Hotuba ya Mwisho ya Profesa Kabudi ndani ya masaa 24 akahamishwa Wizara

Stuka

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
282
Reaction score
906
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa Serikali ina mpango wa kuanzisha chombo cha kuratibu na kusimamia mikataba ambayo Serikali inaingia.

Prof. Kabudi ameeleza kuwa kuanzishwa kwa chombo hicho kutaisaidia nchi kutokuingia mikataba yenye masharti hasi na inayoigharimu serikali, na pia kubaini mapema migogoro ya kimkataba na kuitafutia suluhu bila kwenda Mahakamani.

Amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari na wakurugenzi wa divisheni/idara na wakuu wa vitengo vya sheria katika wizara, taasisi za umma na mamlaka za serikali za mitaa zaidi ya 300, jijini Dodoma, Desemba 6, 2024.

Aidha Prof. Kabudi amesema kuwa moja ya udhaifu uliopo ni usimamizi wa mikataba baada ya kuwa imesainiwa, huku akibainisha kuwa akiwa kwenye timu maalumu ya majadiliano ya Rais katika kipindi cha miaka saba, walibaini baadhi ya watendaji wa taasisi za Serikali kutokuwa na uelewa wa namna ya utekelezaji wa baadhi ya masharti yaliyomo katika hati za makubaliano yaliyofikiwa baina ya Serikali na wawekezaji, hivyo kuwatia hofu wawekezaji.

โ€œIli kuondokana na changamoto hizo, tulishauri kuwa ni vyema serikali kuwa makini kutekeleza makubaliano ya kimkataba na kuona umuhimu mkubwa wa kuwekeza katika majadiliano na huu ndio msingi wa kuja na mpango wa kuanzishwa chombo cha kuratibu na kusimamia mikataba,โ€ amesema Prof. Kabudi.

Pia amesema walibaini uchache wa wataalamu mahiri na wabobezi wa majadiliano katika maeneo mbalimbali yamajadiliano, huku akiwataka mawakili wa serikali kutumia sheria zinazosimamia maslahi ya taifa kama miongozo wakati wa kufanya majadiliano na kuandaa mikataba ili isiwe na masharti hasi.

NB: Kwa sasa nchi imeingia mikataba 43 ya Rasilimali ambayo haijawekwa wazi wala kufika bungeni, je kauli ya Kabudi inaweza kuwa imemponza? hadi kuhamishwa Wizara?


View: https://youtu.be/ZKAittcZjeQ?si=p8Ju44dobu6ml-22
 
Kapelekwa michezo ili asitumie akili yake vizuri akapige tarumbeta na kusifu na kuabudu!!

Hii nchi kamwe haitakaa ipate maendeleo ya kweli sababu ya uchawa!!
 
Kapelekwa michezo ili asitumie akili yake vizuri akapige tarumbeta na kusifu na kuabudu!!

Hii nchi kamwe haitakaa ipate maendeleo ya kweli sababu ya uchawa!!
Watakuwa wamehofia ikiundwa hiyo kamati maalum ya wataalam kuangalia mikataba, ina maana ile mikataba bandia ya mbuga za wanyama na hifadhi za misitu, iliyowafanya wageni kupora rasiliamli asilia za nchi itamwaaibisha wale wazenji walioisaini. Mikataba ya kuuza bandari ya Tanganyika, mbuga za wanyama na hifadhi za misitu ya Tanganyika, imesainiwa na wazanzibari, wakati rasilimali hizo siyo za Muungano.
 
Tanzania ndio ilivyo ukinyooka kwenye Jambo we adui

Ukiwa nzi ndio unafanikiwa kwenye mambo yako uku ukifanikisha mambo yao!!
 
Ameongea madini matupu jinsi ya kuokoa nchi na mikataba ya hovyo kwa muda mrefu. Kuja na chombo cha usimamizi kilichojaa Weledi, Wazalendo, wabobezi.

Wamemtosa sawa na Lukuvi, Slaa wizara ya ardhi.
 
Nakumkubali sana huyu jemedari.

Ndio vuguvugu wa kuamsha fikra za watanzania dhidi ya mali zao (Muite Sir Makinikia)
 
Hichi ndicho kilichomwondoa.
 
Nchi haina Rais tuendelee kumuomba MUNGU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ