Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,992
Hapa niandikapo, Rais Magufuli amehitimisha hotuba yake. Sasa hivi anaongea Rais Museveni.
Hotuba ya Rais Magufuli imejikita katika kuchambua faida ya bomba la mafuta toka Uganda. Lakini kilichojitokeza hasa ni ile "tone" ya Magufuli. Alikuwa anarudiarudia maneno, hana amani, tofauti na Museveni ambaye anaonekana katulia, hana wasiwasi.
Kali zaidi aliyotoa Magufuli ni kudiriki kutamka kwamba kitendo cha Rais Museveni kutua hapo Chato kwa ndege yake, ni mfano hai wa MANUFAA YA UWANJA WA NDEGE WA CHATO. Na akasema wazi kuwa hii ni jibu kwa "wale" wanaodai uwanja huu hauna maana.
Kwa kweli hapo nilimhurumia Rais Magufuli. Kwanza kwa sababu baada ya Magufuli kuondoka madarakani marais wajao wa Tanzania watalazimika kufanyia angalau baadhi ya shughuli zao Chato, ili uwanja wa ndege wa Chato ufanye kazi?
Lakini pia hapo hakuna hoja. Museveni angeweza kutua Makao makuu Dodoma. Amelazimika kutua Chato ili kukidhi haja za kikampeni za Magufuli .
Hili tukio lenyewe lina harufu kali ya kampeni zaidi. Ni kama Magufuli kamuomba Museveni amsaidie KALUMUNA wake. Niseme wazi, hapa nahitaji data zaidi, niko tayari kusahihishwa. Lakini nilivyoangalia tukio zima, baada ya zile shamrashamra za Tanga mwaka ule, mkutano huu wa leo hauna substance. Ni panic tactics za kumpandisha Magufuli , kumtoa sakafuni alupogaragazwa na Lissu. Napata uhakika kutokana na kutetemeka kwa Magufuli katika hotuba yake, na pia wote wawili hawajasema chochote kipya