Hotuba ya mwisho ya mwanaharakati aliyetekwa mbele ya watekaji. Dunia husau haraka

Hotuba ya mwisho ya mwanaharakati aliyetekwa mbele ya watekaji. Dunia husau haraka

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
HOTUBA YA MWISHO YA MWANAHARAKATI ALIYETEKWA MBELE YA WATEKAJI; DUNIA HUSAHAU HARAKA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kabla sijasimulia haya yote mimi Mtibeli nikakumbuka wakati Fulani nilipokuwa Msanii wa muziki. Najua utajiuliza ni lini TaikonMaster aliwahi kuwa mwanamuziki. Lakini nakuambia Mimi nilikuwa mwanamuziki mahiri muimba mashairi. Lakini kwenye matamasha ya siri. Wapi huko? Wapi Kule? Subiri.
Haya yataisha lini haha haha × 2
Kucheka kaburini hehe hehe
Kulia Harusini hoho Hoho
Haya yataisha Lini haha haha haha × 3

Kibao chetu katika jukwaa la siri ndio kinafungua andiko hili. Sauti ya mwanaharakati iliyozimwa sijui kuzimika au kujizima lakini hapana ni sauti iliyozimwa, pumzi iliyokatizwa, na mwili uliofukiwa.

Sasa! Sasa nini? Taikon Leo nitakuwa kifasihi zaidi kuliko kifalsafa.

Jina lake ni James lakini Wengu humuita Kipira huko mitaani na jamhuri za mitandaoni kama mtandao wa X(twitter hapo kale) na huko Facebook.
Mpaka sasa sijui kwa nini walimuita Kipira lakini Jambo moja la uhakika ni kuwa yake ya kuvutika Kila anapovutwa ilimfanya sio tuu apate jina hilo bali avutane na vyombo vyenye nguvu ndani ya nchi.

Wengine walimsifu. Wengine walimuonya na kumtahadharisha. Wachache walimtazama tuu kama filamu ya kusisimua au pengine kama Cartoon ya Coco.

James alituma ujumbe mfupi mtandaoni uliosomeka " Maisha yangu yapo hatarini. Kuna gari nyeupe isiyo na plate number inanifuatilia. Hamtanitisha. Nipo tayari kupigania nchi Yangu kwa kutetea haki za watu. Hamtaninyamazisha. Mimi ni Kipira"

Jumbe hiyo labda nami Taikon niliisoma. Au wewe msomani ulipata kuisoma. Ujumbe kutoka kwa Bwana Kipira. Post hiyo ilileta reactions nyingi mtandaoni.
Wengine Nani akutishe kinyamkera kama wewe. Unanini wewe.
Wengine waliomuonea huruma. Hii haiwezekani. Hatutakubali wakupoteze na wewe. Wajaribu waone.

Mtibeli ningefanya nini? Wewe ungefanya nini? Sijui wewe kipi ungefanya lakini Mimi nilikuwa kimya zangu nafuatilia Kila comment kutoka post Hiyo ya kipira.

Moyo wangu kama wako. Roho Yangu kama yako. Kuna wakati ilipata simanzi na huruma niliposoma baadhi ya comments. Akili Yangu kuna wakati ilivurugika lakini bado nilikuwa kimya vidole na macho Yangu yakiwa kwenye screen.
Comments nyingi zilimpa moyo. Goo! Goo shujaa wetu. Tupazie sauti kipira. Hakuna wa kukuangusha. Kama sio sisi basi Mungu atakuwa pamoja nawe.

Maneno hayo na mengine yalinitia nguvu sijui kama ilikuwa nguvu kweli au kujidanganya.

Mama wewe Kesho yake naingia mtandaoni moyo unapoteza muhimili. Nahisi kifua kizito. Kichwa kinavurugika.
"SAUTI ILIYOZIMWA" ndiyo post ya Kwanza kuiona. Alafu chini yake ulikuwepo picha ya Kipira alafu kwenye picha yalikuwepo maandishi Free kipira.

Ni kwamba Kipira alikuwa ametekwa usiku wa kuamkia Siku hiyo.

Sasa Ametekwaje? Wapi?

Usiku ulikuwa mzito kuliko kawaida.
Mvua haikunyesha mawingu yangalipo, lakini anga lilining’inia chini kana kwamba nalo lilikuwa likimsubiri aanguke.

Kipira alitembea peke yake usiku huo akitoka Kanisani, simu mfukoni, mawazo kichwani yakipambana na hofu aliyoizoea. Alikuwa amezoea kutishiwa. Amezoea kufuatwa. Lakini hakuwahi kuzoea ukimya wa sekunde ile kabla ya kutekwa. Eneo lilikuwa kimya Siku hiyo kuliko kawaida. sehemu ya ujumbe WA vitisho aliotumiwa ilikuwa ikizunguka katikaa mishipa ya damu ya ubongo wake "Dunia husahau haraka"

Ghafla
Gari jeupe lenye vioo vyeusi lisilo na namba lilisimama pembeni yake bila kelele.
Mlango ulifunguliwa haraka.
Mikono mikali migumu ikamvamia kama shetani.

“Usipige kelele.”
“usiharakishe kifo chako”
“Ni kazi tu.”
Kitambaa cheusi kikamfunika usoni.
Mwili wake ukapoteza mwelekeo.
Akajua hii haikuwa mara ya kwanza kwao. Ila kwake, ilikuwa mara ya kwanza kukutana na mwisho ana kwa ana. Mwisho mbele ya mwanzo mpya.

*******
Alipozinduka, kitu cha Kwanza kuhisi ilikuwa harufu ya unyevunyevu iliomchoma pua. Sakafu ya zege ilikuwa ya baridi, ukuta mmoja umevuja maji. Taa ya njano ilining’inia, ikiwaka kwa kupepesa kana kwamba hata umeme haukuwa na uhakika wa kuendelea kuishi hapo.

Mikono imefungwa nyuma.
Miguu imefungwa.
Uso umevimba. Midomo imepasuka. Alikuwa amepigwa Sana Mr. Kipira, mwanaharakati machachari Sana wa mtandaoni.

Sauti ilitokea gizani.

Mtekaji 1:
“Uko hai. Bado. Hilo peke yake linatakiwa likufurahishe.”

Kipira:
“Nipo hai kwa sababu mnahofia mkiniua hatia itakuwa juu yenu kwani mnajua sina kosa lolote”

Kicheko kizito kikapasua chumba.

Mtekaji 2:
“Wewe unaamini sana katika hadithi zako. Unajiona muhimu kuliko ulivyo.”

Ngumi ilishuka puuu!
Si kwa nguvu nyingi lakini kwa makusudi.
Ilikuwa ni mazungumzo kwa maumivu. Mahojiano ya mtekaji na mtekwaji. Ambayo mara nyingi wino wake huwa ni machozi na damu, herufi zake ni maumivu. Ujumbe wake ni kufumbwa Mdomo.
---

Walirudi kila baada ya saa kadhaa.
Maswali yalikuwa yaleyale.
Majibu yalibaki yaleyale. Kila upande ulibaki na msimamo wake.

Mtekaji 1:
“Unapigania nini hasa?”

Kipira (kwa sauti iliyochoka lakini imara):
“Haki. Haki ya maskini. Haki ya kupumua bila kuogopa. Haki ya kusema bila kutekwa. Hata haki yenu nyinyi mliofungwa kwa amri na kiapo.”

Kulikuwa na ukimya mfupi.

Mtekaji 3 (kwa kejeli):
“Tunajua. Ndiyo maana tupo hapa. Tunajua unachosema ni sahihi.”

Akasogea karibu.
“Lakini ukweli mwingine ni huu
tuna watoto. Tuna familia. Tuna mishahara.Na tumeagizwa.”

Kofi likamwangukia usoni. Kipira akagugumia

“Na wewe?”
“Utaachwa bila jina. Bila kaburi. Bila kumbukumbu. Maskini Kipira”
---
Wakati mwili wake ukizidi kudhoofika, dunia iliendelea kupiga kelele.
#FreeKipira
#WhereIsHe
#VoiceOfTheVoiceless

Picha yake ilizunguka mitandaoni.
Maneno yake yakarudiwa na watu aliowahi kuwatetea.
Lakini hapa chini ya ardhi hakukuwa na mtandao. Hakuna aliyejua yupo wapi isipokuwa wasiojulikana
Kulikuwa na pumzi nzito tu na saa isiyoonekana.

Bado Mimi nilikuwa nafuatilia mambo hayo huku uchungu na kiu ya kujua mambo hayo yataisha lini kwa namna ipi ikizidi kupamba Moto.
----------

Mtekaji 2:
“Unajua kinachofuata?”
“Leo wanapiga kelele. Wanakupigania then what? Kesho wanapata trend mpya.”

Akainama karibu na sikio lake.
“Dunia husahau haraka sana.”
---

Walikuja kimyakimya.
Hakukuwa na maswali safari hii.

Walimbeba hadi chumba kingine kikubwa kidogo, tupu, chenye ukuta mmoja wa saruji uliopakwa rangi iliyochoka. Kulikuwa na harufu ya chuma chenye kutu na unyevunyevu.

Mikono yake ilifunguliwa.
Kwa mara ya kwanza.
Mtekaji 1:
“Kama una cha kusema sema sasa.”
Walidhani atalia.
Walidhani ataomba msamaha. Walifikiri ataomba rehema zao. Kumbe je?

Alisimama kwa shida. Miguu ikitetemeka. Uso umejaa damu iliyokauka. Lakini macho naam macho yalikuwa wazi kuliko wakati wowote.

“Mnaniua,” alianza kwa sauti ndogo,
“lakini mnanipa heshima kubwa kuliko mnavyojua.”

Walitazamana.
“Mnaniua kwa sababu nimesema ukweli.
Na ukweli hauhitaji silaha, unahitaji sauti tu. Sauti ya ujasir"

Akapumua kwa nguvu.
“Mmenifunga. Mmenipiga. Mmeniumiza.
Lakini hamjaweza kunifanya niamini kuwa nilikosea.”

Akawaangalia mmoja mmoja.
“Najua hamtanikumbuka kwa jina langu.
Lakini nitawaandama katika usingizi wenu.”

Sauti ikawa nzito.
“Kwa sababu kila mtu atakayelia bila haki
mtanikumbuka.
Kila raia atakayenyamazishwa
mtanikumbuka.”

Akatabasamu kidogo. Tabasamu la mtu aliyefika mwisho bila kushindwa. Uso wake ukiwa mbele ya mtoa roho.
“Mnaweza kuniua.
Lakini hamtaweza kuua kile kilichonifanya niseme.”

Ukimya mzito ukaanguka.
---

Risasi ikasikika.
Ilikuwa sauti isiyohitaji maelezo.
_________

Kipira huyo huo ndio ulikuwa mwisho wake katika dunia ya Siri huku upande wa pili wa dunia ukiendelea kupiga Kelele.
Siku moja
Siku mbili
Siku tatu..
Siku Saba kelele zikapungua kadiri ya kupungua.

Siku kumi. Kipira jina lake likawa kama nahau za wahenga. Ambao hujitokeza kama mvua za jangwani bila sababu bila matokeo.

Sisemi alisahaulika wala sisemi alikumbukwa. Kipira alipotea Henoko na mwili wake haukupatikana kama Mwili wa Nabii Musa.

Hivyo ndivyo jinsi ilivyokuwa. Mimi Taikon nakumbuka post moja ya Kipira ambayo itabaki kama kumbukumbu ya milele.
"Maisha ni safari isiyo na kurudi nyuma. Ni mbele mbele daima"

Nafunga jalada la kitabu. Nyuma nakutana na maandishi. BE SAFE.

Acha nipumzike sasa.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mama alisema hakuna mwanaharakati tajiri-msodoki
Wanaharakati karibu wote ni tajiri wa roho.
Watekaji ni tajiri wa mali na huu hapo chini ni ujumbe wao toka kwa wahenga wa Karne nyingi walioandika biblia:

“What good is it for someone to gain the whole world, yet forfeit their soul?” Mathew 16.

Sooner or later, earthly things will fade away.
Utajiri, uongozi, nguvu za kijeshi, umaarufu, uheshimiwa, uafande vyote vitaondoka au vitakuishia.

Hapo ndipo utakapo poteza roho au nafsi yako kwa uchungu ukijutia matendo yako uliyo watendea uliowatesa na kuwauwa.
Upweke, huzuni na hasira vitakukabili ukiwa peke yako siyo na kikundi cha askari au majasusi, makasisi, au masheikh.

Hiyo siyo mbiguni bali hapa hapa duniani. It's all about guilty conscience.
 
Back
Top Bottom