Hotuba ya Rais Samia naifananisha na ile ya Mzee Kikwete alivyoingia madarakani

Wakati Mhe. Rais kikwete alipoingia madarakani mwaka 2005, alitoa hotuba safi sana, ambayo kweli tulikuwa na matumaini ya kuwa na Tanzania mpya, na yenye maendeleo ya kasi...
Nchi zilizofanikiwa zilibeba wawekezaji wa ndani, hawq wa nje wengi ni wa kuja kuchota rasilimali.

Amezungumzia uchumi wa bahari na kusema serikali itanunua meli nane ambazo nne zitatumika bara na nne visiwani. Tanzania bara ina eneo kubwa la bahari kuanzia bagamoyo, Dar es salaam, Tanga, Lindi na Mtwara kwanini agawe nusu bara na nusu visiwani, asitumie pesa za watanyika kuendeleza Zanzibar kama angetaka kuwapendelea angewapa meli mbili
 
Hicho kitu kipo kila nchi, hivi unajua hasara ya kukaa bila wananchi wako kuwa na ajila . Unazalisha vibaka, majambazi, mateja, malaya na shuguri nyingine zisizo halali.
 
Yote uliyoandika ni mawazo ya Kimasikini, yaani wewe hutaki Maendeleo

Hutaki kuona Bandari ya Bagamoyo ikijengwa na Tanzania kuchukua nafasi yake kama lango kuu la Africa Mashariki na Kati, huku mamia kwa mamia ya Watanzania wakipata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja. Mji ukikua na uchumi kupanda.

Wewe hutaki vibali vya kazi vitolewe ili tupate wataalamu wakati na sisi tunajitahidi kutengeneza skills za maana badala ya degree za ukarani tunazotoa. Mfano mtu anaanzisha kiwanda cha kurefine mafuta hapa analeta Bleacher hakuna mtu wa kuiendesha Tanzania kwanini anyimwe kule Muhindi hata kama hajasoma?
 


Mods pls TUNZENI HII KOMENTI, SAWA!??? (Hata kama mtahitaji malipo kidogo tutawapeni 🙂 )
 


Au kwa vile Zenj imezungukwa na bahari!??? (May be!???)
 
Kikwete alitoa hotuba nzuri kwa sababu alikuwa anamaanisha kufanya kile alichokuwa anaongea toka ndani ya roho yake. Hata hivyo, alivyoanza kazi akaja akagundua kuwa anapokuwa anatuambia twende kulia ili tuweze kufanya kile alichotka tukifanye, sisi tunakwenda kushoto, na aanaposema twende kushoto sisi tunageuka tena tunakwenda kulia.

Mama naye pia ameongea akiwa anamaanisha kile alichoongea, toka ndani ya roho yake. Kisipotokea kama alivyoongea, ujue kuwa tatizo lililotokea wakati wa Kikwete limejirudia
 
Hicho kitu kipo kila nchi, hivi unajua hasara ya kukaa bila wananchi wako kuwa na ajila . Unazalisha vibaka, majambazi, mateja, malaya na shuguri nyingine zisizo halali.
Wapi ukiajiri mtu wanakwambia huyo vigezo vyake havifai?
 
Kwa hiyo unamaanisha utawala wa Kikwete wananchi ndo tulikuwa na matatizo? Wananchi ndo walikula rushwa. Wananchi ndo walishindwa kupanga bajeti imara? Wananchi ndo walisababisha huduma mbovu ktk sekta mbalimbali na ofisi za umma? Je wananchi ndo walifanya ufisadi wa EPA na Richmond?
Najiuliza tu unavyosema wananchi tulishindwa kufanya alichotaka tufanye.
 
Nadhani umekurupuka. Wapi nimesema sitaki bandari ya Bagamoyo ijengwe. Tulia soma uelewe. Nimesema hakuna anae kataa Bandari kujengwa. Kikubwa mkataba wa ujenzi uwekwe wazi hata upelekwe bungeni.
Wewe ndo unamawazo ya kimasikini na haujui dunia inaendaje. Kokote kule ulimwenguni nchi ujali wataalamu wake kwanza. Unawekeza kwa wazawa. Tanzania inawataalamu kila aina.Hata hayo mafuta unayosema kurefine wataalam tunao. Ukikoswa ndo unatafuta wataalamu nje. Hapo nimeongelea vibali kutotolewa ovyo.
Uwe unasoma mada unaelewa usikurupuke kujibu tu bila kuwa na tafakuri ya kina.
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maono na maarifa!
Uko na familia unalialia kila kukicha kwa jilani akufanyie mambo yako kwa kujiona huwezi huu nao ni ujuha! Ndio maana nitaendelea kumpenda na kumkumbuka Magufuli wetu! Tz na watz kwanza, wengine baadaye! Nchi inajengwa na wenyewe wenye moyo wa kujitoa hata uhai wao!
Hii 'dependency syndrome' haipo sawa kabisa! Kutegemea mjomba eeh🙊!
Uwekezaji wowote Yz lazima uwe na tija, utoe ajira 'decent' zenye staha siyo za kikoloni za kufagia tuuúuuuuu😡! Unakuwa na kampuni la nje ambalo halina mtz hata mmoja ktk safu ya uongozi na utoaji maamuzi, mwishowe mnaishia kudanganywa tu kwa kinachoendelea 😭! Kodi inabembelezwa🤣😂🤣😂🤣!
 
Sijui ni utapiamlo wa akili au nini 🤔 kinachokutatiza I see!
Hebu msome vizuri mleta uzi kwanza kabla ya kujibu kwa kukurupuka i see!
 
Hakuna nchi duniani watu wanalipa kodi kwa hiari. Bali nchi zilizoendelea kuna mifumo ya malipo (electronic) inalolazimisha mtu kulipa kodi bila kugombana naye. Wewe unajua ni kwa nini mpaka leo miamala mingi zaidi hufanyika kwa cash? Siku serikali ikiacha uvivu na akili ndogo tutapata suluhu ya kodi. Ila kutaka kuwabembeleza ni kichekesho. Tutaanza kucheka muda si mrefu.
 
Kwenye suala la Kazi mkuu Hongera kama wewe ni mchapa Kazi, ila UKWELI ni kwamba asilimia kubwa ya Watanzania ni wavivu kupindukia kuanzia wa chini mpaka mabosi wao, unaenda ofisini kwa mtu anakukalisha masaa manne Kazi ambayo angeifanya dakika 15,mimi ni HR, katika kampuni ambazo nimewahi kuajiri wageni hakuna hata mgeni mmoja aliwahi kuharibu Kazi, nilijaribu kuwatafutia makosa wale walikuwa wananyanyasa wabongo, walifukuzwa tuu kwa sababu mimi nlikuwa naaminika lakini hawakuwa wameshindwa Kazi. Wabongo seriousness ni zero alaf tunapoteza muda kwenye mambo ya kijinga hospitali manesi wa zamu usiku wanakesha wanachati,tusipobadilika wageni watakuja kuwa hata waosha vyoo sisi tukiwa tunalalamika.
 
Mzee wa msoga na masalia yake akili ndogo sana kuongoza nchi. Mpaka leo sijui ni kwa nini Bro Magu alipeleka majina mawili kamati kuu 2015. Angepeleka la Mwinyi peke yake huenda leo hii nchi isingeshikwa tena na haya majangili.

Kwa kifupi mleta mada alizisikia vema hotuba za JK 2005. Hotuba ya huyu bi mkubwa ilipofika nusu saa tu kuna mtu nilimwambia kuwa ile hotuba iliandaliwa na watu wale wale walioandaa ya bosi wake 2005.

Sijajadili content kwa kuwa mleta mada ni kama kaudukua ubongo wangu. Bandiko lake litasimama kwa miaka yote ya utawala huu akili ndogo.
 
Sasa hapo ukiwa mzalendo suluhu siyo tu kuendelea kuajiri hao wageni. Bali suluhu ni kuleta hiyo nidhamu kazini. Ndiyo sababu Magufuli alikazania hicho kitu.

Baba mwenye akili hawezi tu kulemaa eti "shambani kwangu siwapeleki wanangu kulima, wavivu sana wale; nawatumia wa jirani yangu ndiyo wachapakazi!".

Lazima serikali itatue matatizo yetu ya msingi ili tuajirike badala ya kuwatukuza hao wageni. Rais wenu alidai kuwa kwenye miradi wataalam wa kibongo hawawezi kukuelezea kitu kikaeleweka. Binafsi najua hilo hajalitoa field bali ni mtazamo wake tu wa kitumwa.

Wataalam tunao. Tuwekeze kwa Watanzania. Tuwajengee uwezo zaidi. Tujenge pia mifumo imara ya kuwa-check. Tulikwisha anza vema ila sasa tunarudi nyuma.
 
Naheshimu maoni yako.
Kwa bahati nzuri,sikufahamu na hunifahamu pia.Unapoongelea nchi zilizoendelea inakuwa kama wajisemea kwamba wewe pekee ndiye wazifahamu nchi zilizoendelea? Ungenifahamu,hii isingekuwa hoja,ungejikita kwenye hoja tu.Itoshe kusema kwamba ninapoongelea hiari katika kulipa kodi ninamaanisha kujua umuhimu wa kulipa kodi kwa ajili ya kuchochea maendeleo kuanzia mtu binafsi hadi taifa kwa ujumla wake.
 
Mimi ni mmoja wa watu waliomuunga mkono JPM kwa mambo mengi tu aliyokuwa akiyafanya kwa mustakabali wa Taifa hili.

Lakini hili suala la kuwanyanyasa wafanyabiashara kama sio raia wenye haki na nchi hii ni kosa kubwa sana lililoutia doa muda wote aliokuwa rais wetu.

Kuna unyama mkubwa wamefanyiwa wafanyabiashara. Rais Samia anayo haki kubadilisha mentality ya ukusanyaji wa kodi. Ukimtesa mtu anayo haki ya kukimbia na kwenda kwingine ambapo biashara yake inaheshimiwa.

Kunyanyasa wafanyabiashara kunaenda sambamba na kutovithamini vipaji vya kitanzania. Mohamed Dewji alitekwa na watu ambao mpaka leo hawajulikani lakini Rais wa Afrika ya Kusini amemteua kama mmoja wa washauri wake wa masuala ya uwekezaji.

Na tunao wengi tu wa aina ya Mo Dewji, wazalendo wenye vipaji vya kila aina lakini mwisho wa siku wananyanyaswa na kunyanyapaliwa mpaka wanakatishwa tamaa ya kuutumia uwezo wao kwa faida ya jamii nzima.

Mojawapo ya kanuni za TANU inasema nitautumia uwezo wangu kwa faida ya wote, ukikutana na kukatishwa tamaa au kunyanyaswa huwezi kuutumia uwezo huo kwa faida ya mtu yoyote yule.

Mama Samia anayo haki ya kuja na mtazamo wa kiungwana kwa wafanyabiashara, Huwezi kumtesa Bakhresa ukafikiri unamkomoa, utaishia kuwaumiza wafanyakazi wake maelfu na familia zao.
 
Kama unafanya utafiti lazima ufanye mapitio ya machapisho. Naongelea kitu nacho kifahamu. Na hakuna sehemu nimesema ni mimi tu nae jua hzo nchi. Sijaandika kushindana na mtu.
Kikubwa nimetoa mifano ninayo ifahamu. Hata hivyo nimeizunguka dunia hivyo niliyojifunza na share na yeyote. Kila mtu ana haki kuongea au kutoa uzoefu alonao. Mlinganisho na nchi nyingine ni jambo la kawaida. Ndo maana usafiri wa BRT nchi kadhaa zilikuja kujifunza Tanzania uendeshaji wake. Na vivyo hivyo Watanzania tutajifunza kutoka nchi zingine.
 
Naheshimu mawazo yako.

Wakati huo huo: Mimi pia mbali na kuizunguka dunia,nimeishi muda mrefu "kwa mabepari" tena katika nchi tofauti.Ni mtafiti pia kwa "nature" ya kazi yangu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…