Nimejaribu kujikumbusha lakini nimepata harufu ya chuki binafsi au zenye mzukumo wa kiimani
Maelezo ya wapambe wote uliowanukuu wanatofauti gani na wewe?
Uzuri ni kwamba mtaandika weeeeeeeeee lakini ukweli unabaki palepale hata 1000 ijayo kuwa J.K.Nyerere aliku Rais wa Kwanza wa Tanganyika na mzalendo kuliko yeyote yule!
Hivi inaingia akilini unaleta stori za Mhaini na kuita hoja za kujadiliwa?
Na miaka ishirini baada ya yeye kuondoka madarakani, tumekuwa matajiri duniani?Onyesha cha maana kimoja cha Nyerere tukijadili halafu tuone kweli kina maana? angekuwa na maana angeiacha hii nchi baada ya miaka 24 ya kutawala kidikteta, kuwa maskini duniani?
Zitakujaza ujinga tu. hakuna cha maana utachokipata humo. Kama unabisha zitafute, sikiliza halafu njoo utuambie cha maana ulichokipata.
ni we mwenyewe au umelogwa?
Mkuu kuna bwana mmoja yuko Moshi anauza videos za hotuba za Mwalimu Nyerere. Nikipata contact zake nitakufahamisha.
ni we mwenyewe au umelogwa?
Haya wewe ambae "hujalogwa" tuoneshe kimoja cha maana ulichokisikia kwenye hizo hotuba.
Anapatikana nje ya posta kuu ya mjini Moshi, anatumia gari lenye kila aina ya video na vitabu vya hotuba zake.
FaizaFoxy una maoni gani kuhusu Rais Mh. J.K. kuwashauri wananchi kuskiliza hotuba za nyerere?
Alisema haya jana huko Iringa wakati wa maadhimisho ya kumbu kumbu ya kifo cha Mwl. Nyerere.