Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Mowapo ya hoja za gwiji wa kujenga hoja kama alivyomtunuka mwanzisha uzi ni kuwa 'Serikali ya Zanzibarimetunga Katiba yake inayopingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania'. Anaendelea kujenga hoja kuwa ndani ya Katiba ya Zanzibar, Zanzibar ni nchi, ina mipaka yake, bendera na wimbo.' Kwa maneno rahisi anasema ' Zanzibar imevunja Katiba ya Jamhuri wa Tanzania' Suluhisho la kuvunja Katiba kwa mujibu wa gwiji wa kujenga hoja ni kuhalalisha kuvunja kwa Katiba kwa kuandika Katiba Mpya inayoridhia uvunjivu wa Katiba. Ni tangu lini mkosaji akikosea tunaifuta sheria ili kumwondolea mkosaji kosa.
Mimi sio mwansheria, lakini najua kuwa sheria inabaki kuwa sheria mpaka itakatungwa sheria inayoibatilisha. Ndiyo hata sheria zilizokwisha ainishwa na tume ya Jaji Francis Nyarali kuwa ni sheria mbaya mpaka leo zinatumika kwa kuwa hazijaondolewa vitabuni. Kutunga Katiba juu ya Katiba ilikuwa ni kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama huo ndiyo ugwiji wa kujenga hoja kinzani/ tata basi na iwe hivyo.
Mimi binafsi ningemwita Warioba mtu mwoga wa kuwambia ukweli Wazanzibar kuwa wametunga katiba inayokiuka Katiba mama. Sheria mahali fulani tu au ya kimila kama inakinzana na sheria ya nchi sheria hiyo huwa batili au batilifu. Japokuwa Zanzibar ni sehemu ya Muungano na Tanzania bara pia lakini nchi hizi mbili zikitunga sheria inakinzana na Katiba ya Jamhuri waMuungano, sheria hiyo inapaswa kuwa batili.
Warioba ni mwoga kumwambia JK KUWA NI RAIS DHAIFU kwa kufumbia macho Zanzibar ilipokuwa inatunga Katiba inayokinzana na Katiba kuu. JK aliapa kuilinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini hajailinda na bado yupo Ikulu.
Ningalikuwa mimi ningalisema Zanzibar iondoe katika Katiba yake vingele vinavyokiuka Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Bila kufanya hivyo hakuna maridhiano. Uwoga unaubatizaje kwa jina UGWIJI?

Unajua timu ya Warioba haikutakiwa kukosoa katiba yetu ya muungano au ile ya Z'bar. Kazi yake ilikuwa ni kuleta rasimu ya katiba mpya. Mazingira aliyoyaeleza au uliyoyataja ni sawa na yale ambayo pia hata yeye aliyatoa kwa wananchi. Hayo ni msingi wa rasimu yake.

Waliozembea ni viongozi wa CCM, ni Rais. Wakati Z'bar wanafanya hayo Rais alikuwa wapi? just laughing! Warioba hana kosa lolote! anajuwa kilichotokea lakini vyombo vya kuhangaika na hayo vipo. Yaani una Rais ambaye aliona kabisa sehemu moja ya nchi ikijitangazia kuwa ni nchi na serikali yake, yeye akanyamaza kimya!

Nami namsifu Warioba ni genius! Ameweza kuwaacha waliotengeneza maovu watatuwe wenyewe na yeye ameleta rasimu ili tupate katiba mpya. Sasa hao wapuuzi waliko Bungeni kukataa eyi kwa sababu Nape kasema, hao ndo wanaotugawia ujinga, ili nchi nzima iwe ya wajinga.
 
huwezi jua wewe kima.....Mchakato mzima ulifikkishia Lissu kuonekana ni mbaya kwa zenj aliposema Zenj wamevunja katiba ya muungano...na hii ilikuwa ktk sekeseke la kuunda tume na nini kiwepo ktk tume....

mkuu utajichosha bure , usihangaike na vijana ambao hawataki kufanya kazi , huyo bila ccm NAKUHAKIKISHIA KWAMBA ATAKUFA NJAA BAADA YA WIKI TU .
 
Kwa mujibu wa ripoti ya mwenyekiti wa tume ya kuandaa rasimu ya katiba inaonyesha kuwa takribani 61% kutoka Tanzania bara waliunga mkono hoja ya serikali tatu na 60% kutoka Zanzibar walipendekeza Muungano wa mkataba; ni wazi kuwa ripoti hiyo haionyeshi kiuhalisia wa jumla ya watanzania waliohojiwa na kutamka kwa vinywa vyao kuwa wanataka muundo wa serikali tatu.

Ripoti hiyo inasema “kwa Tanzania Bara wananchi zaidi ya 39,000 walitoa maoni yao kuhusu Muungano na karibu 27,000 walizungumzia Muundo (Hawakusema kama wanataka serikali tatu).

Kwa Zanzibar karibu wananchi wote waliotoa maoni walijikita kwnye suala Muungano. Kati ya wananchi karibu 38000 waliotoa maoni, wananchi 19,000walitoa maoni kuhusu muundo wa Muungano (hawakusema kama wanataka serikali tatu)”.
Sasa swali linalojitokeza ni je, hizi asilimia zinazoonyesha kuwa idadi kubwa ya watanzania wanataka muundo wa serikali tatu inatoka wapi? Ukweli wa mambo unaonyesha kuwa, kimsingi ni kweli kamati teule iliwahoji watanzania takribani 333,516; kati hao watanzania 16,470 walipendekeza muundo wa serikali tatu, kwa Tanzania Bara, wananchi zaidi ya 39,000 walitoa maoni yao kuhusu Muungano, 27,000 walizungumzia Muundo.
Kwa Zanzibar wananchi 19,000 walitoa maoni kuhusu muundo wa Muungano na wengi wakipendekeza muungano wa mkataba. Takribani wananchi 287537 hawakuzungumzia suala la muungano au muundo wa serikali tatu.
Sasa je, asilimia 61% inatonduka wapi amabyo inaunga mkono hoja ya muundo wa serikali tatu? Ni watanzania wapi wengi ambao wameonyesha nia ya kuwa na muundo wa serikali tatu?
 
Unamjua Wassira au unamsikia tu?
Kamuulize huyo Warioba Wassira ni nani kama hajakutoa nduki.

Hoja za huyo Warioba ni chache hazitoshi kwenye kiganja.
 
Leo ndio nimejua kwa mapana mengi san aya muungano na kwanini Zenj mambo hayakuwa yakienda.Ila sitokuwa na mchango kwa hawa watu nilispolisema hili. Sheria za kutoona mbali ziliizuia zenj ktk issue ya maendeleo..km kila kitu kilihitaji kupitishwa na baraza la wawakilishi zenj ndipo kifanye kazi.Kwa serikali km ya CCM kuanzisha wazo achilia mbali kupiti anjia zote ili kitanyike kitu ..ni tatizo. Wazenj kumzuia rais kuwa rais kwa matendo zenj..au hata waziri mkuu....kwa miaka yote hii ni wazi kuwa.....Zenj walijizuia mengi
 
kajitahidi sana.kipengele cha haki za raia kitaleta tabu znz. kuhusu watanganyika kumiliki ardhi znz.hilo naona gumu kwa wazanzibar

Hata sisi hatutaki ARDHI yenu,ILA TUNATAKA NA NYIE MSIMILIKI ARDHI HUKU.ARDHI SIO SUALA LA MUUNGANO!
 
By the way, huyu Mzee Warioba (salute) bado yupo ngangari sana aisee. Da, saa nne anahutubia akiwa amesimama bila hata kupepesuka! (najua alipumzika km dakika tano hivi lakini hilo haliondoi ukweli kwamba huyu Mze wetu (mungu ambariki sana) bado ana nguvu sana kulinganisha na wengine hata walio na umri chini yake. Angekuwa ------, angeshaaanguka mara tatu kama Yesu (samahani kumtaja Yesu hapa). Big UP Bro Warioba!
Mzee ni nouma..hata kutoka nje alikuwa akitaka waachia nafasi akili zzai zijichanganye .....na kuweza jadiliana kijinga ili akija piga msumari basi wajikute ktk ulimwengu kocha na mkunga wao Pinda /wassira/pindi chana/werema hawakuwahi hata kuota wafundisha... Na ndicho alichokifanya
 
Warioba na maoni sahihi ya wananchi wa Tanzania, JK na msimamo wa kulazimisha (batili) wa chama. Haya sasa.

Kwa msingi wa nchi mbili kamili ni muhimu raia wa Tanganyika uwe wa Watanganyika tu.hivyo hivyo kwa Zenj.Kwa hili Tume ilikwepa ukweli kwa Makusudi.Bunge maalum lisahihishe
 
Nadhani hujamsikiliza vzuri Warioba na hujamuelewa kwa nini tume imependekeza muundo wa serikali tatu.
 
mkuu soma vizuri ili ujue content yangu utaelewa wapi vijana tutumbulie macho ili kuokoa jahazi. sio mambo ya serikali 3 au 2 mambo ambayo wazee wameyavalia njuga ili kutuficha kujadili mambo muhimu kama nilivyoyaorodhesha ndo maana vijana sijui kama tunafika asilimia 30 kwenye hili bunge. siasa safi sio serikali 3 au 2 ni kuzingatia hayo mambo niliyoyataja ambayo bunge la wazee limeyaweka pembeni kupitia mgongo wa hizi serikali ili watupime uelewa vijana tusiwe wanyonge.
 
Poti Warioba, hongera na pole kwa kazi iliyotukuka. Kwa mara nyingine you have made Tanzanians proud,tuliotoka Mara kutembea kifua mbele kwamba tunatoka mkoa wa JKN, Warioba, Kyaro,Msuguri, Butiku nk ambao uzalendo na mapenzi yao kwa nchi yao sio ya kufundishwa wala kutiliwa shaka. Aidha nawahongera makamishina wote. you guys you fought so bravely like the lions of Serengeti in favour of your motherland. wazao wenu watawakumbuka na kuwaenzi daima.

jioni hii Ee Maulana kwa moyo wa unyenyekevu na shukrani nyingi, naomba niombe dua hii kwa niaba ya mtumishi wako Warioba kwa niaba ya makamishna na wanasekretari wote wa tume ya katiba.

"Baba kazi uliyonituma kwa niaba ya Taifa lako nimeimaliza, vita nimevipiga vema,safari nimeikamilisha na imani waliyonipa watanzania nimeilinda. Maulana wewe wajua kuwa sikugeuka kushoto ama kulia bali nilikaza nia kuifuta njia ya kweli walimopita wote walionitangulia waliokuwa na nia njema tangu mwl,Karume,Nyarali hadi Kisanga licha ya kukumbana na changamoto kali na nyingi tangu kutukanwa na kudharuliwa hata hivyo sikuicha njia.

Baba napomaliza kazi hii na kumwachia kijiti Sita naomba roho wako aliyekuwa nami siku zote amuongoze siku zote ili kukamilisha safari uliyoinzisha kupitia mimi na wenzangu. Mwisho Maulana nakuomba kwa hisani kubwa unijarie mimi na wajumbe wenzangu maisha marefu ya kuiona nchi tuliipigania kupitia mchakato huu na si kama tupendavyo sisi ila kwa kadri ya mapenzi na rehema zako, aidha tunamuombea pumziko la amani mjumbe mwenzetu ndugu Adriani Mvungi aliyetutangulia na kumpa faraja kwa kufanikisha kazi aliyoitolea jasho na damu kufanikiwa kwa kuwapa watu wako katiba ya viwango alivyovipigania ndugu yetu Mvungi. Naomba yote kwa jina lako Maulana Uliye Mkuu wa viumbe vyote na Mtawala wa milele, Amina!".

(ikiwa sara hii inaoana na nia ya moyo wako sema amina)
 
Kwa msingi wa nchi mbili kamili ni muhimu raia wa Tanganyika uwe wa Watanganyika tu.hivyo hivyo kwa Zenj.Kwa hili Tume ilikwepa ukweli kwa Makusudi.Bunge maalum lisahihishe
utakuwa si muungano kwa fikra zako.na muungano utakuwa umeweka hayo wazi....na alisema hayo bungeni leo mzee....pengine hangover ilikuwa nzito kwako.
 
Tatizo letu watanzania ni kupuuza mambo muhimu. Tume ya kukusanya maoni ilitoa ulingo mpana wa watu kutoa maoni yao kwa njia mbalimbali hadi SMS! Leo hii matokeo ya washiriki yanatolewa tunaanza kuhoji! Hii hutokea pia wakati wa uchaguzi. Watu hawajitokezi siku ya kupiga kura badala yake wanalalamika mteule kuwa bomu!
 
Kiukweli kile kipindi cha Je Tutafika kwenye mada hii ya Rasimu, upotoshaji ni mkubwa mno, halafu kipindi kiko Biased, waalikwa wake ni wa mrengo mmoja, kazi yao ni mapovu tu, hawajengi hoja zaidi ya kukariri tu!
Ndo hao makasuku mkuu. Licha ya ufafanuzi wa kina kutolewa leo na mzee wetu Warioba bado wao watakimbiliao watakimbilia TBC na kuanza ukasuku wao na jamaa aliyefilisika wa Channel TEN utamsikia wiki ijayo. Aibu tupu. Sijui baba askofu Pengo kasikiliza radio au kuangalia TV leo wakati wa uwasilishwaji wa rasimu!
 
Sitarajii kundi la lumumba litakua na mchango chanya kwenye huu uzi
 
Nilichokuwa nasema ni kwamba sasa JK aadhibiwe Ijumaa akienda mponda warioba..kura ya wazi ifanye kazi..Watu wamwache JK ndani.Na maCCM wenzie
 
Back
Top Bottom