Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Hivi wajua kwa nini katangulizwa M/kiti wa katiba Jaji Sinde Warioba badala ya kutangulia Rais kulizindua Bunge la katiba kwanza kama kanuni zinavyotaka?Bao la kisigino hilooooooo.
Tutajuta kumfahamu Sita na kumshabikia bila kufikiri sawasawa.
 
Hakika imani yangu kuwa ukweli hujitenga na uongo inazidi kuimarika. Nondo anazoshusha mzee Warioba bungeni muda huu ni nomaaaaa!

Kama kweli wabunge wa CCM wanajua anachokiongea huyu Jaji, basi ni wazi magamba wanajuta kumjua huyu mzee ambaye naona leo kaamua kutapika yote ya moyoni mwake na mzee anaonekana anaongea kwa hisia toka moyoni mwake kwa dhati kabisa.

Kuna wakti Prof Shivji alimdiscredit ila nimegundua kumbe kuna vitu Prof ameachwa mbali na huyu Jaji anayeongea kwa takwimu na uhalisia wa kinachoendelea ktk maisha ya watanzania wa kawaida. Maprofesa wengi wa CCM ndani ya bunge wamekuwa wadogo na inaonekana somo linawaingia haswaaa!
 
Kiukweli Warioba leo anawasilisha maoni halisi ya wananchi, nimeshawishika kukubaliana na maelezo yake.
 
Zikishatengenezwa hizo DVD zisambazwe kwa wananchi. Pia isambazwe kwa njia nyingine yoyote iwe ni kutengeneza mp3 n.k! Hususani ufafanuzi juu ya Muundo wa Muungano! Hii itawezesha kupata ukweli usioegemea upande wowote.

Kazi hii ifanywe na WanaHarakati au wengineo wenye mapenzi mema na nchi yetu! Ripoti yake inaelezwa reality na haiko biased
 
Mzee yupo vizuri sana aisee. Nipo namsikiliza kwa umakini mkubwa kupitia Redio Maria
 
Lema yupo mjengoni na yupo katikati ya wanawake huku akishika tama
 
Back
Top Bottom