Housegirl alipwe Mshahara wa elfu 80 hadi laki 3

Watu wana comment utadhani hawapo Tanzania,au hapa JF tupo ulimwengu nje ya TZ?? Maana hata juzi tu kuna uzi uliletwa kuomba serikali iingilie kati shule ya sec iliyopo kagera inalipa Laki na nusu kwa walimu...
 
Hapo saaa ni makubaliano yenu ninyi wawili, umlipe 100k ila kila kitu ajitegemee cha kwako ale chakula tu ila matumizi binafsi kama hizo losheni, pedi, sijui kisuka afanye mwenyewe. Wewe unakuwa unafanya mara mojamoja ukipata nafasi
Sawa
 
Watu wana comment utadhani hawapo Tanzania,au hapa JF tupo ulimwengu nje ya TZ?? Maana hata juzi tu kuna uzi uliletwa kuomba serikali iingilie kati shule ya sec iliyopo kagera inalipa Laki na nusu kwa walimu...
Huwa wanajikuta sijui kina nani! Ukihesabu wenye uwezo wa kuwalipa hao housemaids hizo pesa utakuta hata 2% hawafiki! Wanashindwa kuendana uhalisia kabisa!

Hao waajiri wa waalimu kwenye uzi wangu wamelundikana na hiyo mishahara ya 150k hakuna anayefatilia wanaishije na kulisha familia zao, ila hapa kuhusu hg wametukalia kooni wataishije na blabla kibao! Kuna mtu analipwa pesa hata kusave 50k hawezi pesa inaishia, sembuse huyu hawazi pa kula wala kulala?
 
Wewe au mtoto wako anaweza kukubali kulipwa 2700 kwa siku?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…