Mwenyekiti anaeleza kilichotokea jana. Kwamba baada ya kutokea kile kilichotokea, ni kwamba waliitisha kamati ya mashauriano. Katika kikao hicho wamekubaliana mambo yafuatayo.
- Kwamba baada ya kiapo watampokea Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti
- kwamba Warioba atahutubia kuanzia saa tatu na nusu hadi atakapomaliza
- semina zilizokuwa na utata zimefutwa badala yake semina ya kanuni itafanyika leo jioni na kesho
- Siku ya Alhamisi kutakuwa na semina itakayoongozwa na Wakenya.
- Semina juu ya historia ya Tanzania Bara, Zanzibar na Muungano imefutwa kwa vile kwa kadri utakavyoteua watakaoendesha semina hiyo, hawataonekana kama wamesimama kati kati
- Siku ya Ijumaa asubuhi, Mwenyekiti atatangaza Kamati 12 za Bunge Maalum
- Siku ya Ijumaa asubuhi, Rais atakuja kulizindua Bunge