Wilderness Voice
JF-Expert Member
- May 19, 2016
- 921
- 1,649
Wakati Mhe. Rais kikwete alipoingia madarakani mwaka 2005, alitoa hotuba safi sana, ambayo kweli tulikuwa na matumaini ya kuwa na Tanzania mpya, na yenye maendeleo ya kasi. Aliongelea mambo mengi ikiwepo uwekezaji, na kujali wawekezaji, kweli milango ilifunguliwa tulipata wawekezaji wa kila namna hata kule kariakoo walijaa wakiuza karanga na ufuta. Wawekezaji walipata sauti na kuwa wasemaji wa mwisho kwani hatukutaka kuwaudhi bali kuwabembeleza na kujikomba kwao.
Vibali vya kazi vilitolewa kama njugu, ili kuwafanya wawekezaji kuwa na wafanyakazi wenye vigezo wanayotaka wao. Tuliona makampuni ya uwekezaji yakiwa na maafisa wote wa juu kutoka nje ya nchi, huku watanzania wakiishia kuwa vibarua na kufukuzwa kazi muda wowote. Huku wakilipwa mishahara ya chini kabisa.
Leo rais wetu kasisitiza kuwa vibali vya kazi vitolewe haraka, bila usumbufu, na pia milango ifunguliwe kwa wewekezaji. Najiuliza tu, hivi nchi kama China, India, Singapore, na hapa africa kuna Ethiopia uchumi wake unakuwa kwa kasi zinategemea wawekezaji kutoka nje pekee? Kama ingekuwa hivyo kwa Kikwete tulijaza wawekezaji, ni nini Taifa lilipata au kufaidika?
Kwanini tusiimarishe uwekezaji wa ndani, ambao serikali iwawezeshe wazawa kuwekeza na si kudhani tutaendelea kwa huu uwekezaji kutoka nje pekee. Sipingi wawekezaji wa nje lakini nawasiwasi kulingana na historia hapo nyuma. Wawepo ila serikali isiwekwe mfukoni, na si vizuri kutoa vibali vya kazi kama njugu.
Mhe. Rais kaongelea Kuboresha ufugaji kwa kuwa na ufugaji wa kisasa, na kupunguza mifugo. Sawa na Rais kikwete wakati huo alitamba na hii hoja na kudai mifugo inakoda na mchungaji anakonda. Akadai kuondoa tatizo katika serikali yake. Sikuwahi kuona jitihada zozote zilizofanyika, mpaka anaondoka madarakani.
Hii leo rais wetu nae anakuja na mapambio yale yale ufugaji wa kisasa, kupunguza mifugo. Hapa katika kupunguza mifungo sioni kama ni hoja. Mungu katupatia mifugo, ni nchi ya pili kwa mifugo Afrika baada ya Ethiopia. Mbona Ethiopia hawana hoja ya kupunguza mifugo, ila wao wanaviwanda vikubwa na vidogo vya ngozi, wanatengeneza viatu, mabegi, mikanda nk. wanasoko la ndani na nje ya nchi tena kubwa sana.
Sisi tunafikiria kupunguza mifugo. Badala ya kuboresha mifugo. Tunataka ng`ombe wa kisasa! Ethiopia ng´ombe wengi ni wakienyeji.
Rais anasema atakusanya kodi kwa kubembeleza, kuchekeana, anasahau enzi za Kikwete kulileta dharau kwa serikali, watu walikwepa kodi hakuna alie fatilia.
Uzuri rais kakiri mwenyewe kuwa serikali ilikuwa katika maongezi na baadhi ya wawekezaji sasa wameanza kugoma. Mie niseme ngoja wagome tu maake mama yeye ndo amedai tuwabembeleze. Namshangaa analalamika. Anadai yeye na Magufuli ni wamoja, sidhani! Yeye amejitangaza kubembeleza kukusanya kodi, aendelee kubembeleza. Tutalipa tu.
Mwisho Rais naona anarudisha wazo la kujenga bandari ya Bagamoyo tena kasema tutake tusitake. Sisi tunataka lakini mkataba upelekwe bungeni ili ujadiliwe na kupitiwa na watanzania tujue.
Nashukuru Rais hajafuata mienendo ya Magufuli bali kachagua mienendo ya Kikwete. Upole kubembeleza, kusamehe, na kuiweka nchi kwa wawekezaji. Safi sana! Wakati wa Kikwete watu tulisema tunataka kiongozi mkali, asie ogopa, na mwenye uthubutu.
Mungu akasikia maombi yetu akatupatia Magufuli. Tukalalamika kwa Mungu Magufuli mkali, haya Mungu katusikia katupatia tena mama wa kubembeleza, pacha kama Kikwete tusije lalamika tena.
Nampenda mama, kama Rais kipenzi ila naona kivuli cha Kikwete ndani. Mama ningetamani ungekuwa na style ya uongozi wako kivyako vyako. Najua Kikwete ni mshauri wako kama ulivyokiri weye mwenyewe. Ungekuja kivyako vyako. Ila ili swala la machimbo kwenye mbuga zetu tafadhali mama lifikirie mara mbili.
Kuwekeza shirika la ndege, ATCL ilishawahi kuwekezwa hata shirika la reli matokeo kila kitu kilikufa, kuwa makini ktk hili. Ethiopia waliambiwa wawekeze shirika lao, waligoma hadi leo linajiendesha vizuri tu.
Hivi hatuna kabisa watanzania ambao ni wataalamu maswala ya anga na usafiri wa ndege wenye kuweza kuboresha shirika letu. Tuwaazime basi waethiopia walau waje kutuelekeza na kutupatia ujuzi. Shirika la ndege la Ethiopia wana miliki chuo cha marubani, chuo cha wahudumu katika ndege, wanachuo cha uongozi na usimamizi wa ndege, wanachuo cha ufundi wa ndege, pia Shirika la ndege linamiliki hotel kubwa ya nyota tano. Mambo yote wanafanya wenyewe. Kwanini sisi watanzania tushindwe, na kuamini wengine wanaweza sisi hatuwezi? Kwanini narudia kwanini?
Kero za watanzania toka nazaliwa hadi leo ni zile zile, wawe wabunge, wanalalamikia mambo yale yale, hivi serikali imeshindwa maliza kero za wananchi. Migogoro ya ardhi , hivi kweli migogoro ya ardhi haiwezi malizwa? Viongozi tumewachoka, hakuna maono, nini kifanyike! tunahitaji sasa viongozi wenye maono mapya, na kutekeleza maono hayo bila kuogopa. Wanao sababisha migogoro ya ardhi ni serikali za mitaa, tunashindwa kweli kuwabana maafisa ardhi? Tunashindwa kupima ardhi yetu?
Tunasikia madawa hakuna, hivi serikali ili linashindikana? Kweli madawa ati yanakosekana? Ati maji hatuna wakati nchi imebarikiwa kwa maziwa, mito na bahari! Dubai ni kukame, lakini wameondoa shida ya maji! sisi tunaviongozi wapo tu! Kuna muda nawaza kuwa hatuhitaji mawaziri? Yaani sioni wafanyacho zaidi kujipendekeza kwa Rais.