Hotuba ya Rais Magufuli mbele ya Mgeni wake Rais Museveni imejaa Hofu ya Kampeni

Mindi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2008
Posts
3,523
Reaction score
4,992
Hapa niandikapo, Rais Magufuli amehitimisha hotuba yake. Sasa hivi anaongea Rais Museveni.
Hotuba ya Rais Magufuli imejikita katika kuchambua faida ya bomba la mafuta toka Uganda. Lakini kilichojitokeza hasa ni ile "tone" ya Magufuli. Alikuwa anarudiarudia maneno, hana amani, tofauti na Museveni ambaye anaonekana katulia, hana wasiwasi.

Kali zaidi aliyotoa Magufuli ni kudiriki kutamka kwamba kitendo cha Rais Museveni kutua hapo Chato kwa ndege yake, ni mfano hai wa MANUFAA YA UWANJA WA NDEGE WA CHATO. Na akasema wazi kuwa hii ni jibu kwa "wale" wanaodai uwanja huu hauna maana.

Kwa kweli hapo nilimhurumia Rais Magufuli. Kwanza kwa sababu baada ya Magufuli kuondoka madarakani marais wajao wa Tanzania watalazimika kufanyia angalau baadhi ya shughuli zao Chato, ili uwanja wa ndege wa Chato ufanye kazi?

Lakini pia hapo hakuna hoja. Museveni angeweza kutua Makao makuu Dodoma. Amelazimika kutua Chato ili kukidhi haja za kikampeni za Magufuli .

Hili tukio lenyewe lina harufu kali ya kampeni zaidi. Ni kama Magufuli kamuomba Museveni amsaidie KALUMUNA wake. Niseme wazi, hapa nahitaji data zaidi, niko tayari kusahihishwa. Lakini nilivyoangalia tukio zima, baada ya zile shamrashamra za Tanga mwaka ule, mkutano huu wa leo hauna substance. Ni panic tactics za kumpandisha Magufuli , kumtoa sakafuni alupogaragazwa na Lissu. Napata uhakika kutokana na kutetemeka kwa Magufuli katika hotuba yake, na pia wote wawili hawajasema chochote kipya
 
Huyu mzee kachanganyikiwa kwa kweli!!! Kwa iyo ziara ya museveni kuja kumtembelea hasa kwa nia ya kumpigia kampeni ndo anasema faida za uwanja wa ndege chato?

Huyu mzee nadhani si mzima? Hivi huwa anatuelewa tukisema ule uwanja Haina faida za kiuchumi? Labda tumuulize Kuna ndege ipi ya abiria imewai kutua pale na ilishusha watalii wangapi?
 
Hofu aache kuwanayo mbelgiji awenayo Rais JPM mwenye facilities zote za ushindi?
labda kama umeandika tu kishabiki ili kuendelea kuwafariji wachanyembe wenzako wa Chadema.
 
Ukiona mtu anajanga uwanja wa ndege kwao, jua hana mpango wa kutoka madarakani. Hata Mobutu alikuwa hivyo hivyo...
Kwa kweli hapo nilimhurumia Rais Magufuli. Kwanza kwa sababu baada ya Magufuli kuondoka madarakani marais wajao wa Tanzania watalazimika kufanyia angalau baadhi ya shughuli zao Chato, ili uwanja wa ndege wa Chato ufanye kazi?
 
Ahahhaha,eti kuwashia njiti
 
1. CIA is Chato International Airport
2. KIA is Kilimanjaro International Airport
🤣 sikuwa najua mkuu.ila nimeona pembeni ya mahali ndege ya museveni imetua kuna kichaka kikubwa mno
 
Wakuu mimi mgeni kidogo kwenye Siasa, inakuwaje mgombea uraisi Magufuli anaendelea kuwa raisi wa nchi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…