Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Wabunge sasa mnajukumu kubwa sana la Kihistoria kujadili na kuboresha/kubadili Chochote kwa Maslahi ya Taifa na Vizazi vyake.
 
Natamani ile ndege ya Malaysia ingekua imewachukua na hawa wabunge wa bunge la katiba and Nape & the company.

Great thinking!I real like it.Congratulation.That Jet should have taken them all to an unknown place.
 
Inaoenaka CCM tukiwa peke yetu na tukiwa sehemu siri tunataka serekali 3 tukiwa mbele ya vyombo vya habari na watu tunataka srekali 2.
hapa ni wazi ndani ya CCM kuna tatizo.

KWANINI NIMESEMA HIVI


Kama tulivyomsikia Jaji warioba. Sehemu muhimu ndani ya serekali wamependekeza serekali 3.
Kwa mfano afisi ya waziri mkuu, afisi ya makamo wa rais. hizi kama sitakosea zimependekeza muundo wa serekali 3. Hizi ni Ofisi nyeti ambazo kazi yake ni kutatua kero za Muungano.kama zimependekeza muundo wa serekali 3 ni wazi kwamba kuna tatizo.
Hapa CCM tumeshika hatamu. Hapa kuna makatibu wakuu licha ya kutokwa watendaji wa Chama lkn wengi wao ni wakereketwa wa Chama. wakurugenzi na hata mawaziri wote hawa ni Chama chetu.
Kama haya ndio mapendekezo ya ofisi hizi mbele ya jaji Warioba ni wazi CCM pia inataka serekali 3 nyuma ya pazia lkn mbele ya vyombo vya habari inataka serekali 2.
Ofisi ya Bunge na ofisi ya baraza la wawakilishi. Hili kwa kiasi kiikubwa ndio wawakilishi wa wananchi. Kwa mujibu wa warioba hawa pia wamepndekeza serekali 3. hapa CCM imejaa.hapa ndipo alipo spika wa CCM , hapa ndipo penye wenyeviti wa CCM wa kamati za Bunge.Mapendekekezo haya yanaushawishi mkubwa kutoka ccm.




HII NI SEHEMEU YA MAPENEDEKEZO YA TAASISI ZA SEREKALI


103 .Baadhi ya taasisi za kiserikali, ama moja kwa moja au kwa tafsiri ya
mapendekezo yao, pia zilipendekeza au kukubali muundo wa Serikali Tatu. Kwa
mfano, Baraza la Wawakilishi Zanzibar lilipendekeza kuwepo kwa mamlaka huru ya
Zanzibar, mamlaka huru ya Tanganyika na mamlaka ya Muungano na iwekwe wazi maeneo, uwezo, nguvu, utendaji na mipaka ya kila mamlaka. Baraza la Ofisi ya Makamu wa Rais lilipendekeza, kuhusu Muundo wa Serikali kwamba, nanukuu
"kuwe na Rais mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wakuu wa Serikali za Washirika wa Muungano wapewe vyeo vingine 32 vinavyoendana na hadhi na mamlaka zao. Pia katika kutaja hizo serikali tatu inabidi zitenganishwe ili Serikali ya Muungano ionekane ndio ya juu"

104. Baraza la Ofisi ya Waziri Mkuu lilipendekeza, kuhusu uongozi wa taifa kwamba kuwe, na "Rais wa Jamhuri ya Muungano, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Waziri Mkuu wa Serikali ya Tanganyika na Waziri Mkuu wa Serikali ya Zanzibar. Mapendekezo hayo ni kwa sababu hakuna umuhimu wa kuwa na marais watatu (3) katika nchi moja na wala neno Rais halimuongezei hadhi kiongozi yeyote. Pia kutoa nafasi kwa Mawaziri Wakuu kuwa watendaji zaidi na hivyo kusimamia Serikali za Washirika." Aidha, Bunge la Jamhuri ya Muungano katika maoni yake
lilipendekeza kuwepo kwa Tume ya Utumishi wa Bunge ambayo o inajumuisha, katika Wajumbe, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano (Mwenyekiti), Spika wa
Bunge la Tanzania Bara na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.


- Eti kama ninakuelewa unasema CCM hawaminiani ila Wapinzani ndio wanaaminiana au what?

Le Mutuz
 
Revocatus Kashaga, naona unaongelea issue ambayo iko nje ya uwezo wako wa kufikiri. Opinion polls ni Sayansi na huendeshwa kitaalam kwa kufuata misingi ambayo kama utapenda kuielewa, labda thread ifunguliwe. Shida yako kubwa nadhani ni kutoelewa principle inayoongoza utafiti wa maoni ya walio wengi katika jamii. Hakuna namna unaweza kuwauliza Watanzania milioni 45 mawazo yao kama unavyotamani ingefanyika, badala yake unatumia kitu kinaitwa sampling. Ndio maana kwa nchi kama Marekani yenye watu zaidi ya milioni 350, maoni ya watu 35,000 (0.1%)kwa mfano, inatosha kabisa kuonesha wazi muelekeo wa wengi. Bahati mbaya sina muda, labda siku nyingine nitakuelewesha zaidi...naomba nikuache na hili hapa;

wape somo maccm hao. Sio suala la sample size, pia katika kufikia uamuzi warioba ameeleza wametumia pia ripoti za kamati mbalimabali zilizoundwa kuangalia suala la muungano. Pia taasisi mabali mbali km Bunge na BLW, TEC, Bakwata, CCT, n.k wote walitoa mapendekezo yanayoelekea serikali tatu. Kwa hiyo hiyo idadi ya watu japo inatosheleza sio kigezo pekee warioba ametumia.
 
Le mutuz mimi huwa ckuelewagi kabisa, ebu rudia kusoma hapo juu then jenga hoja


Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app

- ha! ha1 ha! ha! kaka nimeuliza tu maana nimeona kwamba CCM hatuaminiani maana yake ni kwamba Wapinzani wa Tanzania wanaaminiana au nimekosea kaka? ha! ha1 ha!

Le Mutuz
 
Kwani kama 1+1=2 na si tatu, iweje tulilie muungano wa serikali tatu. Me ningemuelewa warioba angekuja na suluhu la serikali moja

Hukumsikia aliposema tulitakiwa twende kwenye serikali moja na ndilo lengo la waasisi. lakini akasema kwa hali ilivyo sasa na maoni ya wazanzibari wengi hilo limeonekana haliwezekani kabisa. Au umeamua tu kujitoa ufahamu. Yaani Chabruma, hakuna hoja yoyote mtakayotoa ambayo warioba hayaitolea ufafanuzi fasaha. Mnabaki kurudia rudia tu mambo ambayo yameshafafanuliwa.
 
MODS, mbona mmebadilisha topic ya uzi wa Hotuba ya warioba leo Bungeni. Hakuna mahali popote kwenye uzi wenye hotuba ya warioba leo Bungeni wakati wachangiaji wamefikia zaidi ya elfu thelathini wanaompongeza warioba?
 
pamoko sana! Jamani tunzeni hizi kumbukumbu kwa ajili ya siku za mbeleni. Mafindofindo na manyofunyofu aliyoyaibua Warioba leo, nikajiona kama sijui kitu............records ni muhimu sana ktk haya maisha
 
Sitanii, hawa watu wanatia wasiwasi kwa sasa. Leo nimetazama hotuba ya Jaji Warioba mwanzo hadi mwisho. Sijaona hata mbunge mmoja kutoka CCM alionyesha furaha, wote walikuwa kimya, walikumbwa na ubaridi, wengine walikuwa wafyonza..mbaya zaidi kuna mahali walikuwa wanashindwa kujizuia na kutaka kuleta lapsha mpaka makamu mwenyekiti anawasihi watulie.

Kuna nini huko ccm? Mmeapishwa nini na chama chenu kiasi cha kukataa maoni ya wananchi? Kikwete ndie aliyeteua wajumbe wa katiba, je walipoanza mchakato wa kukusanya maoni waligeuka wote wakawa CHADEMA,CUF,NCCR,CHAUSTA au UDP kiasi cha kuwasaliti? Warioba ni CCM na mlihakikisha mmeteua wajumbe miongoni mwao wakiwa wanachama wenu watiifu, mojawapo ni Mwenyekiti wa Tume, sasa wapi kakosea step? mbona amefanya kazi nzuri?!....

Tayari mmeshaanza kuropoka kuwa mtatumia wingi wenu kuzishinda hoja za wananchi kupitia tume ya Warioba, nie sio watu wa kawaida, yawezekana watu mnaowatumikia sio sisi, wapo watu wengine katika ulimwengu wa roho mnaoujua nie, hii ni hakika, mmetukataa mchana kweupe, maana yake hamtaki tuione Tanganyika tena, agenda mliyonayo anaifahamu Mungu wenu, sio yule Mungu wa Watanganyika..
 
Bora wapinzani tunajua hawaaminiani na hilo tunaliona wazi, sasa ccm mkiwa chemba mnataka serikali tatu but kwenye media mnataka serikali mbili sasa tutawaelewa vipi? Hapo kuna kuaminiana kweli? Hivi kaka serikali ya tanganyika iko wapi? Katiba yake iko wapi? Na mamlaka yake ndani ya muungano ni yapi? Ebu angalia zanzibar wana katiba yao,nk! Je kwanini tusidai serikali ya tanganyika?


Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom