Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa Serikali ina mpango wa kuanzisha chombo cha kuratibu na kusimamia mikataba ambayo Serikali inaingia.
Prof. Kabudi ameeleza kuwa kuanzishwa kwa chombo hicho kutaisaidia nchi kutokuingia mikataba yenye masharti hasi na inayoigharimu serikali, na pia kubaini mapema migogoro ya kimkataba na kuitafutia suluhu bila kwenda Mahakamani.
Amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari na wakurugenzi wa divisheni/idara na wakuu wa vitengo vya sheria katika wizara, taasisi za umma na mamlaka za serikali za mitaa zaidi ya 300, jijini Dodoma, Desemba 6, 2024.
Aidha Prof. Kabudi amesema kuwa moja ya udhaifu uliopo ni usimamizi wa mikataba baada ya kuwa imesainiwa, huku akibainisha kuwa akiwa kwenye timu maalumu ya majadiliano ya Rais katika kipindi cha miaka saba, walibaini baadhi ya watendaji wa taasisi za Serikali kutokuwa na uelewa wa namna ya utekelezaji wa baadhi ya masharti yaliyomo katika hati za makubaliano yaliyofikiwa baina ya Serikali na wawekezaji, hivyo kuwatia hofu wawekezaji.
“Ili kuondokana na changamoto hizo, tulishauri kuwa ni vyema serikali kuwa makini kutekeleza makubaliano ya kimkataba na kuona umuhimu mkubwa wa kuwekeza katika majadiliano na huu ndio msingi wa kuja na mpango wa kuanzishwa chombo cha kuratibu na kusimamia mikataba,” amesema Prof. Kabudi.
Pia amesema walibaini uchache wa wataalamu mahiri na wabobezi wa majadiliano katika maeneo mbalimbali yamajadiliano, huku akiwataka mawakili wa serikali kutumia sheria zinazosimamia maslahi ya taifa kama miongozo wakati wa kufanya majadiliano na kuandaa mikataba ili isiwe na masharti hasi.
NB: Kwa sasa nchi imeingia mikataba 43 ya Rasilimali ambayo haijawekwa wazi wala kufika bungeni, je kauli ya Kabudi inaweza kuwa imemponza? hadi kuhamishwa Wizara?
View: https://youtu.be/ZKAittcZjeQ?si=p8Ju44dobu6ml-22