Me nadhani ni dhana isiyo sahihi kabisa.
Jamii zinabadilika sana. Civilization ni mchakato mrefu sana, hata Afrika inayopitia leo ni njia kuelekea kustaarabika kwa jamii. Unapokubaliana na botha kuwa africans ni wabaguzi, wauaji, jiulize kuna mtu aliyefanya ushenzi kama mzungu kipindi cha Utumwa? Unakumbuka Civil War US ilitokana na nini? Tunahitaji kumkubusha Botha juu ya Vita ya kidini ufaransa? Kuna muafrika aliyemuua myahudi duniani? Wayahudi waliochinjwa Ufaransa, na ujerumani waliuliwa na waafrika?
Kinyume chake, dunia nzima inajua kuwa migogoro ya kiafrika mingi inatokana na ushetani wa hali ya juu walio nao hao kina Botha. Wazungu hawa waliotengeza chuki dhidi ya wahutu na watusi kule Rwanda, wana haki gani ya kunyooshea kidole waafrika? Walipoharibu umoja wa Rwanda na kuunga mkono makundi ya waasi, waliombwa wazime kituo cha radio cha kichochezi, wakagoma kwa sababu tu eti inacost dola ef 8 kwa saa, hawa ndio wanajua thamani ya humanity? Huko afrika kusini ni nani aliyewabagua weusi, kuwagawa na kutumikisha hadi leo wamekuwa wageni kwenye nchi yao?
Ni muhimu waafrika tuwe na fikra sawa sawa. Huwezi muona yuko sahihi anayesema waafrika ni wabaguzi hawawezi jitawala, wakati mtu huyo ndiye aliyewavamia kimabavu, akaharibu mifumo yao ya utawala, akaharibu elimu yao, akaharibu uchumi wao, akaharibu mifumo yao ya utawala, akawatengenezea matabaka kati yao, akawajengea chuki kati yao akawapa na silaha wauwane kisha awaibie mali na kuwatawala. Ni mtu asiyefikiri na kujua jamii za wazungu zimetoka wapi, ndio ataona kauli ya Botha iko sawa sawa. Kimsingi ni dhihaka, ni sawa na mtu anayekukata miguu halafu anakucheka huwezi panda mti kuangua matunda.