Hotuba ya Rais Magufuli mbele ya Mgeni wake Rais Museveni imejaa Hofu ya Kampeni

Hotuba ya Rais Magufuli mbele ya Mgeni wake Rais Museveni imejaa Hofu ya Kampeni

Kuongelea bomba la mafuta ni geresha tu, Museveni kamletea mbinu za kampeni baada ya pumzi kuisha... waliyoongea faragha ndiyo hasa lengo la ugeni ule.

Uwanja wa kimataifa Chato ni tembo mweupe.
 
Tatizo nionavyo mimi lipo kwa wasaidizi wake kumruhusu kuongea badala ya kusoma hotuba ilio andaliwa. PhD ni msomi mkubwa sana, but who knows very much about a very little thing.

Kifupi ni kwamba hana wasaidizi, wote walishaamua kumpuuza sababu ya jeuri na ukatili... wamehofia kukosa ugali wao.
 
Lengo la hotuba ya Rais kurushwa mubashara ni ili Watanzania tuone na kusikiliza atakachosema. Nakushukuru sana kwa kumsikiliza. Mpende Rais wako. Ipende Serikali yako. Ipende nchi yako. Kidumu Chama cha Mapinduzi!!!!

Rais anasema nini zaidi ya kutapeli wananchi, na kufanya kampeni za bei rahisi na kumtumia rais wa nchi nyingine kuvunja diplomasia ya kimataifa kutokuingilia siasa za nchi nyingine? Mwaka 2017 kulifanyika igizo lingine kama hilo la kuweka mkataba wa huo mradi, na ikasemekana 2020 mradi utakuwa tayari. Siku ile mpaka wazungu wa Total walikuwepo, lakini igizo la leo hakuna mzungu yeyote wa Total, zaidi ya kundi haramu la ccm kwenye kampeni, na viongozi wawili wakiwatapeli wananchi. Au huu mkataba wa leo ni tofauti na ule utapeli wa 2017?

Halafu ukitaka kujua ni kampeni za kilaghai, eti ndani ya dakika 5 wamekubaliana kuwa Tanzania ipate 60% na Uganda watapata 40%, huku wawekezaji ambao ni total hazitajwa asilimia zao. Kisha watu wanashangilia hilo igizo!
 
Kiini cha ugeni ni hiki hapa tu, zingine zote porojo.
IMG_7481.jpg
 
Leo Tanzania imeshinda.

Hatimaye mradi utakaotupa faida ya asilimia 60 na ajira elfu 10 umekamilishwa kwa hatua muhimu.

Mungu yupo nasi.

Asante sana Rais Museveni upendo wako kwa watanzania tumeguswa nao siku ya leo itaingia katika vitabu vya kihistoria.

Magufuli tunakushukuru sana kwa jitihada unazozifanya kuhakikisha Nchi yetu inasonga mbele.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Rais anasema nini zaidi ya kutapeli wananchi, na kufanya kampeni za bei rahisi na kumtumia rais wa nchi nyingine kuvunja diplomasia ya kimataifa kutokuingilia siasa za nchi nyingine? Mwaka 2017 kulifanyika igizo lingine kama hilo la kuweka mkataba wa huo mradi, na ikasemekana 2020 mradi utakuwa tayari. Siku ile mpaka wazungu wa Total walikuwepo, lakini igizo la leo hakuna mzungu yeyote wa Total, zaidi ya kundi haramu la ccm kwenye kampeni, na viongozi wawili wakiwatapeli wananchi. Au huu mkataba wa leo ni tofauti na ule utapeli wa 2017?

Halafu ukitaka kujua ni kampeni za kilaghai, eti ndani ya dakika 5 wamekubaliana kuwa Tanzania ipate 60% na Uganda watapata 40%, huku wawekezaji ambao ni total hazitajwa asilimia zao. Kisha watu wanashangilia hilo igizo!
Ungelisifia ndio ningeshangaa!
 
Huo ndiyo uhalisia,mradi wa bomba la mafuta ulishazinduliwa Tanga Tanzania na Uganda pia walishafanya hivyo.Leo nimesikia walikuwa wanaufufua ingawa hatuambiwi ulikufa lini na sababu za mauti yake.Mzee Baba walikuwa anahalalisha Chato International Airport yake kuwa unaweza kutumika na marais wa nchi zingine.Ukiacha ndege ya Kenyatta na Museveni,ndege ngapi zingine zimewahi kuutumia?
Je,huo uwanja baada ya kukamilika umeshaingizia nchi mapato kiasi gani hadi sasa?
 
Ungelisifia ndio ningeshangaa!

Nisifie uhuni? Ni vyema ungesema kile kilichosainiwa chongoleani 2017 ni nini, na hiki kilichosainiwa leo kwenye kampeni za ccm ni nini. Bado karne hii mnafanya siasa za kitapeli, halafu utakuta gharama zote za Museveni kuja nchini kwenye hii episode ya kampeni, ni hela za umma.
 
Huyu mzee kachanganyikiwa kwa kweli!!! Kwa iyo ziara ya museveni kuja kumtembelea hasa kwa nia ya kumpigia kampeni ndo anasema faida za uwanja wa ndege chato????

Huyu mzee nadhani si mzima??? Hivi huwa anatuelewa tukisema ule uwanja Haina faida za kiuchumi????? Labda tumuulize Kuna ndege ipi ya abiria imewai kutua pale na ilishusha watalii wangapi???
Kaliamsha dude ngoja msomi wetu mutu ya watu Lisu kesho anaye
 
Hofu aache kuwanayo mbelgiji awenayo Rais JPM mwenye facilities zote za ushindi?
labda kama umeandika tu kishabiki ili kuendelea kuwafariji wachanyembe wenzako wa Chadema.
Laurà Bagbo wakati anavutwa kutoka uvunguni na akatoka akiwa na singlendi, bukta Aina ya kanyeaumo bila kusahau ndala papa na nguru unadhani yeye hakuwa na facilities zote za ushindi? Alassane ambae hakuwa na nyenzo ndiye akaapishwa kuwa rais na yule mzee nadhani bado ananyea debe.

Acha kukariri ndugu maisha ni mzunguko yupo mtu flani tena mkubwa akisikia jina la Lissu lazima n'nya igonge SAnLG au boxer.
 
Ni kawaida watoto wa mama wa jambo kulalama hata kwa mambo yasiyokuwa na maana!
Sasa huo mradi haina faida kwa nchi au??
 
Hapa niandikapo, Rais Magufuli amehitimisha hotuba yake. Sasa hivi anaongea Rais Museveni.
Hotuba ya Rais Magufuli imejikita katika kuchambua faida ya bomba la mafuta toka Uganda. Lakini kilichojitokeza hasa ni ile "tone" ya Magufuli. Alikuwa anarudiarudia maneno, hana amani, tofauti na Museveni ambaye anaonekana katulia, hana wasiwasi.

Kali zaidi aliyotoa Magufuli ni kudiriki kutamka kwamba kitendo cha Rais Museveni kutua hapo Chato kwa ndege yake, ni mfano hai wa MANUFAA YA UWANJA WA NDEGE WA CHATO. Na akasema wazi kuwa hii ni jibu kwa "wale" wanaodai uwanja huu hauna maana.

Kwa kweli hapo nilimhurumia Rais Magufuli. Kwanza kwa sababu baada ya Magufuli kuondoka madarakani marais wajao wa Tanzania watalazimika kufanyia angalau baadhi ya shughuli zao Chato, ili uwanja wa ndege wa Chato ufanye kazi?

Lakini pia hapo hakuna hoja. Museveni angeweza kutua Makao makuu Dodoma. Amelazimika kutua Chato ili kukidhi haja za kikampeni za Magufuli .

Hili tukio lenyewe lina harufu kali ya kampeni zaidi. Ni kama Magufuli kamuomba Museveni amsaidie KALUMUNA wake. Niseme wazi, hapa nahitaji data zaidi, niko tayari kusahihishwa. Lakini nilivyoangalia tukio zima, baada ya zile shamrashamra za Tanga mwaka ule, mkutano huu wa leo hauna substance. Ni panic tactics za kumpandisha Magufuli , kumtoa sakafuni alupogaragazwa na Lissu. Napata uhakika kutokana na kutetemeka kwa Magufuli katika hotuba yake, na pia wote wawili hawajasema chochote kipya
Week ijayo ataita Kagame....Lissu kaza kamba hivyo hivyo
 
Ule upara umebaki tu wa kuwashia njiti za viberiti,siku za mwisho za dikteta Adolf Hitler zilikuwa za huzuni akijua dola yake inakwenda kuanguka na axis power inakwenda kuwin ww2.Dikteta magufuli naye siku zake hizi za mwisho ni za huzuni kwakuwa anajua atadondoka kwenye uchaguzi ujao na chadema itachakua dola
Hili liko wazi
 
Tundu Lissu anamsubiri kwa hamu kwenye mdahalo ili watz wawakue vilivyo wagombea wao.....

Note: Wagombea wasiruhusiwe kubeba silaha ya aina yoyote
 
Back
Top Bottom