Hotuba ya Rais Magufuli mbele ya Mgeni wake Rais Museveni imejaa Hofu ya Kampeni

Ni kawaida watoto wa mama wa jambo kulalama hata kwa mambo yasiyokuwa na maana!
Sasa huo mradi haina faida kwa nchi au??
Hapa shida siyo mradi. Shida ni jinsi anavyoutumia huo mradi kukidhi haja binafsi. Mfano anajaribu kuutumia mradi kuonesha kuwa uwanja wandege wa Chato una manufaa kwa taifa. Kama wewe unaamini uwanja wa ndege wa Chato una manufaa kwa taifa, basi tuko ligi tofauti
 
Labda anamaanisha na marais wanaofata watakuwa wanatumia uwanja huo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Tundu Lissu anamsubiri kwa hamu kwenye mdahalo ili watz wawakue vilivyo wagombea wao.....

Note: Wagombea wasiruhusiwe kubeba silaha ya aina yoyote
Ukitaka kufahamu Hutu Baba hana uwezo wowote,aalikwe kwenye mdahalo hata kwa kutumia lugha ya Kiswahili utasikia ana udhuru.Hana uwezo wa kujenga hoja kabisa.
Napendekeza DottoEmanuel Bulendu awe moderator wa mdahalo,Mzee Baba atagoma kuhudhuria.
 
Pole sana kwa kutoa hoja kwa hisia. Bila shaka hata hufuatilii taarifa sahihi kutoka sehemu sahihi. Total bado wapo na mradi upo. Kwani mnalivyoikejeli Mfugale Flyover leo hampitiPO? Mlivyozikejeli ndege leo hamzipandi? Mlivyosema ukarabati wa MV Victoria ni kiinimacho sio kweli, leo wana Chadema hawapandiMO wakienda na kurudi Mwanza na Bukoba tena na kunya mnakunyaMO?

Sasa kwa taarifa yako, Bomba la Mafuta litajengwa. Nyie ropokeni. SGR itaisha. Nyie ropokeni. Mwalimu Nyerere Hydroelectric Power itaisha. Nyie ropokeni. Na Daraja letu la Busisi/ Kigongo litaisha na ninyi mtaendelea kuropoka. Mwisho wa siku utakuwa mbaya kwenu kwani Watanzania hasa wenye macho na uelewa wanajua!
 

Umetaja mambo mengi ili kubadili hoja ya msingi. Suala hapa sio kuisha kwa huo mradi, bali ni usanii wa kampeni nyepesi kwa jambo ambalo lilihitaji kuwa limekalika hivi sasa. Tuko nje ya muda mlioletea mbwembwe, kisha mnarudia jambo lile lile la kusaini mkataba, kama ni jambo jipya kumbe ni kampeni za kichovu.

Ni nani anaponda hiyo mfugale flyover, hiyo pesa si kaitoa Mjapan Zaidi ya 90%? Ndege zina kelele nyingi ikiwemo kificho zilivyonunuliwa na tija yake kwa sasa v/s vipaombele vingine kama kilimo. Kabla ya hizo ndege watu walikuwa hawasafiri na ndege? Fast jet ilikuwepo na mkaihujumu.

Nani aliponda ukarabati wa meli? Hilo daraja la Busisi sio baya, lakini ni utekelezaji wa kukurupuka, unaenda kuweka 600b sehemu moja, badala ya kuweka viwanda. Hiyo 600b vingejengwa viwanda 1O vya 50b@ vya kimakakati si vingefanya makubwa na kutoa ajira kwa wengi?

Kuisha kwa SGR na SG sio issue kwani ni vingapi vimeisha mpaka leo? Kuisha sio issue Bali issue Ni vitaisha lini, na deni letu litakuwa kubwa kwa kiasi gani hapo ndio ngoma. Watanzania gani, sisi wenyewe ni watanzania lakini hatudanganyiki na siasa za kiki za kishamba.
 
Magafuli na Museveni wanatuch3zea michezo ya kishamba, kila baada ya muda fulani wanaitana na kusaini makubaliano, hivi ni makubaliano yapi hayo ambayo huwa hayakamiliki tu.

Mbaya zaidi wakikutana basi watalikuza hilo tukio kwa mbwembwe nyingiiii lionekane kama vile limefanyika kwa mara ya kwanza kumbe ni utopolo kama utopolo mwingine tu.
 
Kama unaunga mkono kelele za nini sasa? Unajua kuwa nyumbu shida sana!
 
Magufuli ataendelea kuwa Rais, na pia watz mtabanwa maradufu ya mlivyobanwa awamu ya kwanza yake
 
Kama unaunga mkono kelele za nini sasa? Unajua kuwa nyumbu shida sana!

Naunga mkono nini boss, usitake kuongea mambo mengi kufunika hoja ya msingi. Siasa za kitapeli wapelekeeni hao hao mazoba, huku jukwaani mnapewa kubwa yenu. Shubamiit.
 
Swali langu ni je katiba ya nchi inaruhusu rahisi kufanya mikataba ya kiimataifa nyumbani kwake?
 
Uitwe uwanja wa Museveni, ila naogopa utageuka kuwa uwanjwa wa fisi muda mfupi ujao.
 

Hakika umeongea Ukweli na Ukweli mtupu..!!
Kitendo Cha M-7 kutua Chato kipindi hichi cha Uchaguzi Ni Mkakati wa Kampeni baada ya kuona MAJI YAMEZIDI UNGA kutokana na Challenge toka kwa adui yake "Numero Uno" Mhe. Tundu Antipas Lissu ambaye imedhihirika mpaka sasa ndiye anampelekesha Jiwe....!!!
Jiwe ameingiwa na hofu na inaonekana kila hotuba yake lazima AJIBU HOJA ZA LISSU....!!!
 
Hoja ya uwanja was Chato ingenyamaziwa tuu maana kila anaejaribu kujibu anaharibu Yusuphu Makamba alisema hajajenga Magufuri wamejenga CCM,Kheri James nae anasemaChato IPO Tanzania kwahiyo ni halali kujenga bila kuangalia faida ya uwanja huo.Magufuri nae anamualika M7 kujibu hoja ya uwanja huo,kinyume chake wanaifanya hoja ya Lisu kuwa ngumu zaidi kujibika majibu hayajitoshelezi.
 
Lengo la hotuba ya Rais kurushwa mubashara ni ili Watanzania tuone na kusikiliza atakachosema. Nakushukuru sana kwa kumsikiliza. Mpende Rais wako. Ipende Serikali yako. Ipende nchi yako. Kidumu Chama cha Mapinduzi!!!!
Kidumu kilishatoboka kitambo mkuu. Labda mtafute diaba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…