Hotuba ya Rais Magufuli kufungua Bunge la 12: Utumbuaji majipu utaendelea ili kuhakikisha Watumishi wanatenda kazi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni

Hotuba ya Rais Magufuli kufungua Bunge la 12: Utumbuaji majipu utaendelea ili kuhakikisha Watumishi wanatenda kazi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni

Dah...Hivi Bwana Robati na mteja wake watakuwa wanaangalia? [emoji2960]
 
Kamanda yuko kazini ngoja tuendelee kumsikiliza...
 
Wataalamu wa TEHAMA wataanza kutambuliwa na serikali
Kazi nzuri hii!!!
 
Kwa sasa anaeongea ni spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na anasema kikatiba wabunge wanaotakiwa ni 393 jumla na waliopo ni 359 wakisubiri wabunge watano kutoka baraza la wawakilishi, wateule 10 wa Rais, viti maaum kutoka vyama vingine.

Kwa sasa spika anamkaribisha Rais Magufuli kuhutubia

=========

MAGUFULI: Kabla ya kuanza hotuba yangu, nawasihi tusimame tumkumbuke mheshimiwa Mkapa pamoja na waheshimiwa wabunge waliofariki dunia tangu kufungwa kwa Bunge la 11.

Nitumie fursa hii kuwaahidi, serikali ninayoiongoza itaendelea kuwaamini wanawake katika kushika nafasi mbalimbali za uongozi.

Napenda kuwapongeza wabunge kwa kuchaguliwa kwenu, mmechaguliwa kwa kuwa mna uwezo, nawasihi msiwaangushe wananchi waliowachagua, wananchi wana Imani kubwa sana.

Nimekuja kulizindua Bunge hili baada ya nchi yetu kufanikiwa kumaliza uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba mwaka 2020 kwa uwazi, amani na utulivu mkubwa.

Kwa msingi huo napenda kuipongeza tume ya Taifa ya uchaguzi kwa vizuri zoezi la uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

=>Namuahidi Dkt. Mwinyi kwenye miaka mitano ijayo, Serikali ya JMT itatoa ushirikiano mkubwa wa kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Zanzibar

=> Tutafanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kuleta maendeleo kwa pande zetu zote mbili za muungano

=>Tumethibitisha uwezo mkubwa katika kusimamia Uchaguzi bila kutegemea misaada kutoka nje

=> Uchaguzi wa mwaka huu uligharamiwa na Serikali kwa 100% ambapo kiasi cha Bilioni 331 kilitengwa. Hata hivyo mpaka Uchaguzi umekamilika Tume imetumia Bilioni 262 tu

=>Kwenye miaka 5 ijayo tutaendelea kuimarisha utawala bora hususan kwa kusimamia kwenye utumishi wa umma

=>Tutazidisha mapambano kwenye dhidi ya rushwa, wizi, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.

=>Natoa shukrani kwa watanzania wenzangu wote kwa kushiriki vizuri na kuonesha utulivu mkubwa kwenye Uchaguzi uliopita

=>Hakuna shaka Uchaguzi huu kwa mara nyingine umethibitisha watanzania ni wapenda amani, tunajitambua, hatudanganyiki na tumekomaa kidemokrasia

=>Utumbuaji majipu utaendelea. Tutaboresha maslahi ya watumishi wote, watumishi wasiwe na wasiwasi wachape kazi

=>Tumeingia kwenye Uchumi wa Kati na tutazidi kukuza uchumi kwa wastani wa angalau 8% kwa mwaka na kutengeneza ajira zipatazo milioni 8

=>Tunakusudia kukuza kilimo biashara, mazao tunayolenga kuyapa kipaumbele ni pamoja na korosho, kahawa, pamba, chai, michikichi, miwa

=>Tunaagiza ngano nyingi na vyakula vingine kutoka nje, ni aibu kwa Tanzania, Waziri wa Kilimo nitakayemteua akaanze na hili



Bila hata aibu anasema eti wabunge wamechaguliwa. Alaaniwe na Lucifer
 
Mambo mengine mkiitwa hamna akili mnasema mnatukanwa. Watanzania gani wenye kufurahia hotuba wakati ni nchi yenye huzuni duniani? Eti mabeberu wanatuonea wivu! Pumbaf kabisa!
Screenshot_20201113-110326.jpg
 
Back
Top Bottom