mgonjwa yaani hata haieleweki tunapoelekea.

Tupo tupo tu yaani.
Kabisa, enzi hizo nchi ilikuwa imechangamka sana kulinganisha na sasa hivi
 
Kabisa, enzi hizo nchi ilikuwa imechangamka sana kulinganisha na sasa hivi
Ukitembelea sehemu za starehe ikifika saa mbili tu.

Miziki inazimwa taarifa ya habari wanaongeza sauti.

Watu kimyaa wanamsikiliza kiongozi wao.

Ila sasa hivi hakuna hata anayejali kwanza ukiweka taarifa ya habari wateja wanaweza hama kabisa.
 
Mama anapoint mmmno kumzidi na anakiingereza kizuri mmmno SEMA hapendi makiki kama mtangulizi wake ambaye mpaka ibadani alitaka makamera kujionesha!!!
 
Magufuli kimawazo na kimatendo alikuwa mbali sana na Watz wengi. Wengi hawakumuelewa.
Alitaka vitu vikubwa ambavyo watu wanaopenda vitu vya kawaida hawawezi, hawataki na hawa imagine.
Aliamini vitu vinawezekana. Hakutaka uzembe.
Kabisa yaani
 
Back
Top Bottom