Uchaguzi 2020 Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Juni 08, 2020

Ukweli mchungu wasotaka kuusikia, sera zao ni JPM kafukuza wenye vyeti feki alitakiwa awaache (tusingemwelewa maana hangekuwa tofauti na watangulizi wake kukumbatia wizi), JPM kaiba 1.5 T (tunajua hajaiba bali kaibadilishia matumizi kwa maslahi mapana ya umma na tumeridhia), JPM ni dikteta anawabambikizia kesi wapinzani (ukweli wanaujua ila wanapotosha, tena hapa hajakaza ipasavyo bado, Zitto alitakiwa awe jela kwa kesi ya majuzi, hao wengine wote waloyafanya ni uhaini lakini bado wanabembelezwa tu, hapa tunataka aongeze kidogo), JPM hajaongeza annual increment (tunajua na alituomba tufunge mikanda tukakubali hivyo si hoja)....sijui hawa jamaa watakuja na kipi kipya, yote tunayajua na watanzania tumeridhia.
 
Hata mimi nimeona aibu kubwa sana. Yaani jamaa kaongea pumba tupu toka mwanzo hadi mwisho.
 
Nyumbu watakupinga tu wakati umetoa ushauri mzito Na muhimu sana
 
Haya una kazi ya udaktari kugundua ana matatizo ya kisaikolojia yanayohitaji matibabu ya zaidi ya mwaka mmoja?
 
Yaani wajane lazima kuwajali maana hata wewe inaonekana kabisa akili yako ilishakufa sasa umo kwenye kundi la kuokolewa maana kifikra hujiwezi ni mjane wa akili
 
Wewe huna masala kichwani kabisa
 
Leo hadi mods wameambua kuwaondoa pro ccm kwenye mjadala kwa kuondoa posts zao na kuzuia wasijibu chochote

Naona chadema ikipotea kabisa baada ya October ijayo
 
UTANGULIZI

Utofauti ni mkubwa sana wa vyama vya siasa tangu mwaka 1952 - 1965 ( tulipofuta vyama vingi) na kurudishwa vyama vingi tena mwaka 1992 - 2020. Utofauti huo upo katika ubora wa aina ya siasa iliyokua ikifanyika Mfano. Akina Marehemu Mzee Mapalala, Bibi Titi Mohammed, Suleiman Takadir nk. Walifanya siasa zenye ubora zenye maono na zenye lengo hasa ambalo ndio muhimili wa kuanzishwa kwa chama cha siasa.

Tofauti na vyama vilivyoanzishwa kuanzia mwaka 1992 - 2020 siasa zake zinakosa jambo moja kubwa nalo ni uzalendo na ile dhamira ya dhati katika kulitimiliza lengo la kuanzishwa kwa chama cha siasa.

Nimeisikiliza hotuba ya Mhe. TUNDU A. LISSU leo ni kajaribu kuirejea mara Mbili mbili nikidhani labda kuna kitu naweza kuambulia ila niliambulia kumaliza MB zangu tu.

Nitajaribu kuwa muungwa na kutiririka na flow ile ile aliyoitumia na kubainisha UPUUZI nilioubaini

**********

NCHI IKO NJIA PANDA

Ukitaka kuishi baada ya kifo chako hakikisha unafanya haya mawili katika uhai wako

1. Kuwa mtu mwenye kuamini katika Lile unalolifanya na kuhakikisha unalisimamia ipasavyo

2. Watangulize unaowaongoza dhidi ya maslahi yako au ya watu wako wakaribu...

Na huu ndio msingi Mkuu wa kiongozi.

UPUUZI WA TAL ni kwamba
Anahitaji kiongozi ambaye yupo tayari ku compromise msimamo na malengo yake ili kumridhisha jirani.

************

UCHUMI UMEANGUKA

Ugomvi wangu mkubwa siku zote kati yangu na wanaojiita wasomi ni pale wanapoujua ukweli nankuamua kuupotosha...

1. Serikali ya Tanzania si Serikali ya kwanza Duniani kumiliki shirika la ndege. IPO Ethiopian Airways iliyoasisiwa na aliyekua Rais wa nchi hiyo Hayati Tafar Macnon aka Haile Selasie.

Lipo shitika la Ndege la RwandanAir shirika linalomilikiwa na Serikali ya Rwanda nk.

Serikali karibu zote duniani zina mfumo wa mabenki ya aina mbili ambayo ni Mabenki ya community na Mabenki ya kibiashara, Mabenki ya community huendeshwa kwa jichobla Serikali ukiachilia mbali mabenki ya biashara.

Benki ya Poster, TIB zimekua benki za Serikali miaka dahari hivyo kumshutumu Magufuli na Serikali take ni kutofahamu historia ya nchi hii.

Serikali inafanya biashara ya Madini? Hata bila haya mtu msomi anasema Serikali inafanya biashara akisahau kwamba Serikali chini ya Wizara ya Nishati na Madini wamefungua magulio ili kudhibiti utoroshwaji na ukwepaji wa Kodi ya Madini hivyo Serikali kufanya kazi ya ku- monitor magulio na kuhakikisha Kodi inalipwa na kwanmwaka huu wamefanikiwa kukusanya bilioni 436.

Kuyatuhumu majeshi ya ulinzi na Usalama kunachangamoto kubwa sana, mfano:;

JWTZ na Maafisa wa Benki kuu kufanya operation kwenye maduka ya kubadilisha fedha, taarifa zilizopatikana ni zile zilizokua zikihusisha Mabenki hayo kusababishwa scarcity ya fedha za kigeni hasa dola ili kuiongezea thamani na kushusha uchumi wa nchi ambalo ni jaribio la economy sabotage ambayo ni JWTZ pekee wenye dhamana ya kosa Hilo kwani ni above pay grade ya polisi na TISS hawafanyi ambushing kwa mujibu wa sheria.

Swala la wakulima wadogo wadogo au wakati Mhe. Dr. Magufuli amekua mstari wa mbele katika kupandisha thamani ya mazao ya shamba hasa pale mara kadhaa alipokua akisisitiza mkulima asipangiwe bei ya kuuza mazao yake kwani hakuna aliye wasaidia kulima.

NCHI YA WAJANE, YATIMA NA VILEMA
Huyu Bwana mkubwa ukimfuatilia kwa umakini utagundua kwamba anachuki binafsi na Rais Magufuli ambaye kimsingi kamzidi Elimu na Uelewa

Hakuna Taifa lolote linaloweza kuvumilia kikundi kidogo au mtu mmoja kuhatatisha usitawi wa Taifa Mfano;

Wakati wa utawala wa awamu ya Kwanza ulishuhudiwa mauaji ya Komando Faraji Tamimu maeneo ya Kinondoni, kipindi cha Mzee Kikwete ambaye leo hii Tundu Lisu ameonekana kumsifu alitekwa kiongozi wa Mgomo wa Madaktari Dr. Ulimboka.

Mhe TAL anatakiwa kuuonyesha weledi wake wa kisheria hata anapokua anaongea kwa mihemko ya kisiasa yeye anajua kwamba Kifo cha Akwelina Akwelina hakina ushahidi wowote unaoonyesha kilisababishwa na polisi.

Aidha mwanamuziki Ney wa Mitego hakuna sehemu yoyote yenye rekodi kwamba alitekwa na kuteswa na polisi

UTAWALA WA KIIMLA
Mhe. Rais Magufuli alizungumza kauli hiyo lakini haikuwa direct bali katika muktadha wa kuhakikisha kwamba anawatumikia wananchi kwa dhati kiasi kwamba wananchi hawatafikiria tena kuhusu vyama vya upinzania

Katika tafsiri za sisisi ndio huweza kuleta mkanganyiko huo.

BUNGE DHAIFU
Hapa Mheshimiwa TAL alinishangaza Jambo moja amesahau kwamba mdomo huu huu anaoutumia leo hii kumsifu Mhe. Kikwete na Sika marehemu Samwel Sita kwamba walifanya vizuri amesahau aliutumia katika Bunge Lile kusema Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ni rais LEGELEGE wakamtunga majina lukuki kwa kumuita Dikteta Uchwara, Vasco Dagama, Boyz II Men nk.

Wakati wa Bunge la Mzee Sita wapinzani walianzisha hoja gani ya maana kwani hata zile zilizotikisa nchi ziliibuliwa na hao hao ccm Mfano wa Richmond iliyosababisha utenguzi wa Waziri Mkuu Edward Lowassa mwaka 2007 na lile la EPA?

MAHAKAMA MATEKA
Mahakama hii inakua mateka pale tu inapowapa haki wapinzani ila haki hiyo hiyo ukienda upande wa mashtaka mahakamaninakua imetekwa na Serikali.

Ni kweli zipo kesi ambazo zinautata Mfano ni zile za Masheikh wa Zanzibar. Japo haitusahaulishi ile kauli ya KOSA MOJA HALIACHI MKE kwani ni Rais huyo huyo ambaye kwankutumia mamlaka yake alimuachi huru Papi Kocha na familia yake.

‘FUNGO WA KIMATAIFA’
Kwa kitendo alicho kifanya USA kutambua Mji Mkuu wa Israel kutoka Telaviv kwenda Jerusalem ni kuwa "Fungo wa Kitaifa" nchi yeyote yenye Sovereignty inayo mamlaka ya kuamua Mambo yake yenyewe.

Sasa hivi tumepata Rais ambaye hatuimbishi kiitikio bali wimbo alioutunga yeye hivyo kama unadhani ili tuwe salama ni LAZIMA tuimbe nyimbo zao wakati huo umekwisha na huu ni msimamo ambao ni dira mpya ya Taifa langu Tanzania.

ULINISTUA PALE ULIPOAMUA KUTUAMBIA NI KWANINI UMEAMUA KUTANGAZA NIA

Yapo Mambo ambayo unayaongea kisiasa sana kiasi kwamba mtu akikufuata na kukuambia uyarudie unaweza kuruka futi 100

1. Utawaruhusu wananchi wanaoandamana waandamane kwa amani na polisi wafanye kazi ya kuwalinda
a. Nchi yetu ina dini kuu mbili ambazo ndio muhimili wa Taifa hili. Vipi iwapo watakao andamana watakua wakidai haki yao ya ndoa za Jinsia moja?

Utakaa upande upi?

b. Vipi vijana wetu wakidai haki yao ya kutoa mimba na kuendelea na masomo

2. Kuna ule msemo unaosema HUWEZI KUMRIDHISHA KILA MTU sasa hivi wanafunzi wanufaika wa Mkopo wa Elimu ya Juu wanataka waondolewe ile Riba ya asilimia 15 walipe principle peke yake.

Labda nikuulize kwakua swala hili ni la kisheria utuambie ukishaingia mkataba na mtu na hakuna kifungu chochote linachoruhusu mazungumzo unaamua kuzuka tu na kuugomea mkataba ule?

Watu wa pwani wanasema MAELEWANO HUWA PWANI BAHARINI NI KUVUA TU.

HITIMISHO
Wapinzania wa nchi hii wanayo kazi kubwa sana katika safari ya kujitambua na kuchambua mambo wanayotakiwa kuyasimamia.

Nimefanikiwa kuisikiliza hotuba ile kwa undani na kwa umakini mkubwa 90% ya alichokieleza ni Manung'uniko ambayo hauwezi kumpa mtu uhakika kwamba wewe ukivivaa viatu vyake utafanya tofauti.

Anazungumzia jicho kwa jicho ya Mahatma Gandi akisahau kwamba India bado inaishi maisha Yale Yale ambayo Mahatma Gandi alikua akiyapinga ikiwa ni pamoja na ubaguzi wa kidini, Rangi na umasikini uliotopea.

AHSANTE
 
Makamanda wao wanataka Uzi wanalia na vyombo vya habari kwamba vinamuogopa magufuli mwanzo walilia kwenye kesi maakaman baada ya kuanzisha no hate no fear na watu wakaingia mitin walianza kusema wanamuogopa magufuli [emoji24][emoji1787]
 
Sasa kama washauri wenyewe wakina Lema, Mdee, Jacob, Sugu na DJ unategemea nini? Wameamua kumtwisha dunia la misumali bila kujali mwenzao anahitaji wataalamu wa saikolojia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…