Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Jana, Mbowe kwenye hotuba yake, alitumia muda mwingi kuzungumzia maridhiano. Na yeye mwenyewe alisema kuwa angetumia muda mrefu kuongelea maridhiano.
Kwa hotuba ile ya Mbowe, ni dhahiri chini ya uongozi wake, CHADEMA itakuwa chama rafiki wa CCM ya Samia, na mwanachama yeyote atakayekuwa kiherehere wa kupambana na CCM, ni dhahiri atakuwa pia adui wa Mbowe, na atakuwa adui wa CHADEMA ya Mbowe.
Mbowe aliyasifia sana maridhiano, na kwamba maridhiano yake na Samia yalifuta mabaya yote ya CCM ya Hayati Magufuli.
Hii ina maana kuwa kama Mbowe atajibakiza kuwa mwenyekiti wa CHADEMA, watakaokuwepo ndani ya CHADEMA, watatakiwa kuwa makini sana. Wakijifanya viherehere wa kupambana na CCM, si ajabu CHADEMA yenyewe itashiriki kuwakabidhi mikononi mwa vyombo vya CCM.
Kwa maoni ya Mbowe, ni dhahiri amekwisharidhika na hapo ilipofikia CHADEMA, na bila shaka CHADEMA itakuwa ikitumika kuuhadaa Ulimwengu kuwa Tanzania ina demokrasia ya vyama vingi, ili kuendelea kuvuta pesa za wafadhili, wakati kiuhalisia, nchi ipo kwenye mfumo wa chama kimoja.
UJUMBE MUHIMU:
Viherere wa kujifanya mnapambana na CCM wakati mpo ndani ya CHADEMA, muwe makini. Hiyo itakuwa ni sahihi na kumsema vibaya Rais wa nchi ukiwa kwenye kituo cha polisi.
Baada ya uchaguzi, tarajieni kuongezeka kwa safari za Mbowe kwenda Ikulu ili kupanga mikakati ya uchaguzi wa mwakani.
Kinahitajika chama cha upinzani kitakachopambana na CCM na vyama rafiki wa CCM. Baada ya CCM kufanikiwa kuipata CHADEMA, vile vyama 14 rafiki wa CCM vitapewa uzito mdogo sana.