Haya ni matokeo ya makosa yaliyofanywa (kwa makusudi) na 'aliyeanzisha' mchakato huu wa katiba mpya. Suala la uwepo wa muungano na aina ya muungano yalipaswa kufanyiwa referendum kwanza kabla ya kuandika katiba.
Kwa namna mchakato huu ulivyokwenda, kuna uwezekano mkubwa tukawa tumepoteza mabilioni yaliyotumika pasipo kupata katiba mpya. Rasimu imetengenezwa on the basis of a three tier government, endapo wajumbe wa BMLK wakiamua tu kuwa wanataka serikali mbili na si tatu, kimsingi watakuwa wamevuruga mchakato mzima na kwa uhalisia kazi nzima ingepaswa irudi ifanywe tena na tume ya katiba. Si rahisi kwa BMLK kuja na Rasimu yenye msingi wa serikali mbili katika muda mfupi uliopo (labda kama watachukua katiba iliyopo (ya 1977) na kuibadilisha).
Ndio sababu Jaji Warioba alitahadharisha kazi ya BMLK iwe ni kuboresha Rasimu na sio kubadilisha hoja ya (za) msingi.