Hotuba za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Hotuba za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Kwani viwanda na mashirika ambayo wakuu wako wanauza alijenga nani?muulize mzee wako aliesoma bure atakuambia

Hilo ndio lilikuwa moja kati ya makosa yake makubwa. Vilikufa yeye mwenyewe akiwa hai. Wewe ulichukuwe jitu limezaliwa, limekulia, limesomea porini. Mjini kaja kwa kupelekwa chuo kwa upendeleo, halina exposure, halina muono, halijawahi kufanya kazi, ukalipe kiwanda liendeshe? huo ulikuwa ni ujinga mkubwa sana.

Mfano kuna mtu alikuwa kuli wa kubeba mizigo bandarini, kamfanya sijui mshauri wake Ikulu (kama sikosei ni baba'ke Nape Nnauye), hiyo kweli ni akili?
 
Natafuta hotuba za nyerere zikiwa katika audio au video. Mwenye kujua nitazipata wapi anijulishe

Zitafute on the Internet. Mojawapo ni hii hapa chini. Ilikuwa kabla ya muungano. Mwalimu Nyerere anazungumzia umuhimu wa elimu nchini Tanganyika. Video inapoendelea, bila audio, inaonyesha sehemu fulani ya Dar pamoja na watoto nadhani wakiwa nje ya shule ya watoto wadogo au katika uwanja fulani wakicheza. Some of the viewers may be able to recognise themselves when they were pupils at the school or at the playground in the early sixties.

Interview with Julius Nyerere, 1960s - YouTube

"The interviewer is thought to be a member of University of Edinburgh staff and the interview is thought to have taken place in the years shortly after Nyerere was elected Prime Minister of Tanganyika in 1961. Following the interview, there is some silent footage, presumed to have been taken in the vicinity.

We know nothing more about this so would be interested in hearing from anyone who does.

Copyright in this is assumed to rest with the University of Edinburgh. If you think different, please let us know." - (euarchives, Youtube, 19 December 2012).
 
Wewe ndiyo mjinga .kwa sababu ujuwi ulisemalo.hivi Tz hii wapo watu wachache kama wewe wasiompenda nyerere.yule mzee aliipenda Tz sana na alipenda watu wote tuwe na maisha sawa bila kujali dini .ukabila au rangi ya ngozi but nowday kila corner umejaa udini ,ufisadi na rushwa iliyokithili.halfu wewe unamtukana??au baba fisadi nini??
 
Changamoto: tafuteni "best" ya hotuba za nyerere ileteni hapa tuichambue.

btw ningependa sana kusikia hotuba ya nyerere kuhusu demokrasia kama ipo au hata anayolitaja neno demokrasia.
 
Monile wakuu! Mwenye hotuba zake kwa mfumo wowote ule,wa maandishi,audio au video, naomba anisaidie niweze kumsikiliza au anijulishe wapi ntazipata.
 
Zitakujaza ujinga tu. hakuna cha maana utachokipata humo. Kama unabisha zitafute, sikiliza halafu njoo utuambie cha maana ulichokipata.
 
Monile wakuu! Mwenye hotuba zake kwa mfumo wowote ule,wa maandishi,audio au video, naomba anisaidie niweze kumsikiliza au anijulishe wapi ntazipata.

Tafuta za Kikwete ujue mizaha iliyopo ikulu
 
Ila kama utazikosa,mengi aliyosema katika hotuba zake ndiyo yamekua kweli yakitokea... IKULU PANGO LA WALANGUZI,TAIFA KUNUKA RUSHWA,MIIKO YA UONGOZI KUTUPWA,JOTO LA UDINI NA UKABILA,KUKIUKWA KWA KATIBA,WATU KUKICHOKA CHAMA,UKUAJI WA MATABAKA,TIMBWILI LA MUUNGANO,SERIKALI CORRUPT HAIKUSANYI KODI INAKIMBIZANA NA MACHINGA..... yapo mengi sana... Usiwasikilize "waislamu wachache" wenye chuki na husda juu ya Hayati Nyerere..tafuta sikiliza.
 
Zitakujaza ujinga tu. hakuna cha maana utachokipata humo. Kama unabisha zitafute, sikiliza halafu njoo utuambie cha maana ulichokipata.

pamoja na mapungufu yake ya kibidamu, alikuwa genius na misimamo imara alikuwa anajua sana kutumia lugha kwa ufasaha kuifikia hadhira yake
 
nenda pale kwenye ofisi za mfuko wa taasisi ya mwl.nyerere karibu na ifm muone mze josef butiku utazipata zote unazohitaji.
 
Monile wakuu! Mwenye hotuba zake kwa mfumo wowote ule,wa maandishi,audio au video, naomba anisaidie niweze kumsikiliza au anijulishe wapi ntazipata.

TBC wana hotuba zote za Nyerere tangu uhuru mpaka kifo chake.
 
Zitakujaza ujinga tu. hakuna cha maana utachokipata humo. Kama unabisha zitafute, sikiliza halafu njoo utuambie cha maana ulichokipata.

Shetani aendelea kukusaidia!
Pamoja na kwamba huru wa kusema na kutapika huu ujinga ni wako ni bora ukaweka akiba maana mawazo mengine unaweza kusababisha utindo wa ubongo kwa wanao maana watajiuliza u-mama wa aina gani katika dunia hii!
 
Monile wakuu! Mwenye hotuba zake kwa mfumo wowote ule,wa maandishi,audio au video, naomba anisaidie niweze kumsikiliza au anijulishe wapi ntazipata.

Mkuu kuna bwana mmoja yuko Moshi anauza videos za hotuba za Mwalimu Nyerere. Nikipata contact zake nitakufahamisha.
 
Back
Top Bottom