Hotuba ya Rais Magufuli kufungua Bunge la 12: Utumbuaji majipu utaendelea ili kuhakikisha Watumishi wanatenda kazi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni

Hotuba ya Rais Magufuli kufungua Bunge la 12: Utumbuaji majipu utaendelea ili kuhakikisha Watumishi wanatenda kazi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni

Anasema ataboresha Demokrasia, Uhuru wa vyombo vya habari, na atafanya kazi bega kwa bega wa Jumuia ya kimataifa -

anaaminika??
 
Kwa sasa anaeongea ni spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na anasema kikatiba wabunge wanaotakiwa ni 393 jumla na waliopo ni 359 wakisubiri wabunge watano kutoka baraza la wawakilishi, wateule 10 wa Rais, viti maaum kutoka vyama vingine.

Kwa sasa spika anamkaribisha Rais Magufuli kuhutubia

=========

MAGUFULI: Kabla ya kuanza hotuba yangu, nawasihi tusimame tumkumbuke mheshimiwa Mkapa pamoja na waheshimiwa wabunge waliofariki dunia tangu kufungwa kwa Bunge la 11.

Nitumie fursa hii kuwaahidi, serikali ninayoiongoza itaendelea kuwaamini wanawake katika kushika nafasi mbalimbali za uongozi.

Napenda kuwapongeza wabunge kwa kuchaguliwa kwenu, mmechaguliwa kwa kuwa mna uwezo, nawasihi msiwaangushe wananchi waliowachagua, wananchi wana Imani kubwa sana.

Nimekuja kulizindua Bunge hili baada ya nchi yetu kufanikiwa kumaliza uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba mwaka 2020 kwa uwazi, amani na utulivu mkubwa.

Kwa msingi huo napenda kuipongeza tume ya Taifa ya uchaguzi kwa vizuri zoezi la uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

=>Namuahidi Dkt. Mwinyi kwenye miaka mitano ijayo, Serikali ya JMT itatoa ushirikiano mkubwa wa kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Zanzibar

=> Tutafanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kuleta maendeleo kwa pande zetu zote mbili za muungano

=>Tumethibitisha uwezo mkubwa katika kusimamia Uchaguzi bila kutegemea misaada kutoka nje

=> Uchaguzi wa mwaka huu uligharamiwa na Serikali kwa 100% ambapo kiasi cha Bilioni 331 kilitengwa. Hata hivyo mpaka Uchaguzi umekamilika Tume imetumia Bilioni 262 tu

=>Kwenye miaka 5 ijayo tutaendelea kuimarisha utawala bora hususan kwa kusimamia kwenye utumishi wa umma

=>Tutazidisha mapambano kwenye dhidi ya rushwa, wizi, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.

=>Natoa shukrani kwa watanzania wenzangu wote kwa kushiriki vizuri na kuonesha utulivu mkubwa kwenye Uchaguzi uliopita

=>Hakuna shaka Uchaguzi huu kwa mara nyingine umethibitisha watanzania ni wapenda amani, tunajitambua, hatudanganyiki na tumekomaa kidemokrasia

=>Utumbuaji majipu utaendelea. Tutaboresha maslahi ya watumishi wote, watumishi wasiwe na wasiwasi wachape kazi

=>Tumeingia kwenye Uchumi wa Kati na tutazidi kukuza uchumi kwa wastani wa angalau 8% kwa mwaka na kutengeneza ajira zipatazo milioni 8

=>Tunakusudia kukuza kilimo biashara, mazao tunayolenga kuyapa kipaumbele ni pamoja na korosho, kahawa, pamba, chai, michikichi, miwa

=>Tunaagiza ngano nyingi na vyakula vingine kutoka nje, ni aibu kwa Tanzania, Waziri wa Kilimo nitakayemteua akaanze na hili

JITU LINAIBA KURA, HATA AIBU LINAHUTUBIA, LOL
 
Lissu asinyeweza kutoa hotuba Kama hiyo hana uwezo huo hotuba imekaa vizuri kila Kona
Hatuwezi pata maendeleo makubwa ya uchumi bila viwanda; hakuna viwanda bila rail, barabara, ndege, na nishati

Mungu ibariki Tanzania
 
Hotuba yake inatia matumaini mazuri. Mambo mengi aliyoyasema ni mazuri Ila ili kujenga nchi yenye watu wamoja ningetamani sana kama angekutana na wapinzani wake ili kuwe na maridhiano ya kitaifa. Tuache chuki ambazo hazijengi kisha tuchape kazi tukiwa wamoja.

Ampe cheo Lisu kama alivyomuhaidi kwenye kampeni. Tukiwa wamoja hii nchi itapiga hatua kubwa sana kimaendeleo na sio kufanya ubabe kwenye kila kitu.
 
Lissu alikataa cheo ,
 
Mtanzania wa kwanza na ni muafrika wa Tatu baada ya Mandela na Kofi Annan kuhutubia bunge la ulaya lenye wajumbe 790 huwezi kulinganisha na mtu anaehutubia Halmashauri kuu ya CCM yenye wageni wawili waalikwa
Lissu Ni mwanasiasa wa kwanza kutoka Afrika kwenda kuchongea nchi yake kwa wazungu.

Mandela, Museveni , Kagame ,Laila Odinga nk hawajawahi kwenda ulaya au bunge la ulaya kuchongea nchi zao katika harakati zao za kisiasa wakiwa wapinzani.

Lisu Ni mwanasiasa mwafrika wa kwanza kwenda kuchongea nchi kwenye mabunge ya wazungu.

Hivi hajisikii aibu kuwa msaliti nba moja wa kiafrika kusimama kazungungukwa na wazungu watupu bungeni kusalitinchi yake?
 
Hotuba yake inatia matumaini mazuri. Mambo mengi aliyoyasema ni mazuri Ila ili kujenga nchi yenye watu wamoja ningetamani sana kama angekutana na wapinzani wake ili kuwe na maridhiano ya kitaifa. Tuache chuki ambazo hazijengi kisha tuchape kazi tukiwa wamoja.

Ampe cheo Lisu kama alivyomuhaidi kwenye kampeni. Tukiwa wamoja hii nchi itapiga hatua kubwa sana kimaendeleo na sio kufanya ubabe kwenye kila kitu.
Hamna mtu anataka cheo cha kupewa kama zawadi.
ngoja tuone maendeleo watayoleta wakiwa wenyewe bila wapinzani maana amesikika kila mara akisema wapinzani wanamchelewesha sana kuleta maendeleo.
 
Mh. Askofu Gwajima kapewa nafasi ya kushukuru hotuba ya Rais kwa niaba ya wabunge,,,,
Mdee kazima tv yake hahahahah!
"...hakuna beberu atakayekupenda kwa projection ya hii hotuba yako...." Mh. Gwajima (MB)
 
Hotuba yake inatia matumaini mazuri. Mambo mengi aliyoyasema ni mazuri Ila ili kujenga nchi yenye watu wamoja ningetamani sana kama angekutana na wapinzani wake ili kuwe na maridhiano ya kitaifa. Tuache chuki ambazo hazijengi kisha tuchape kazi tukiwa wamoja.

Ampe cheo Lisu kama alivyomuhaidi kwenye kampeni. Tukiwa wamoja hii nchi itapiga hatua kubwa sana kimaendeleo na sio kufanya ubabe kwenye kila kitu.

Ni kweli hii hotuba imegusa nyanja zote.
Rais alishaahidi kumpa Tundu kazi, ila Tundu ameshaondoka ameenda kuanza kazi ya kuhutubia mabunge ya wazungu huko alikoenda
 
Mtanzania wa kwanza na ni muafrika wa Tatu baada ya Mandela na Kofi Annan kuhutubia bunge la ulaya lenye wajumbe 790 huwezi kulinganisha na mtu anaehutubia Halmashauri kuu ya CCM yenye wageni wawili waalikwa
Dah....akili za kitumwa hizi... Afrika bado sana kujitawala...[emoji2960]
 
Back
Top Bottom