Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haki za wanawake zinawekwa kwenye katiba?
Wanaume hatuna haki za kuwekwa kwenye katiba?
Haki za walemavu pia ndani ya katiba.
Mtu ana haki ya kumiliki mali na asinyang'anywe bila kupewa fidia stahiki.
Uraia ni mmoja tu,tena wa JMT
Mkuu, alikuwa nyima ya kiti cha Mwenyekiti ambako kuna Washroom. Nadhani alienda kupubguza maji au alienda kutafakari jinsi ya juu ya Muundo wa Muungano
Pamoja sana mkuuMama Samia anaongoza kikao sasa.
Mzee Warioba anaendlea.
Wabunge wengine ndio kwanza wanaenda nje!
Suala nyeti zaidi ya hizi tulizonazo la Muungano linachua nafasi sasa.
Bro.Zitto anaupdates Twitter.
Maelezo ya kutosha kuhusu 3 govt,Yanatolewa.
Haki za wanawake zinawekwa kwenye katiba?
Wanaume hatuna haki za kuwekwa kwenye katiba?
Haki za walemavu pia ndani ya katiba.
Mtu ana haki ya kumiliki mali na asinyang'anywe bila kupewa fidia stahiki.
Uraia ni mmoja tu,tena wa JMT
Ha ha ha ha ha ha ha ha! Mkuu mzee mgongo ulichoka siunajua tena umri alikuwa back ofisi akijinyoosha kidogo.
Ninaamini kuwa Wajmbe wote wa Bunge Maalum la Katiba ni watu makini. Ni watu wenye sifa mbalimbali za elimu,ujuzi na fani.Wanazo sifa za kuwafanya kuwepo Dodoma Bungeni. Kila Mjumbe anajua kilichompeleka Dodoma, yaani,kujadili na kupitisha Rasimu ya Katiba.
Ninaamini pia kuwa kulikuwa na ulazima wa kuwapa semina Wajumbe wa Bunge Maalum juu ya Kanuni zao wakati zilipokuwa zikiundwa.Mantiki hapa ni kuwa Kanuni hizo hazikuwepo kabla. Vyema walivyojadili na kukubaliana juu ya Kanuni zao achilia mbali Kanuni za 37 na 38 zilizobuma.Kanuni hizi zinajikita kwenye namna ya kufanya uamuzi Bungeni na kama itumike kura ya wazi au ya siri.
Lakini,siamini kama kuna ulazima wa kuwahutubia Wajumbe juu ya Muungano. Kila Mjumbe Bungeni humo ni mtanzania.Anajua,kama si kupitia shuleni basi mtaani,kuhusu Muungano. Na isitoshe,Jaji Warioba atawafafanulia vyema kuhusu Muungano na kujenga hoja za kwanini kuwe na aina ya Muungano wa Serikali tatu.Wasikilize kwa Jaji Warioba na waanze kujenga cha kujadili.
Nasema,hakuna haja ya wanaoitwa 'Wanaoujua Muungano' kwenda Bungeni na kutoa mhadhara juu ya Muungano. Itakuwa ni kupoteza muda na rasilimali nyinginezo. Itakuwa ni kufanya mashindano ya nani ni Mwalimu mzuri kwa Wajumbe na hiyo haitasaidia kitu.Na wala si suala lililowapeleka Dodoma.
Ni wazi kuwa kila Mjumbe anapaswa awe tayari au anaelekea kujisomea nyaraka mbalimbali zinazoweza kumsaidia kujenga hoja jadilifu wakati wa kujadili Rasimu ya Warioba. Hakuna haja ya kuwaleta 'Malecturer' wa Muungano katika muda huu.Muungano unajulikana. Sasa ni muda wa kujadili,kwa sababu zenye maana, aina ya muungano tuutakao. Hakuna haja ya mihadhara ya Mapuri,Ngwilizi,Kavishe au yeyote awaye juu ya Muungano.
Bunge Maalum lisigeuzwe 'Lecture Room'. Muda unakwenda na rasilimali zinazidi kuteketea.Si jambo jema hata kidogo
Wadau, naamini mmeamka salama na akili zimetulia baada ya yale yaliyotokea jana.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum ambayo ameyatoa jana usiku, ni kwamba Bunge litaendelea na kikao chake leo saa tatu kamili asubuhi. Kwamba, baada ya dua, wabunge ambao walikuwa hawajaapa watakula kiapo. Baada ya kiapo hicho ndipo Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba atakapowasilisha Rasimu ya Katiba. Na kwa mujibu wa makubaliano waliyofikia, ni kwamba Warioba ataongea hadi atakapomaliza hotuba yake.
Nami kama kawaida kwa kushirikiana na wadau wenzangu akinina Skype, MaishaPesa, Simiyu Yetu, Deo Corleone, kbm, Mkuu ya Kaya na wengine tutaendelea kuwaletea yatakayojiri. Hadi wakati huo, Stay Connceted.
-================================================================
UPDATES
Mwenyekiti anaeleza kilichotokea jana. Kwamba baada ya kutokea kile kilichotokea, ni kwamba waliitisha kamati ya mashauriano. Katika kikao hicho wamekubaliana mambo yafuatayo.
*Kwamba baada ya kiapo watampokea Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti
*kwamba Warioba atahutubia kuanzia saa tatu na nusu hadi atakapomaliza
*semina zilizokuwa na utata zimefutwa badala yake semina ya kanuni itafanyika leo jioni na kesho
*Siku ya Alhamisi kutakuwa na semina itakayoongozwa na Wakenya.
*Semina juu ya historia ya Tanzania Bara, Zanzibar na Muungano imefutwa kwa vile kwa kadri utakavyoteua watakaoendesha semina hiyo, hawataonekana kama wamesimama kati kati
*Siku ya Ijumaa asubuhi, Mwenyekiti atatangaza Kamati 12 za Bunge Maalum
*Siku ya Ijumaa saa 10 jioni, Rais atakuja kulizindua Bunge
Eee Mungu mlinde Warioba wetu yasije yakatokea ya Kolimba.
Pamoja sana mkuuWananchi wengi walijikita kwenye muundo kama njia ya kuondoa kero.
Haki za binadamu iliongoza kwa kutolewa maoni mengi ikifuatiwa na muungano.
Asilimia 60 ya Wanzanbari walipendekeza muungano wa kimkataba.
Wadau wengi walipendekeza serikali 3!!