Hotuba ya Pieter Willem Botha aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini ya Makaburu

Hii hotuba bila shaka inawakilisha fikra za weupe walio wengi, najaribu kufikiria na kinachoendelea Marekani kwa sasa.......kupitia kwa askari wake wanayoyafanya kwa weusi mpk huyo mgombea wao kutoka Republican.
 
Watu weusi wengi hawajitambui na hawana discipline katika mambo mengi, lakini huyu jamaa amekosea, amefanya generalization sana, wapo weusi wengi pia wanafanya vizuri mno na wenye busara, kusema weusi sio binadamu ni uboya mkubwa sana
 


Kwa nini umeileta hapa? Unataka kufikisha ujumbe gani hasa kwetu?
 
Nimejuta kusoma hii speech na hasa nilipofika hapa:
"Ukweli kuwa watu weusi
wanafanana na binadamu na
kutenda mambo kama binadamu
hauhalalishi wao kuwa watu wenye
akili timamu au binadamu
waliotimia. Kanunguyeye si
nungunungu na mijusi hawawezi
kuwa mamba eti kwa sababu tu
wanafanana."
Daaah, maisha yangu ya utoto Morogoro, nilijionea wale "jamaa" wa ANC kule Mazimbu, najaribu kupata taswira halisi! Hivi Botha bado yu hai ama?
 
hahahahah Botha huwa namkubali hapo kuwa weusi wanapenda sana kuoa wanawake wengi,wanapenda sherehe na wanaendekeza ngono,ukweli mtupu,ila kwingine sikubaliani nae kabisa
 
Bufa nakubaliana na wewe 10000% tatizo la mtu mweusi lipo kwenye kujitambua, kujithamini. Unaona hapo Botha anachosema ni kuwa weupe ni bora kuliko weusi. Na ukweli uko wazi. Inasikitisha lakini ni kweli. Kinachosumbua sana ni kuwa mpaka hapa pamoja na ushahidi wote mtu mweusi hajui tatizo liko wapi. Masikini wa Mungu kiumbe huyu mpaka leo hajui tatizo liko wapi.
 
Kwa nini umeileta hapa? Unataka kufikisha ujumbe gani hasa kwetu?
Sera za kibaguzi za makuburu vidi ya weusi siyo tofauti sana na sera ya CCM vidi ya upinzani. Huo ndio ujumbe loud and clear.
 
Mweusi, angalia hata hapa kwetu kinachofanyika!
 
Japo kuna sehem ametudhalilisha Sana ila hii hotuba kwa kiasi ina ukweli ndani yake. Weusi tuna matatiZo makubwa Sana. Nadhani ndio maana tunabaguliwa na kila race
 
Alafu utakuta mtu akifanyiwa figisu kwenye uchaguzi Africa anaenda ulaya..na wapiga kura wake wakimuona anaenda huko wanachekelea na kuona kama haki imeenda kutafutwa..

MTU akialikwa na hizi ngozi nyeupe anapiga mapicha na kuona kama Mungu amemuona vile..

Huu ni ugonjwa wa kujiona ngozi nyeusi hatuwezi kitu..

Wengine wakapungukiwa na akili kabisa wakasema wanampenda Trump atainyoosha Africa..hovyo kabisa.
 
Watu weusi wengi hawajitambui na hawana discipline katika mambo mengi, lakini huyu jamaa amekosea, amefanya generalization sana, wapo weusi wengi pia wanafanya vizuri mno na wenye busara, kusema weusi sio binadamu ni uboya mkubwa sana
Huyu nae kwa ghadhabu hii hatari

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…