Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

MZEE WARIOBA NI MTU HATARI SANA KATIKA KUJENGA HOJA, ANATHIBITISHA KUWA MWILI UNAWEZA UKAZEKA LAKINI AKILI IKAENDELEA KUFANYA KAZI VIZURI.

Joseph Sinde Warioba ni nguli wa kujenga hoja, kama umefuatilia uwasilishaji wake leo Bungeni ameonesha uwezo wa hali ya juu katika kuonesha uhalisia wa mambo hasa kuhusu muungano na muundo wa serikali. Ni rahisi kumbeza Warioba kwa kejeli za kisiasa lakini kupinga hoja zake kwa hoja mbadala ni kazi inayohitaji maandalizi ya hali ya juu.

Ndio maana waliofilisika sera kichwani, watu wanaotaka kusikia wanachotaka kusikia, watu wanaozuwia uhalisia kuchukua nafasi yake wanaamua kutumia fujo za kumzomea ili kufifisha uzito wa hoja za Warioba lakini wameshindwa.

Hongera sana Mzee Warioba kwa kutuelimisha.



waziri-mkuu-na-makamu-wa-rais-mstaafu-jaji-joseph-sinde-warioba.jpg
 
Dakika Zimeongezwa......Six Bhana,Somo Kalipenda Au....
 
Sitta anaongeza muda kidogo ili Warioba aendelee na hotuma kwani muda wa kazi wa serikali kwa ngwe ya kwanza ya siku umeisha
 
Vijana chukueni madini hayo, coz baadae tunahitajika kuwa nondo kama huyo mzee wetu, sio kama hao snitches wengine waliotuharibia nchi kisa chama!!
 
Sitta anaongeza dakika 30 za ziada ili Warioba aweze kuendelea vyema, hahaaa leo Sitta kapakwa mafuta akalainika kabisa
 
Hii ndoa ivunjike tu, Tubaki na Tanganyika yetu na wao na Pemba na Unguja yao.
 
Serikali tatu uraia mmoja ndiyo nini hii au ndiyo kujenga hoja unakokuita wewe.
 
Nina mashaka juu ya gharama za serikali ya muungano. Hawa wazanzibari sijui kama watachangia. Pia sijajua kama gharama hizo zitakuwa sawa kwa sawa baina ya pande mbili hizi
 
Rai wa nchi nyingine aruhusiwe kwenda kupiga kura na kugombea uongozi popote hii nayo imekaaje kisheria.
 
Wakuu, naomba kufahamu waliokua wakizomea wapo upande upi(kundi lipi) haswa??
 
Eti nguli? kuwa nguli bila kujali maslah ya wengi ni u p u u z i mtupu
 
Back
Top Bottom