Mada ni madini matupu. Yastahiki kukaziwa kifungu kwa kifungu:
1. Korona:
(a) "... kuwa maombi ya kusajili vifo kupitia mfumo wa E-Huduma yameongezeka kufikia vifo
112,487 mwaka 2020 ukilinganisha na vifo
35,000 mwaka 2019. Hili ni ongezeko la zaidi ya
200% kwa mwaka."
(b) "Takwimu za Serikali zinaonyesha kuwa kulikuwa na wastani wa vifo
132 kwa wiki vinavyosababishwa na Korona mwezi Aprili 2021. Mwezi uliopita, Julai 2021, kumekuwa na wastani wa vifo
507 kwa wiki. Hili ni ongezeko la vifo vinavyosababishwa na Korona la takribani
300% ndani ya miezi mitatu tu."
(c) "Ni maoni yangu kuwa Waziri wa sasa wa Afya na Naibu wake na Waziri wa sasa wa Katiba na Sheria ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi (aliyebeba ndege ya Serikali kwenda Madagaska kutuletea kilichoitwa dawa ya kutibu Korona), wanapaswa kuwajibika au kuwajibishwa kwa kuwadanganya wananchi na kuleta maafa makubwa nchini."
View attachment 1885023
View attachment 1885026
--------
Tutakuwa tumepoteza na tunapoteza watu wengi kuliko mataifa karibu yote duniani kwa sababu ya upumbavu wa watu wachache.