MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,011
- 2,185
Mowapo ya hoja za gwiji wa kujenga hoja kama alivyomtunuka mwanzisha uzi ni kuwa 'Serikali ya Zanzibarimetunga Katiba yake inayopingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania'. Anaendelea kujenga hoja kuwa ndani ya Katiba ya Zanzibar, Zanzibar ni nchi, ina mipaka yake, bendera na wimbo.' Kwa maneno rahisi anasema ' Zanzibar imevunja Katiba ya Jamhuri wa Tanzania' Suluhisho la kuvunja Katiba kwa mujibu wa gwiji wa kujenga hoja ni kuhalalisha kuvunja kwa Katiba kwa kuandika Katiba Mpya inayoridhia uvunjivu wa Katiba. Ni tangu lini mkosaji akikosea tunaifuta sheria ili kumwondolea mkosaji kosa.
Mimi sio mwansheria, lakini najua kuwa sheria inabaki kuwa sheria mpaka itakatungwa sheria inayoibatilisha. Ndiyo hata sheria zilizokwisha ainishwa na tume ya Jaji Francis Nyarali kuwa ni sheria mbaya mpaka leo zinatumika kwa kuwa hazijaondolewa vitabuni. Kutunga Katiba juu ya Katiba ilikuwa ni kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama huo ndiyo ugwiji wa kujenga hoja kinzani/ tata basi na iwe hivyo.
Mimi binafsi ningemwita Warioba mtu mwoga wa kuwambia ukweli Wazanzibar kuwa wametunga katiba inayokiuka Katiba mama. Sheria mahali fulani tu au ya kimila kama inakinzana na sheria ya nchi sheria hiyo huwa batili au batilifu. Japokuwa Zanzibar ni sehemu ya Muungano na Tanzania bara pia lakini nchi hizi mbili zikitunga sheria inakinzana na Katiba ya Jamhuri waMuungano, sheria hiyo inapaswa kuwa batili.
Warioba ni mwoga kumwambia JK KUWA NI RAIS DHAIFU kwa kufumbia macho Zanzibar ilipokuwa inatunga Katiba inayokinzana na Katiba kuu. JK aliapa kuilinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini hajailinda na bado yupo Ikulu.
Ningalikuwa mimi ningalisema Zanzibar iondoe katika Katiba yake vingele vinavyokiuka Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Bila kufanya hivyo hakuna maridhiano. Uwoga unaubatizaje kwa jina UGWIJI?
Unajua timu ya Warioba haikutakiwa kukosoa katiba yetu ya muungano au ile ya Z'bar. Kazi yake ilikuwa ni kuleta rasimu ya katiba mpya. Mazingira aliyoyaeleza au uliyoyataja ni sawa na yale ambayo pia hata yeye aliyatoa kwa wananchi. Hayo ni msingi wa rasimu yake.
Waliozembea ni viongozi wa CCM, ni Rais. Wakati Z'bar wanafanya hayo Rais alikuwa wapi? just laughing! Warioba hana kosa lolote! anajuwa kilichotokea lakini vyombo vya kuhangaika na hayo vipo. Yaani una Rais ambaye aliona kabisa sehemu moja ya nchi ikijitangazia kuwa ni nchi na serikali yake, yeye akanyamaza kimya!
Nami namsifu Warioba ni genius! Ameweza kuwaacha waliotengeneza maovu watatuwe wenyewe na yeye ameleta rasimu ili tupate katiba mpya. Sasa hao wapuuzi waliko Bungeni kukataa eyi kwa sababu Nape kasema, hao ndo wanaotugawia ujinga, ili nchi nzima iwe ya wajinga.