Nikiwa mmoja miongoni mwa raia wa taifa hili napaswa kufungua mdomo hasa ktk mambo mazito na muhimu kama uchaguz mkuu wa mwaka huu.
Leo Juni 8, kupitia vyombo vikubwa vya habar kama DW na mitandao ya kijamii tumepata habari kwamba wakili maarufu na mbunge wa zamani Tundu Antipasi Lissu amekusudia kuomba ridhaa kupitia chama chake kugombea nafasi ya uraisi wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania.
Jambo hili limezua mjadala mkali ktk jamii, baadhi ya watu wakimbeza kuwa hatoweza kuishinda CCM ktk uchaguz mkuu, wengine hata wakimtukana hasa ktk mtandao wa Facebook lakini kiasi kaungwa mkono ktk mtandao wa tweeter, kila mmoja ana mtazamo wake lakini tusipingane kwa matusi bali kwa hoja zenye mashiko na maslahi mapana kwa taifa hili.
Binafsi namtazama advocate Lissu kama ifuatavyo;
1: Msomi aliyebobea hasa ktk sheria.
2: Mwanasiasa mahiri mwenye uwezo wa
kujenga hoja na kuitetea.
3: Ni miongoni mwa wanasiasa maarufu
duniani baada ya kunusurika kifo cha ris
asi mjini Dodoma na kutumia jukwaa la
kimataifa kuihabarisha dunia juu ya jarib
io la kutaka kumuua.
Hayo mambo makuu matatu (3) naamini wakili Lissu ndio nguzo zake za kutegemewa ambazo anahisi anaweza kugombea uraisi mwezi October 2020. Huku kipengere namba tatu (3) akitegemea kupata kura nyingi zilizojaa huruma kutoka kwa wananchi.
USHAURI KWA LISSU.
Namshauri asigombee mwaka huu kwa sababu kuu zifuatazo;
1: Raisi Magufuli kisiasa amekuwa more
popular it means hayupo mwanasiasa
wa kumshinda ktk uchaguzi mkuu 202
0, majority ya wananchi wanaridhishw
a na utendaji wa raisi Magufuli.
2: Upinzani mwaka huu watakosa sera z
a kujinadi mbele ya wananchi na waka
eleweka maana Magufuli ameingia kt
k nyoyo za watanzania.
3: CHADEMA sasa hiv imekuwa kama ny
umba iliyogeuka gofu baada ya kukim
iwa na wakazi wake.
Binafsi namhurumia wakili Lissu namshauri kubaki kuwa mpiga kura tu kwa wengine labda akagombee ubunge lakini sio uraisi wa Jamhuri, asubiri mpk 2025 Magufuli akimaliza muda wake lakini sio mwaka huu.