Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa sasa anaeongea ni spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na anasema kikatiba wabunge wanaotakiwa ni 393 jumla na waliopo ni 359 wakisubiri wabunge watano kutoka baraza la wawakilishi, wateule 10 wa Rais, viti maaum kutoka vyama vingine.
Kwa sasa spika anamkaribisha Rais Magufuli kuhutubia
=========
MAGUFULI: Kabla ya kuanza hotuba yangu, nawasihi tusimame tumkumbuke mheshimiwa Mkapa pamoja na waheshimiwa wabunge waliofariki dunia tangu kufungwa kwa Bunge la 11.
Nitumie fursa hii kuwaahidi, serikali ninayoiongoza itaendelea kuwaamini wanawake katika kushika nafasi mbalimbali za uongozi.
Napenda kuwapongeza wabunge kwa kuchaguliwa kwenu, mmechaguliwa kwa kuwa mna uwezo, nawasihi msiwaangushe wananchi waliowachagua, wananchi wana Imani kubwa sana.
Nimekuja kulizindua Bunge hili baada ya nchi yetu kufanikiwa kumaliza uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba mwaka 2020 kwa uwazi, amani na utulivu mkubwa.
Kwa msingi huo napenda kuipongeza tume ya Taifa ya uchaguzi kwa vizuri zoezi la uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
=>Namuahidi Dkt. Mwinyi kwenye miaka mitano ijayo, Serikali ya JMT itatoa ushirikiano mkubwa wa kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Zanzibar
=> Tutafanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kuleta maendeleo kwa pande zetu zote mbili za muungano
=>Tumethibitisha uwezo mkubwa katika kusimamia Uchaguzi bila kutegemea misaada kutoka nje
=> Uchaguzi wa mwaka huu uligharamiwa na Serikali kwa 100% ambapo kiasi cha Bilioni 331 kilitengwa. Hata hivyo mpaka Uchaguzi umekamilika Tume imetumia Bilioni 262 tu
=>Kwenye miaka 5 ijayo tutaendelea kuimarisha utawala bora hususan kwa kusimamia kwenye utumishi wa umma
=>Tutazidisha mapambano kwenye dhidi ya rushwa, wizi, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.
=>Natoa shukrani kwa watanzania wenzangu wote kwa kushiriki vizuri na kuonesha utulivu mkubwa kwenye Uchaguzi uliopita
=>Hakuna shaka Uchaguzi huu kwa mara nyingine umethibitisha watanzania ni wapenda amani, tunajitambua, hatudanganyiki na tumekomaa kidemokrasia
=>Utumbuaji majipu utaendelea. Tutaboresha maslahi ya watumishi wote, watumishi wasiwe na wasiwasi wachape kazi
=>Tumeingia kwenye Uchumi wa Kati na tutazidi kukuza uchumi kwa wastani wa angalau 8% kwa mwaka na kutengeneza ajira zipatazo milioni 8
=>Tunakusudia kukuza kilimo biashara, mazao tunayolenga kuyapa kipaumbele ni pamoja na korosho, kahawa, pamba, chai, michikichi, miwa
=>Tunaagiza ngano nyingi na vyakula vingine kutoka nje, ni aibu kwa Tanzania, Waziri wa Kilimo nitakayemteua akaanze na hili
Shimboni shafo meku!Punguani la Lumumba utalijua tuu,yaani ccm hata yakichangua kitu utajua tu ni kujipendekeza na pumba
Yahane 😂😂😂😂Shimboni shafo meku!
AnasomaKwaiyo leo Raisi kaweka kila kitu kichwani sioni akisoma??
Hatuwezi pata maendeleo makubwa ya uchumi bila viwanda; hakuna viwanda bila rail, barabara, ndege, na nishati
Mungu ibariki Tanzania
Acha upuuzi weweBwashee usichanganye Imani ya dini yako na siasa!
Hii ile kelele ya Tanzania ya viwanda ilifia wapi?Hatuwezi pata maendeleo makubwa ya uchumi bila viwanda; hakuna viwanda bila rail, barabara, ndege, na nishati
Mungu ibariki Tanzania
Lissu alikataa cheo ,Hotuba yake inatia matumaini mazuri. Mambo mengi aliyoyasema ni mazuri Ila ili kujenga nchi yenye watu wamoja ningetamani sana kama angekutana na wapinzani wake ili kuwe na maridhiano ya kitaifa. Tuache chuki ambazo hazijengi kisha tuchape kazi tukiwa wamoja.
Ampe cheo Lisu kama alivyomuhaidi kwenye kampeni. Tukiwa wamoja hii nchi itapiga hatua kubwa sana kimaendeleo na sio kufanya ubabe kwenye kila kitu.
Lissu Ni mwanasiasa wa kwanza kutoka Afrika kwenda kuchongea nchi yake kwa wazungu.Mtanzania wa kwanza na ni muafrika wa Tatu baada ya Mandela na Kofi Annan kuhutubia bunge la ulaya lenye wajumbe 790 huwezi kulinganisha na mtu anaehutubia Halmashauri kuu ya CCM yenye wageni wawili waalikwa
Hamna mtu anataka cheo cha kupewa kama zawadi.Hotuba yake inatia matumaini mazuri. Mambo mengi aliyoyasema ni mazuri Ila ili kujenga nchi yenye watu wamoja ningetamani sana kama angekutana na wapinzani wake ili kuwe na maridhiano ya kitaifa. Tuache chuki ambazo hazijengi kisha tuchape kazi tukiwa wamoja.
Ampe cheo Lisu kama alivyomuhaidi kwenye kampeni. Tukiwa wamoja hii nchi itapiga hatua kubwa sana kimaendeleo na sio kufanya ubabe kwenye kila kitu.
Kwenye michezo hakuna ushindi wa mezani,au anataka apeleke jeshi!Tunataka ushindi, Tanzania tumechoka kushindwashindwa - John Pombe Joseph Magufuli
Hotuba yake inatia matumaini mazuri. Mambo mengi aliyoyasema ni mazuri Ila ili kujenga nchi yenye watu wamoja ningetamani sana kama angekutana na wapinzani wake ili kuwe na maridhiano ya kitaifa. Tuache chuki ambazo hazijengi kisha tuchape kazi tukiwa wamoja.
Ampe cheo Lisu kama alivyomuhaidi kwenye kampeni. Tukiwa wamoja hii nchi itapiga hatua kubwa sana kimaendeleo na sio kufanya ubabe kwenye kila kitu.
alafu baada ya hapo ?Mh. Askofu Gwajima kapewa nafasi ya kushukuru hotuba ya Rais kwa niaba ya wabunge,,,,
Mdee kazima tv yake hahahahah!
Dah....akili za kitumwa hizi... Afrika bado sana kujitawala...[emoji2960]Mtanzania wa kwanza na ni muafrika wa Tatu baada ya Mandela na Kofi Annan kuhutubia bunge la ulaya lenye wajumbe 790 huwezi kulinganisha na mtu anaehutubia Halmashauri kuu ya CCM yenye wageni wawili waalikwa
Ndio maana kumetengwa budget kuandaa wanamichezokwenye michezo hakuna ushindi wa mezani,au anataka apeleke jeshi!